ZIFAHAMU MBOLE NA MATUMIZI YAKE KWA AJILI YA KUOTESHEA MAZAO.

Image result for mbolea za samadi
Wapendwa wasomaji wa makala za kilimo katika blog yetu ya Kilimo bora leo tumekuandalia makala nzuri juu ya Mbolea . Mbolea kwa maana ya kueleweka kwa haraka ni kitu chochote kinacho ongeza virutubisho muhimu kwenye udondo ambavyo hutumiwa na mimea ili kuboresha ukuaji wa mimea na upatikanaji wa mavuno mazuri.
Kuna aina mbalimbali za mbolea kama mbolea za asili Mbolea za asili mfano, Samadi, Mboji, mbolea za kijani na  Mbolea za viwandani mfano DAP, YaraMila

1. Mbolea za asili
Mbolea aina ya Mboji (Mabaki ya Mazao). Mbolea hizi hutokana na vinyesi vya wanyama, mabaki ya mazao shambani,majivu na takataka nyingine ambazo ni rafiki kwa mazao na udongo (takataka zisizo na madhara kwenye udongo).


Mbolea za asili zinafaa sana kutumika wakati wa kuandaa shamba/ mkulima anaweza kuchamganya mbolea ya asili na udongo wakati wa kulima au mkulima kuitumia mbolea ya asili kupandia mazao yake mfano mahindi, mharagwe, mboga mboga na mazao mengine.


Mbolea za asili hufanya kazi ya kuboresha hali ya udongo kuufanya udongo uwe na uwezo wa kuifadhi maji na hewa, vilevile mbolea za asili ufanya udogo kuweza kutengeneza matundu mazuri ambayo husaidia mizizi ya mazao na hewa kupenya kwa urahisi.


2. Mbolea za viwandani/ mbolea za kisasa
Mbolea hizi zimetengenezwa kiwandani kwa kuchanganya virutubisho mbalimbali vinavyo hitajika katika ukuaji wa mimea. Mbolea za viwandani zipo za aina mbalimbali na pia hutumika kwa wakati tofauti katika hatua za ukuaji wa mimea, zipo mbolea maalumu kwa ajili ya kupandia mazao mfano DAP na Urea, zipo za kukuzia mazao mfano CAN na NPK


Mbolea hizi zinapaswa kutumiwa kwa uangalifu kulingana na mahitaji ya mimea kwani mbolea ikizidi katika udongo husababisha mimea kukua sana na kusahau kutengeneza matunda ambayo ndio tegemeo kwa mkulima hivyo mkulima anavyo paswa kuweka mbolea kulingana na vipimo vinavyotakiwa kitaalamu (ni vyema mkulima kupata ushauri wakilaamu kutoka kwa mtaalamu wa kilimo aliepo karibu nae ili kujua kiasi cha mbolea anacho paswa kuweka kwenye mimea yake shambani)


3. Mbolea za kupandia
Mimea ya jamii ya nafaka hufanya vizuri zaidi kama itapandwa kwa kutumia mbolea ya NPK au DAP kwa kuweka gramu tano za mbolea husika katika shimo, vilevile mimia ya jamii ya mikunde na mboga mboga hufanya vizuri ikiwa itapandwa kwa kutumia mbolea ya NPK kama inapatikana.


4. Mbolea za kukuzia
Mahindi yaliyofikia ukubwa wa kukuzia. Kuna aina nyingi ya mbolea za kukuzia mazoa, mkulima anashauriwa kuwa anatunza kumbukumbu ya taarifa zake za shamba hii itamsaidia kujua huduma sahihi ya kuipatia mimea yake.


Kwa mfano kama mkulima alipanda mazao yake kwa kutumia aina Fulani ya mbolea mfano TSP au DAP mkulima anatakiwa kuwa na kumbukumbu hii itamsaidia mshauri wa kilimo kuweza kufanya kazi kwa urahisi zaidi, pia itaepusha kutoa ushauri unaohusu kutumia pembejeo mkulima alizo tumia mwanzo.


