UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI



 










Mfumo wa kilimo shadidi cha mpunga (MKiShaMpunga) unaojulikana kwa Kimombo kama ‘Sytem of Rice Intensification’ au ‘SRI’ kwa ufupi unajumuisha mbinu  vumbuzi za kilimo ambazo kwa sasa zimeendelea kupata umaarufu kote duniani. Mfumo wenyewe ulibuniwa kwa mara ya kwanza nchini Madagascar yapata zaidi ya miaka ishirini (20) iliyopita kupitia juhudi za Padri Henri De Laulanié. Mfumo shadidi ulivumbuliwa kutokana na juhudi za majaribio na wakulima pamoja na uvumbuzi wa mashirika ya nyanjani nchini humo. Habari za kuthibitishwa kutoka kwa mashamba ya wakulima zinaonyesha kuwa taratibu za mbinu MKiShaMpunga yaani “SRI” zinaongeza kiwango cha mazao ya mpunga zikilinganishwa na njia za kawaida zilizotumika ikiwemo pamoja na kuboreshwa kwa mbinu za ukuzaji.



Umuhimu wa Mfumo wa Kilimo Shadidi cha Mpunga
1. Gharama ya kulimia ni ya chini sana,
2. Kiwango kidogo cha mbegu kutumika (kilo 2 hadi 3 kwa ekari),
 3. Eneo la mita 40 mraba kwa ekari moja ya bustani ya miche linatosha,
4. Mche mmoja kwa kila tuta hutumika,
   5. Matuta kumi na sita (16) peke yake kwa mita moja mraba, 6. Mahitaji ya ufanyikazi kwa upaliliaji hupunguzwa,

  7. Ukuwaji wa mimea na mizizi utaboreshwa kupitia njia ya upaliliaji,
8. Maji ya Kuelea kwa shamba kwa muda murefu hayatahitajika,
  9. Asilimia 40 hadi 50 ya maji ya kumwagilia yanahifadhiwa,
10. Matumizi kidogo ya nguvu za umeme wakati wa umwagiliaji maji iwapo unahitajika
12. Idadi kubwa zaidi ya mizizi mieupe inayotumia maji kidogo,14. Kiwango cha juu cha uchipuzi wa mikombo na vichwa vya nafaka,
15. Mazao mengi yanayotokana na na idadi kubwa ya mikombo (tillers),  vichwa vya nafaka (productive tillers) na nafaka yenyewe,
16. Mimea kustahimili kuanguka au kulala chini kwa sababu ya upepo mkali au kimbunga.






                                 
Utaratibu wa Mfumo wa Kilimo Shadidi cha Mpunga Bustani ya miche 
Panda miche michanga kwa uangalifu katika mazingira ya udongo ulio na hewa ya kutosha, isizame katika udongo uliolowa maji. Kwa kuwa idadi ya miche itakuwa chache katika mfumo huu wa ukuzaji mpunga, unaweza kutumia bustani iliyoinuliwa (kwa muinuko) kwa ukuzaji wa miche Image result for system of rice intensificationImage result for system of rice intensification
  • Kiwango cha mbegu kinachopendekezwa ni kilo 3 kwa ekari moja
  • Mita 40 mraba ya bustani iliyoinuliwa inatosha kwa upanzi katika ekari moja.
  • Tengeneza bustani ya kuinuka kima cha sentimita 5 kwa kila 1m x 5m, yaani na bustani 8         zinahitajika kwa sehemu ya 40m2
  • Matumizi ya ya mbolea asili (samadi) ya shambani iliyoiva vizuri yafanywe kwa uangalifu
  • Usitumie mbolea ya ziada baadaye kwa bustani iliyoinuliwa kwa udongo ulio na rotuba ya kutosha. Lau sivyo weka mbolea ya dukani ya ‘DAP’ kiasi cha gramu 760 kwa kila ekari (gramu 95 kwa kila bustani ya 5m2 iliyo muinuko pamoja na udongo.
  • Tandaza magunia yaliyokuwa ya mbolea ya dukani (polythene bags) juu ya bustani kwa ulainifu.
  • Jaza udongo ukilainisha juu ya magunia hayo kwa kima cha mpaka sentimita 4 kwa urefu.
  • Mbegu zihifadhiwe na dawa ya ‘Pseudomonas’ kwa kiwango cha gramu 10 kwa kila kilo ya mbegu 
  • Tumia gramu 200 za mbolea asili ya ‘Azophos’ kwa kila kilo 3 za mbegu • Changanya ‘Pseudomonas’ na mbolea asili ya ‘Azophos’ na mbegu za mpunga kwa kutumia mchanganyiko wa mpunga huo na maji kwa masaa 24.
  • Weka mbegu hizo kwa masaa 24 katika magunia ya mikonge kwa minajili ya uchipuzaji.
  • Panda gramu 375 za mbegu iliyooteshwa katika kila mita 5 mraba (5m2 ) ya bustani iliyoinuka.
  • Mwagilia maji kwa kutumia nyungu ya maua au mkebe. Maji ambayo husimama kando kando ya bustani iliyoinuka yaweza kutumika.
  • Funika bustani kwa kutumia mali ghafi inayopatikana kirahisi popote ulipo kama vile vifufu vya nazi, mabua ya mpunga na uiondoe siku 3 baada ya kupanda mbegu iliyooteshwa. Baada ya juma moja iwapo ukuaji wa miche ni mdogo, weka 8

