NJIA BORA ZA KUKINGA MIMEA YAKO DHIDI YA JUA KALI NA MVUA KUBWA
Jua kali utakabiliana
nalo kwa kujua aina ya udongo ulionao mfano kama udongo wako unahifadhi sana
maji na jua kali lipo ila bado uhifadhi wa maji ni mkubwa hapa utapaswa
kukabiliana na hali hii kwa kumwagilia mara moja kwa siku moja ili kuepukana na
ugonjwa wa kata kiuno. Ila kama udongo unahifadhi maji na jua likawa kali kiasi
ambacho saa sita mchana maji yashakauka na mmea unaanza kusinyaa au kuweka
rangi ya njano kutokana na jua kali hapo inabidi ukabiliane na changamoto hii
kwa kufanya yafuatayo:-
a. Kuweka matandazo ya majani (Organic mulch)
b.
Kuweka matandazo ya plastiki (Plastic mulch) wasiliana na sisi tukupatie
c.
Au kuweka kichanja kama ni bustani ndogo ya mboga mboga
d.
Kufunga mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone pamoja na njia ya matandazo pia. Hapa kama mkulima waweza
kabiliana na jua na ukafanya kilimo chenye tija. Bila kufanya haya mmea wako
utatoa mazao madogo, au kusinyaa au kubadilika rangi na kuwa wa njano na
kudumaa pia. Kumbuka mmea kabla ya kubakia na maji yatayotumika na mmea kuna
kiwango maalumu cha maji yanayopotea hewani kwa njia ya stomata. Na hapa mmea
unapaswa kubaki na kiwango cha maji ambayo yatatumika na kazi muhimu mbali
mbali kwa mmea wako. Njia nlizoeleza pale juu zitausaidia mmea wako kuhifadhi
unyevu kwa matumizi ya mmea.
KUMBUKA: Kila mmea una mahitaji maalumu ya mwanga na
maji.
NET MAALUMU KWA AJILI YA MABANDA KITALU |
Lakini pia upande wa pili
kujikinga na jua kali japo njia hii itakusaidia kujikinga na mvua yenye madhara
hapa unaweza
kujenga Banda kitalu (Green House), au Net house jengo ambalo tumelieleza vyema sana katika
nakala zilizopita faida na hasara zake. Hili jengo husaidia kwa kiasi kikubwa
katika kupunguza mionzi ya jua na mtone ya mvua. Lakini pia kuna majengo
mengine ambayo yataweza kutumika kupunguza miale mikali ya jua kama kichanja
house, net house faida ya majengo haya hupunguza miale ya jua na mvua japo net
house huingiza maji. Kwa ujumla maeneo ya pwani jua huwa kali sana hivyo basi
mkulima napaswa kuzingatia haya ili aweze kufanya kilimo chenye tija.
KUHUSIANA
NA MVUA
Kama mkulima mvua ina faida kubwa sana hasa
ikanyesha kipindi ambacho ndo unaotesha au kipindi amacho ndo unahamisha mazao
yako shambani kutoka kitaluni. Kikubwa jitahidi kujua aina ya zao lako na
uhitaji wake wa maji. Kumbuka uhitaji wa maji kwa kila mmea hutofautiana.
Ukiachilia mbali kuwa uhitaji tofauti tofauti wa maji kwa kila mmea. Maji
yakiwa mengi huleta madhara yafuatayo:-
Magonjwa ya fangasi, mfano mmea kukata kiuno
(Damping Off), ugonjwa wa ukungu ambao ni hatari sana, na magonjwa mengine ya
kuozesha tunda (Fruit end root) japo ugonjwa huu wa kuoza tunda wakulima wengi
hujua sababu moja tu ya kukosekana madini ya kalshamu lakini pia ikitokea huna
ratiba maalumu ya umwagiliaji pia ugonjwa huu utakupata haswa mvua ikianza
kunyesha huwa inanyesha kipindi tofauti tofauti sana na hivyo huleta madhara
moja kwa moja.
SWALA
LA KUFANYA
Ni muhimu sana unapoona muda mwingi kuna mawingu na
mionzi ya jua ni hafifu, basi ni muhimu sana kutafuta dawa zenye kiambata cha
KOPA (Copper) mfano Blue Copper, au Red Copper, au dawa kama Ivory, Ebony 72
WP, hizi dawa zoote zenye copper husaidia mmea kuwa wa moto, hivyo kupunguza
fungus kujijenga.Fungus hupenda hali ya unyevu unyevu.. kwa mfano katika zao la
kahawa inashauriwa sana katika kuzuia ugonjwa unaoitwa Coffee Berry
Diseases-CDB, ugonjwa wa kunyauka matunda, ni vizuri mkulima akapiga dawa za
kuzuia ukungu mwezi mmoja kabla ya mvua kuanza, ili kuupa mmea moto, lakini
wakulima wengi hawafanyi hivyo. Huwa wanasubiri hadi wavamiwe ndio wapige,
lakini ugonjwa kama huo CBD ukivamia mkahawa hakuna jinsi utafanikiwa
kuupunguza ndo hapo ambapo unakuta sasa mkulima anapata hasara kubwa kwa kuwa
mashambulizi yanakuwa ni makubwa sana ya mdudu huyo. Hii pia ipo kwa mazao
mengine kwa hivyo mkulima ajue jinsi ya kuukinga mmea wake na ukungu.
NJIA BORA ZA KUKINGA MIMEA YAKO DHIDI YA JUA KALI NA MVUA KUBWA
Reviewed by BENSON
on
March 07, 2018
Rating:
No comments