NUFAIKA NA KILIMO CHA TIKITIMAJI NA FAHAMU SOKO LAKE
Tikitimaji ni zao la kitropiki linalo
tumia siku 65-90 kutoka kupandwa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu
uliyotumia na hali ya hewa ya eneo husika kwani maeneo ya pwani na
yenye joto sana tikitimaji na mazao mengine hukomaa mapema ukilinganisha
na maeneo ya milimani yenye baridi kwa hiyo tunashauri kama unataka
kulima tikitimaji basi tafuta sehemu zenye hali ya hewa nzuri kuendana
na mahitaji yako na soko lako lilivyo
ENEO
Chagua eneo ambalo halina historia ya
kuwa na magonjwa au wadudu wanaoshambulia tikiti maji.Eneo ambalo maji
yanapatikana kwa urahisi kwa ajili ya umwagiliaji wa tikiti maji ,pia
eneo lisilo na udongo wenye chumvi chumvi na unaotuamisha maji soma hapa
kujua aina za udongo. tikiti maji linastawi sana katika udongo tifutifu na kichanga lakini
udongo wa mfinyanzi sio mzuri sana kwa tikiti maji kwani husababisha
matunda kuwa na nyufa(cracks)
KUANDA SHAMBA.
Lima shamba lako vizuri kwa kuvunja
vunja udongo na pia andaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu kwenda
juu sentimita 30 ili kusaidia mizizi ya tikiti kukua vizuri na kuzuia
maji kutuaama hasa katika kipindi cha mvua.mfano wa picha kwa uandaaji
wa shamba
Nikaribishe kwenye shamba lako nikupe utaalamu namna ya kuandaa shamba kwa ajili ya kilimo hiki na mazao mengine
MFANO WA MASHAMBA YALIYOLIMWA VIZURI TAYARI KWA KUPANDA |
MAHITAJI YA TIKITIMAJI
Tikiti linakua vizuri katika udongo
unaoshika maji vizuri lakini yasio tuama na kuruhusu mzunguko mzuri wa
hewa na maji.Udongo wenye pH 5.8-6.6.pia kama pH ni ndogo tutakushauri
cha kufanya ili iweze kuwa nzuri na ya kiasi kwa ajili tikitimaji. Tikiti halistawi vyema ktk baridi na linahitaji joto la udongo kiasi cha 18-29 0c. Joto
chini ya 18 0c na juu 29 0c litaathiri kuota kwa mbegu na ukuaji wa
mmea.Katika kipindi cha ukuwaji tikitimaji linahitaji unyenyevu wa
udongo wakati wote lakini maji yakizidi katika udongo wakati wowote wa
ukuwaji na uwekaji wa matunda hupelekea upasukaji wa matunda na
kupunguza mavuno na ubora wa matunda.
UPANDAJI
Mbegu/mche wa tikiti maji utapandwa mita
1-2 kati ya mmea na mmea na uwekwa sentimita 2.5 kwenda chini(shimo la
kupandia), na kati ya mstari na mstari iwe mita 2,kwa umbali huu panda
mbegu 2 kila shimo.Au weka umbali wa sentimita 50 kwa mita 2 lakini hapa
panda mbegu moja moja. katika hekari moja utahitaji mbegu gramu
500gms-600gms
DOUBLE ROW PLANTING |
SINGLE ROW PLANTING |
Mbegu ya tikitimaji utokeza baada ya siku 5-7.
UTUNZAJI WA MMEA.
a) Mbolea.
Mbolea ya samadi kwa kiasi cha 4-6 tani
kwa ekari,ichanganye na udongo wiki moja kabla ya kupanda,pia mbolea hii
unaweza iweka katika kila shimo siku kadhaa kabla ya kupanda kisha
mwagilia ili kupunguza kiasi kikubwa kitakacho hitajika kuweka katika
ekari moja.Kama huna samadi tumia Yaramila winner au DAP weka gram 5 kwa
kwa kila shimo ,hakikisha mbolea na mbegu havigusani.
Wiki mbili baada ya miche yako kutokeza
weka mbolea ya kiwandani -N-P-K (Yaramila winner) gram 5 tena kwa kila
shimo,hakikisha unaichimbia chini na isigusane na mmea.
Weka mbolea yenye Calcium kana Yaramila
nitrabo gram 10 kwa kila shina unapoona matunda yameanza ili kusaidia
kupata matunda makubwa na mazuri.
UMWAGILIAJI
Maji kwa sentimita 1-5 katika udongo
yanatakiwa kwa mvua au umwagiliaji ili kupata tikitimaji zuri,kipindi
cha muhimu sana kwa mahitaji ya maji kwa tikitimaji ni :kabla ya mche
kutokeza ,mwanzo wa kutoa maua na siku 10 za mwisho kabla ya kuvuna.Maji
machache kipindi cha kupanda husababisha kutoota kwa mbegu,kipindi cha
kuweka maua husababisha matunda machache kutokeza na matunda kukosa
maumbo yake.Siku 10 za kuelekea kuvuna husababisha matunda kuwa madogo
kama maji ya kutosha yasipopatikana.Matunda yakielekea kuiva punguza
umwagiliaji maana kiasi kikubwa cha maji kitasababisha kiasi kidogo cha
sukari kutengenezwa na kupasuka kwa matunda, pia kumbuka kweka mfumo wa
utoaji maji shambani yaani drainage sytem(nitakuonyesha zaidi nikifika
shambani kwako) hii itasaidia kuondoa chumvi na kuhakikisha mazao
yanastawi vizuri
Angalizo:
Usimwagilie jion sana hii itasababisha
kukua kwa magonjwa kwa sababu ya kuacha majani ya mmea yakiwa na
unyevunyevu .Pia angalia wakati mzuri wa uchavushaji /wakati ambao
nyuki wanakuwepo shambani mwako hivyo jitahidi kumwagilia mda ambao
hautawasumbua nyuki.
