MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA WAKATI UCHAGUZI WA ENEO LA KULIMA TIKITI MAJI.
Matikiti
maji husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto
kali sana, baridi kali, mvua nyingi wala udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya
fangasi na wadudu waharibifu.
Joto: Matikiti hukua
vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21 - 30 sentigradi.
Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za
sentigrade huchelewa kuota.
Mvua: Matikiti maji
yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400 - 600 kwa msimu. Mvua nyingi
husababisha uwepo wa magonjwa ya fungasi na bakteria ambayo huathili
mavuno.
Hali
ya Udongo:
Kilimo cha matikiti huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho.
Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa.
Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una
uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
Mikoa
ya Tanzania:
Kilimo cha matikiti maji kinakubali vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko
kidogo kama DSM, Tanga, Morogoro, Mtwara, Lindi na Pwani ambapo kuna jua la
kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu mpaka wa
tisa.
MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA WAKATI UCHAGUZI WA ENEO LA KULIMA TIKITI MAJI.
Reviewed by BENSON
on
October 25, 2017
Rating:
No comments