KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO.
Viazi mviringo au Viazi Ulaya ni zao ambalo la asili,
pia zao hili ni miongini mwa mazao jamii ya mzizi (tuberous crop) na
linalodumu, kwa jina la kitalaam linaitwa Solanum tuberosum .
Neno “Kiazi” linatokana na maana ya mmea ambao una aina
“tuber ” yaani chenyewe. Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara
katika nchi nyingi zinazoendelea. Viazi hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu
hadi mitano. Viazi mviringo vina virutubisho vingi mfano vitamin, protin,madini
na maji.
Asili yake.
Viazi mviringo kwa mara ya kwanza viligundulika huko
kusini mwa nchi ya Peru na kufuatiwa kaskazini magharibi mwa nchi ya Bolivia
kati ya miaka 8000 na 5000 kabla Yesu hajazaliwa (BC). Na vimekuwa viki sambaa
kwa kasi katika maeneo tofauti duniani na kuwa zao la chakula katika nchi
nyingi. Hapa Tanzania viazi mviringo kuzalizwa katika maeneo yenye miinuko ya
kaskazini kama vile Arusha, Moshi, Lushoto na meneo ya kusini yenye miinuko
kama vile mkoa wa Njombe, Iringa, Mbeya na mkoa wa Songwe. Pia maeneo ya
Morogoro yenye miiunuko hususani Tarafa ya Mgeta yameonekana kuweza kuzalisha
zao hili kwa wingi.
Aina za viazi.
Viazi mviringo vipo aina mbalimbali zilizoingizwa Afrika Mashariki kutoka Ulaya
ambako huzalishwa kwa wingi.
Aina hizo ni kama ifuatavyo:
1. Dutch Robijn – kutoka Holland
•inavumilia kidogo ugonjwa wa ukungu
• hushambuliwa sana na Mnyauko Bakteria
• hupendwa na walaji wengi.
Roslin – kutoka Scotlland
•ngozi yake ni nyeupe
•dani ni nyeupe
• huvumulia ugonjwa wa ukungu.
Kerr’s Pink –
•ngozi yake ni nyeupe au nyekundu
•ndani ni nyeupe
•hushambuliwa sana na ukungu na Mnyauko Bakteria.
2. Atzimba – kutoka
Mexico
Huvumilia ugonjwa wa ukungu
Uyole: Kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole kuna aina kama baraka,
sasamua, tana, subira(EAI 2329), Bulongwa, kikondo(CIP 720050).
Hali ya hewa ifaayo kwa kilimo cha
viazi.
Viazi Mviringo hustawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700
juu ya usawa wa bahari. Viazi huhitaji mvua za kiasi cha sentimita 25 kwa wiki
ambazo hutakiwa kuendela kwa muda wa miezi 3 .5 hii huweza kukuza viazi na
kupata mavuno mazuri, pia hutoa mavuno mengi kwenye udongo usio mzina na
unaopitisha maji kiurahisi, na uwe na rutuba.
Utayarishaji wa shamba.
Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75
kutoka tuta hadi tuta, hii husaidia kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi
nzuri wakati wa upanukaji wa viazi. Inashauriwa pia kama matuta hayajatumika
basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini kwenye shina
ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo mavuno
huongezeka.
Utayarishaji wa mbegu.
Tumia viazi vyenye umbile dogo kama mbegu, hutakiwa kuwa
na upana wa yai au upana wa sentimita 3 – 6. Kiasi cha robo tatu za tani
huhitajika kuotesha ekari 1 sawa na tani 1.85 kwa hekta 1. Mbegu hazitakiwi
kuhifadhiwa kwenye giza nene kwani zitaanza kutoa vichipukizi virefu vyeupe.
Sifa za mbegu bora za viazi.
1.Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja.
2. Ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi
zaidi ya manne.
3. Zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa.
4. Zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa
kama vile ukungu na mnyauko.
4. Zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la
kuku.
Upandaji.
Viazi hupandwa kipindi mvua zinapotaka kuanza, kuchelewa
kuotesha kutapunguza kipindi cha ukuaji wa ile mizizi ili iwe viazi na hivyo
kukabiliwa na kipindi cha ukavu. Uoteshaji hufanyika kwa mikono na mbegu
ziwekwe chini udongo kwa kina cha sentimita 10.
Kama mbegu zitaoteshwa bila matuta basi zioteshwe kwa kina
cha sentimita 15 na kufunikwa na udongo mchache na wakati wa palizi udongo
utaongezwa ili kuongeza utoaji wa viazi kwa wingi. Nafasi ya kuotesha ni
sentimita 75 toka mstari hadi mstari na sentimita 23 – 30kwa mche hadi mche.
Mbolea.
Kama kuna uwezo wa kupata mbolea ya asili (samadi au
mboji) ni vema kutumia. Mbolea za viwandani zinazotakiwa ni zile zenye
Nitrogeni kwa kiasi cha kilo 22 – 45 kwa ekari; zenye Chokaa P2O5 kwakilo 45 –
65 kwa ekari. kwa mbolea za viwandani tumia kilo 300 au mifuko 6 za mbolea ya
TSP kwa hekta moja, na kilo 300 mifuko 6 za mbolea ya CAN au kilo 400 mifuko 8
ya S/A au kilo 175 mifuko 3.5 za UREA.