  Utaratibu wa Mfumo wa Kilimo Shadidi cha Mpunga
 Usimamizi wa miche
  • Ng’oa miche pamoja na udongo wake kutoka kwa bustani ili miche iweze kunawiri kwa haraka
  • Usumbufu kidogo wa mizizi wakati wa kung’oa utasaidia sana miche kukua kwa haraka.
  • Panga miche katika kisanduku cha mbao na ukisafirishe hadi shambani utakapopandia, ili unapopanda kutawanisha miche itakuwa rahisi.
Eneo la Bustani na kiwango cha mbegu (kwa Hekta) Njia ya Uzalishaji Eneo la bustani (Kwa mita mraba) Kiwango cha mbegu(kwa kilo) Idadi ya miche katika mita moja mraba * * Upandaji wa kawaida 800 50 2500 Mfumo shadidi wa upandaji mpunga(SRI) 100 7.5* 375 *Kulingana na uzito wa mbegu 1000 kiwango cha mbegu ya kupanda kitatofautiana, hata hivyo, kilo 7.5 ndicho kiwango cha juu zaidi kinachohitajika. * * mbegu za mpunga 1000 zina uzito wa wastani wa kiasi cha gramu 20. Viotesho (au bustani) vya miche vyaweza kutengenezwa kwenye sehemu iliyotengwa kwenye shamba la kupandia, au hata karibu na nyumba ya mkulima kwa ajili ya ulinzi na usimamizi mwema. Wakati wa kuhamishia miche kwenye shamba la kupandia, ipangwe kwenye vijisanduku vidogo ili kurahisisha usafirishaji. Ni sharti miche isipitishe zaidi wa muda wa dakika thelathini (nusu saa) kabla ya kupandwa. Mbinu hii ya kukuza miche na kuisafirisha husaidia kuokoa wakati kati ya bustani na shambani.    

                             Eneo la Bustani na kiwango cha mbegu (kwa Hekta)
                                                                                                                              Idadi ya miche katika
Njia ya Uzalishaji                    Eneo la bustani        Kiwango cha mbegu           mita moja mraba
                                               (Kwa mita mraba)          (kwa kilo)
                                                                     
                                               
                                             
Upandaji wa kawaida;                     800                             50                                          2500



Mfumo shadidi wa
upandaji mpunga(SRI)                      100                            7.5*                                         375



  • Kulingana na uzito wa mbegu 1000 kiwango cha mbegu ya kupanda kitatofautiana, hatahivyo, kilo 7.5 ndicho kiwango cha juu zaidi kinachohitajika.
  • mbegu za mpunga 1000 zina uzito wa wastani wa kiasi cha gramu 20.

