KILIMO BORA CHA EMBE
Zao la embe hustawi
vizuri katika maeneo ya tambarare na miinuko kati ya futi 0-600 usawa wa bahari. Kiwango cha
wastani cha mvua inayohitajika kwa kilimo cha embe ni mililita 650 hadi 1850 kwa
mwaka. Miembe hustawi katika udongo wenye uchachu (ph) kati ya 5.5 na 7.2.
udongo wenye chachu Zaidi huwa na upungufu wa madini mbalimbali ikiwemo
Zinki, Chuma, Fosforas na Kalsham.
KUANDAA MASHIMO
Kuchimba mashimo
mapana kutafanya udongo uwe laini ili kusaidia mizizi kuzaliwa kwa wingi, upana wa shimo uwe
sentimita 60x60 upana kwa urefu, kwa maeneo yenye udongo mgumu na miamba ya mawe
kipimo kiwe sentimita 100x100 upana na urefu. Uchimbaji wa mashimo uwe wa
kutengeneza udongo katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni udongo wa juu
wa kina cha sentimita 30 na sehemu ya pili ni udongo sentimita zilizobaki
za kina cha shimo.
MBOLEA ZA KUPANDIA
Tumia mbolea samadi
au mboji iliyoiva vizuri debe moja hadi mbili kwa shimo, changaya mbole na udongo wa kwanza
kutoka shimoni, iwapo itatumika mbolea ya viwandani kama DAP, TSP, NPK au
Minjingu Phosphate changanya mbolea hiyo na udongo wa juu wenye mboji (top
soil).
UPANDAJI
Panda miche ya
miembe katika misimi ya mvua za mwaka, au wakati wowote iwapo inatumika njia ya umwagiliaji kwa
vipindi visivyo na mvua. Weka maji ya kutosha wakati wa upandaji ili kuimarisha
mshikamano wa udongo na unyevu.
KIPIMO
Miembe hupandwa katika vipimo tofauti kutegemeana mipango ya
matumizi ya ardhi husika na miundombinu ya shamba. Upandaji
unaweza kuwa wa miti 160 hadi 1300 kwa hekta moja. Vipimo vya umbali
kati ya mti ana mti vifuate mistari iliyonyooka. Kipimo cha wastani kwa
wakulima wadogo na wakati ni mita 8x8, mita 6x8, mita 4x8, mita 4x7 au mita
5x7. Wastani kwa hekta ni miembe 200-400 ujazo wa vipimo vingine vinaweza
kufikia miti 1200 na Zaidi kwa hekta. Matumizi kwa vipimi hivyo vinahitaji
ushauri wa mtaala, kabla ya kutumia.
UKATIAJI
Ukatiaji hufanyika
katika hatua ya kwanza ya ukuaji miti ukifikia urefu wa sentimiti 60-100, ukatiaji wa kwanza
utatofatiana na ukatiaji wa pili na kuendelea. Ukatiaji wa kwanza, kata sehemu majani
yanapopishana ili kupata umbo la mti unaopishana kutoka katika chanzo cha tofauti. Ukatiaji wa pili na kuendelea kata sehemu
ya juu ya pingili ya tawi ili
kupata matawi mengi.
MAGONJWA NA WADUDU
Miembe hushambuliwa
na magonjwa kama Ubwiru unga (powder mildew), Chule
(Antharacnose),
magonjwa mengine hutokea kwa mara chache sana. Wadudu mbalimbali wanaoshambulia mazao
tofauti, hushambulia miti ya miembe kama Vidukari, Vung’ata, Kifaurongo, Mbawa
kavu, nk.
UDHIBITI WA MAGONJWA NA WADUDU
Fanya usafi wa palizi shambani kila inapolazimu ili kupnguza
vyanzo wa wadudu na magonjwa, matumizi ya dawa
yanafanyika kila dalili za ugonjwa zaitakapo jitokeza au mashambulizi ya wadudu
yatakapoonekana.
UKATIAJI MKUBWA
Miembe inapokuwa
katika hatua ya uzalishaji huhitaji kukatiwa kila imaliziapo hatua ya uvunaji na kujiandaa
kwa uzalishaji katika msimu ujao. Ukatiaji huu huwezesha mti kuchipua majani
mapya kwa pamoja na kukomaa kwa pamoja, hatimae hutoa maua kwa pamoja kwa
wakati unaokusudiwa.
URUTUBISHAJI NA MBOLEA
Mbolea ni muhimu
katika uzalishaji wa embe, mbolea huendelea kutumika
wakati wa kukuza
miche na kuzalisha matunda. Mbolea zinazotumika ni N.PK, MOP, Urea,
Minjingu, Samadi, Mboji, Chokaa na virutubisho visaidizi. Mbolea zitawekwa kulingana na mahitaji ya
udongo na kwa wakati maalum, uwekaji holela wa mbolea unaweza ukaathiri
uzalishaji utakaotokana na ukosefu wa maua.
UVUNAJI NA UHIFADHI
Embe zitunzwe
zikiwa zimekomaa, embe lililokomaa lina umbo tofauti kulingana na aina ya embe, kiashiria
kikuu ni embe kubonya kwa eneo la kikonyo, alama nyingine ni kubadilika kwa rangi
ya ndani ya nyama ya embe kutoka nyeupe kuwa njano hafifu.
Embe zinazovunwa
zioshewe kwa maji ya moto na kuhifadhiwa sehemu kavu na
salama, chagua embe
na kuziweka katika madaraja mfano daraja la 1 na daraja 2. Hii itakusaidia
kujua ipi embe ni tayari kwa kupeleka sokoni.
KILIMO BORA CHA EMBE
Reviewed by BENSON
on
August 30, 2017
Rating:
Nahitaji miche ya miembe ya muda mfupi tafadhali. Niko dar
ReplyDeleteKuna mtaalam mzuri sana yuko Morogoro anazalisha miche iliyopandikizwa na ya muda mfupi. Ukihitaji mawasiliano yake naweza kukupatia
DeleteNaomba unipatie
DeleteNahtaj Miche ya maembe tanga ,embe za India na za muda mfupi
ReplyDeleteNipo Lindi
Unaweza niunganisha na huyo mtaalamu wa morogoro wa maembe ya muda mfupi?
ReplyDeletenipatie tafadhali
DeleteUtaalam huo umesambazwa katika maeneo yote ambayo maembe yanaweza kustawi
ReplyDeleteMtaalamu nisaidie , mda gani sahii wakuwekea miembe mbolea. Na udogo upi unahitaji mbolea gani.
ReplyDeleteKwa atakae hitaji miche ya embe ya muda mfupi,karibu SUA,horticultre tukuhudumie.
ReplyDelete+255719527062
Miembe yangu inashambuliwa na funza kwenye matunda cjui vinavyosababisha ni nn
ReplyDelete