Kama mkulima alipanda kwa kutumia mbolea inayotoa kirububisho kimoja tuu kwenye mimea mfano UREA au TSP wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia mkulima anashauriwa kuweke mbolea itakayo ipatia mimea virutubisho zaidi ya kimoja mfano NPK au CAN kwakua virutubisho vinavyo itajika kwenye mimea hufanya kazi tofauti hivyo mkulima anatakiwa kulizingatia sana hili.


Muonekano wa mbolea ya UREA
Pia kama mkulima kama alipanda kwa kutumia mbolea ya samadi wakati wa kupandia anapaswa kutumia mbolea inayotoa kirutubisho kimoja mfanyo UREA hii ni kwa sababu samadi ya wanyama ina virutubisho vingi ambavyo vinahitajika katika ukuaji wa mimea shambani. Lakini mkulima anaweza kutumia mbolea zinazo ongeza virutubisho zaidi ya kimoja mfano CAN na NPK kwa mavuno bora .


Mazao ya jamii ya nafaka hufanya vyema kama yatakuziwa kwa kutumia mbolea ya NPK, vilevile mimeaya mbogambopa na matunda hufanya vizuri kama itakuzwa kwa kutumia NPK au CAN. Kwa mimea ambayo hutoa matunda CAN inafaa zaidi kwa kua CAN hifanya matunda kua makubwa na mazuri


Mbolea za Viwandani
Mbolea za viwandani zimegawanyika katika makundi makuu matatu, nayo ni mbolea za chumvichumvi, chokaa na kijivu,


5. Mgawaniko/makundi ya mbolea za viwandani
(a) Mbolea za Chumvichumvi
Mbolea hizi hujulikana kama mbolea za kukuzia na huwekwa shambani baada ya mimea kuota.
Zina virutubisho vingi vya Naitrojeni ambavyo huifanya mimea kukua haraka.
Zinahusika na utengenezaji wa kijani kibichi kwenye mmea.
Mbolea za chumvichumvi zinazotumika zaidi Nchini Tanzania ni:-
– Sulphate of Ammonia (S/A)
– Calcium Ammonium Nitrate (CAN)
– Urea.
– Mbolea ya mchanganyiko N.P.K.


(b) Mbolea za Chokaa:
Hizi ni mbolea zinazotumika kupandia mbegu au miche.
Husaidia uotaji mzuri wa mimea, huimarisha mizizi, na hutumika katika utengenezaji wa chakula na mbegu kwenye tunda.


Huhusika na usafirishaji wa nguvu kwenye mmea na hufanya mazao kukomaa haraka.
Mbolea hizi huwekwa shambani wakati wa kupanda.
Aina ya mbolea za chokaa zinazotumika hapa nchini ni Triple Super Phosphate (TSP). Vilevile unaweza kutumia N.P.K kwa kupandia.


(c) Mbolea za Kijivu (Potashi):
Potashi ni kirutubisho kinachosaidia mimea katika utengenezaji wa protini na wanga.
Pia huhusika na utumiaji wa madini muhimu kwa maisha ya mimea.
Pia huwezesha matunda kukomaaa, kuiva haraka, na kutengeneza mbegu bora.



Husaidia ongezeko la maji kwenye mmea na kuufanya ustahimili magonjwa, ukame, baridi na hali ya udongo wenye alkalini nyingi.
Mbolea za Potashi zinazotumika ni:-
– Muriate of Potash (MoP)
– Sulphate of Potash (SP)
ZIFAHAMU MBOLE NA MATUMIZI YAKE KWA AJILI YA KUOTESHEA MAZAO. ZIFAHAMU MBOLE NA MATUMIZI YAKE KWA AJILI YA KUOTESHEA MAZAO. Reviewed by BENSON on December 11, 2017 Rating: 5

14 comments