  Shambani kupandikiza
  •   Lainisha/sawazisha shamba la kupandia vizuri. Yaani ni muhimu sana iwe tambarare.
  • Mbegu zenye nguvu zikipandwa katika shamba lisilosawazishwa zina nafasi kubwa ya kuoza.  Hivyo basi, epuka kupanda katika shamba lisilolainishwa.
  • Tengeneza mitaro midogo kwa minajili ya kurahisisha mkondo wa maji.
  • Hatua ya cha sentimita 25 mraba (25cm x 25cm) kutoka tuta la mmea hadi mwingine kwa upanzi  inapendekezwa

                            Upanzi wa kimrabaImage result for Picha za kilimo shadidi cha mpunga
  •   Ni sharti mche mmoja peke yake upandwe kwa kila tuta.
  • Usipande katika shimo la kimo cha ndani sana.
  • Upandaji mraba wa sentimita 25 x 25 huhakikisha nafasi ya kutosha
  • Katika upandaji huu kifaa cha kutia alama kinachozunguka (rolling marker) au kamba iliyowekwa       alama vinaweza kutumiwa kwa upanzi ili kupata vipimo halisi.

                    Usimamizi wa umwagiliaji maji
  • Hakikisha hakuna maji ya kusimama katika shamba la kupandia na pia udongo uthibitiwe katika hali ya unyevu au ukavu.
  • Mwagilia maji mpaka kina cha 2.5cm baada ya mistari ya mipasuko kutokea kwenye udongo. Wakulima wa Mwea (Kenya) wameona kwamba itachukua siku saba baada ya kumwagilia maji ili udongo upasuke. Kwa njia hii, itabidi basi kumwagilia maji kwenye shamba kila baada ya siku saba hadi mpunga uanze kuzaa (Panicle Initiation) ambapo utamwagilia shamba mara tu kidimbwi cha maji shambani kinaponyauka.
  • Badilisha zamu za kulowesha na ukaushaji ili hewa ipenye kwenye udongo na kuongeza ukuwaji wa mizizi na kuendeleza utendaji kazi wa vijiumbe (micro-organism
       
                                      Upaliliaji unaotumia mashineImage result for Picha za kilimo shadidi cha mpunga
  • Utumiaji wa mashine ya kupalilia ni mojawapo ya hatua muhimu sana katika mfumo huu maalum. Mashine za kupalilia zinatumika kila baada ya muda wa siku kumi tangu siku ya kupandikiza miche (jumla ya mara nne kwa uhai wa mpunga shambani).
  • Vibarua watatu wanatosha kupalilia ekari moja kwa mara moja (kwa siku moja).
  • Kwekwe hukanyagwa na kuoza na kuwa mbolea.
  • Kiwango cha maji ni sharti kiangaliwe vilivyo kwa matumizi ya mashine.
  • Kwekwe zilizoachwa baada ya kupalilia ni sharti ziondolewe kwa mikono. mara, udongo husumbuliwa, jambo ambalo lina manufaa kwa kilimo.

  Faida za Mfumo wa Kilimo Shadidi cha Mpunga
  • Upandikizaji wa miche changa na yenye nguvu na imara, inayostawi kwa haraka bila kuwa na  mshutuko wowote unaoletwa na kuhamishwa toka kwenye bustani hadi shamba la kupandikizwa.
  • Kiwango cha ukuwaji wa mizizi ni bora zaidi kuliko mbinu ya kawaida
  • Uwezo mkubwa wa miche kuchipuza, kukua na kutoa mbegu
  • Utendakazi wa majani ya mimea kutengeneza chakula cha mmea (photosynthesis) huongezeka kwani majani huwa kijani kibichi hata mpaka wakati wa majira ya kuvuna.
UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI UFAHAMU MFUMO WA KILIMO SHADIDI Reviewed by BENSON on March 08, 2018 Rating: 5

No comments