Upaliliaji na unyevunyevu.
Zao la viazi likioteshwa kwa nafasi zilizoshauriwa basi huweza kufunika ardhi
yote na hivyo kugandamiza magugu, hii husaidia kwa kipindi cha wiki 6 za
mwanzo. Katika mpando wa matuta, basi huwa ni kuondoa magugu na kujaza udongo
kwenye mashina.Palilia viazi wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. Inulia
udongo kufanya tuta zuri ili pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi
kutokana na mwanga wa jua.
Maginjwa ,Wadufu & Magonjwa
Ukungu
Ili kuzuia ugonjwa wa ukungu tumia Ridomil, changanya gram 100 za dawa katika
lita 20 za maji na nyunyuzia mara baada kila wiki mbili au tatu kutegemea na
hali ya hewa.
Nyunyuzia dawa ya karate kiasi cha mililita 20 mpaka 40 za
dawa katika lita 20 za maji ili kuzuia wadudu kama inzi weupe na wengine. Tumia
mbinu bora za kilimo kama usafi wa shamba au kilimo mzunguko kama mbinu ya
kuzuia magonjwa na wadudu.
Wadudu
Vidukari:-Ni wadudu wadogo wanoshambilia majani na mashina
kwa:
1. kufyonza utomvu na kusababisha kunyauka kwa mmea.
2. Majani kujikunja kuelekea juu.
3. Majani kuwa magumu
4. Mimea kudumaa
5. Pia hubeba vimelea aina ya virusi ambao huathiri mimea.
6. Pia hueneza ugonjwa wa virus.
Kuzuia: – Wakati wa utunzaji wa mbegu za viazi ni muhimu
kupiga dawa ya wadudu ili kuepuka kupuliza shambani kwani dawa nyingi itapotea.
Nondo wa viazi:
Wadudu huathiri viazi vilivyooteshwa wakati ambao sio wa
msimu wa viazi. Viwavi wanaoanguliwa huingia ndani ya viazi na kusababisha
kuoza. Pia huingia ndani ya viazi wakati vikiwa stoo.
Kuzuia: Otesha viazi katika kinachoshauriwa au zaidi ya sentimita 3
kwani kiwavi aingiae ndani ya hawezi kuchimba kina kirefu na inulia matuta
wakati viazi vinakuwa, hii husaidia kuzuia nondo kutaga mayai.
Minyoo fundoo.
Hushambulia viazi vilivyoachwa kwa muda mrefu ardhini na kwenye ardhi
iliyoathirika na mmomonyoko.
Kuzuia.
1.Usioteshe mbegu ambazo zimeshambuliwa na wadudu.
2. Andaa shamba mapema ili masalia yote ya mazao yaweze kuoza ili kutoruhusu
makazi ya minyoo fundo.
Mbawakavu: -Ni wadudu wadogo ambao hutafuna majani na kuacha matundu
matundu.
Kuzuia: Tumia dawa aina ya Malathion, Thiodan.
Uvunaji.
Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka
kupanda. mda wa kuvuna unategemea na mda wa kupanda na dhumuni la zao. Uvunaji
wa viazi hufanyika kwa kutumia jembe la mkono, viazi vikishang’olewa kutoka
chini ya udongo visiachwe kwa muda mrefu kwani vitabadilika rangi na kuwa
kijani.
Ili kuifanya ngozi ya viazi kuwa ngumu na isiharibike
kirahisi basi mashina yote yanyofolewe wiki 2 – 3 kabla ya kuvuta viazi juu ya
udongo. Baada ya viazi kuvunwa haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwani huanza
kuchipua.
Viazi huweza kuhifadhiwa kwenye ardhi, lakini si zaidi ya
wiki 6 kwani vitakabiliwa na magonjwa na kushambuliwa na minyoo fundo.
Kuvitunza viazi ardhini utahitajika kuvifunikia na nyasi ili visibadili rangi
ya ngozi kwa kupigwa na jua, usiache viazi shambani bila kufunika kwa nyasi au
udongo kwa mda mrefu.
Uhifadhi
Viazi vya chakula viiafadhiwe kwenye ghara hewa ya kutosha pasiwe na
unyevunyevu na joto kali, Viazi vilivyowekwa ghalani visilundikwe kwa kina
kirefu, visambazwe ili visipate joto.
Asante sana kwa kusoma makala haya,
nikutakie siku njema na kazi njema.
KILIMO BORA CHA VIAZI MVIRINGO.
Reviewed by BENSON
on
July 25, 2017
Rating:
Nashukuru kwa elimu uliyotoa, swali langu, Je kwa ekari kama viazi vimestawi vizuri unaweza pata mavuno kiasi gani?
ReplyDelete