Matandazo.
Ni muhimu kutumia matandazo katika
shamba lako ili kusaidia kutunza unyevunyevu katika udongo na matandazo
haya baadaye yakioza uongeza rutuba katika udongo na pia kusaidia kuzuia
kumea kwa magugu na husaidia tunda kutogusana na udongo kitu ambacho
kinaweza kusababisha tunda kuathiriwa na joto la udongo au magonjwa
kirahisi.Weka matandazo pale mche wako utakapo fikia urefu wa sentimita
10.
Punguza urefu wa mmea
Ili kupata matunda mazuri na yenye afya
ni vema kuupunguza mmea kwa mbele ,pale unapoona mmea umefika urefu wa
kutosha ili kusaidia kutengeneza matawi ya pembeni ambayo mara nyingi
ndio ubeba maua ya kike.
Kuondoa magugu
Ni muhimu sana kuondoa magugu katika
shamba lako hasa wiki za mwanzo ili kuzuia ushindani wa mahitaji kati
ya magugu na mmea ambapo hupelekea kupungua kwa mavuno na muda mwingine
magugu haya yanaweza kuwa ndio chanzo cha baadhi ya magonjwa katika mmea
wako
Uchavushaji
Ili kupata kiasi kikubwa cha matunda ni
vyema kuwa na mzinga wa nyuki karibu na shamba lako ili kusaidia
uchavushaji wa maua ya tikitimaji.Tunashauri uwe na mizinga 1-2 kwa
hekari moja.Waweza pia pands alizeti jirani na shamba lako ili kuvuta
nyuki.Pia zuia kupulizia dawa za wadudu kipindi cha maua maana unaweza
wakimbiza au kuwaua nyuki, kumbuka maua ambayo hayakuchavushwa vizuri
huzaa matunda yenye umbo baya lisilo shabihiana na mengine.
Punguza idadi ya matunda
Kwa kawaida tikitimaji uweka zaidi ya
matunda manne ,ili kupata matunda makubwa na yenye afya ni vyema
kupunguza matunda kwa kuondoa baadhi ya matunda ambayo yanaonekana
hayana afya nzuri na yaliopoteza umbo zuri na kuhakikisha kila mche
unabaki na matunda 2-3 tu.
Uvunaji
Tikitimaji uvunwa baada ya miezi miwili
na nusu hadi mitatu kutoka siku ya kupanda,lakin yapo ambayo hukomaa kwa
siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu.
Mangonjwa
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
Huu ungonjwa husababishwa na fangasi
(Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani
na hupendelea sana wakati wa baridi,
Dalili zake:
Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na
kuwa kama ya njano huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka na
madoadoa meus kwa mbali..
Tiba yake.
Tafuta dawa yenye viambato...Metalaxyl na mancozeb ....kama vile Ridomil gold.
2) Ubwiru juu (Powdery mildew )
Dalili za huu ungonjwa...utaona majani yanakuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu
Tiba yake
Tafuta dawa yenye kiambato...Difenoconazole ..kama vile Score.
3) Kata kiuno.(Damping off)
Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini ,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.
Tiba yake.
Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea yako kuota.
Wadudu
1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis
ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea
mangonjwa ya virusi.
Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.
Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.
,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.
Mbegu bora za tikitimaji.
Kuna mbegu chotara na opv(Sio chotara)
But mbegu bora ni chotara na baadhi ya hizo mbegu ni...
1) Arashani F1-kutoka syngenta
2) Sukari F1-Kutoka East Africa seeds.
3) Sugar king F1-kutoka africasia
4) Juliana F1-kutoka Kiboseed
5) zebra F1-Kutoka Balton.
6) Pato F1-Kutoka Agrichem
Pia zipo mbegu za Sugar king na PATO F1 250gms kwa shilingi 130,000 ambapo utapata mbegu 2,500 na matunda yake yana uzito wa kilo 3-5 na matamu sana , potable kwa kuuza na kwa kusafirisha
SOKO LA TIKITI
Napenda kuwashauri wakulima wetu kuwa
njia nzuri ya kulima tikitimaji ni ile ya umwagiliaji, ukiwa mkulima wa
tikitimaji lazima uwe mjanja kupanda zao lako ili uje uvune wakati soko
liliwa vizuri, mzunguko mzuri wa kupanda tikiti ni huu, panda zao lako
katikati ya msimu wa mvua wakati walimaji wa matikiti kwa kutegemea mvua
(ambao ni wengi) mazao yao yametoa maua ili wakati wao wanavuna tikiti
zao, mazao yako yawe ndio yanaanza kutoa maua kwa hiyo wakati unavuna
wakulima wa kutemea mvua watakuwa washamaliza soko lao.Pia kwa wale
wanaotegemea mvua ni vizuri uchunguze soko lako vizuri ili uwe na
uhakika wa kuuza matunda yako wakati yakiwa tayari yamekomaa.
NUFAIKA NA KILIMO CHA TIKITIMAJI NA FAHAMU SOKO LAKE
Reviewed by BENSON
on
March 06, 2018
Rating:
No comments