KILIMO CHA PILIPILI

Related image
Pilipili ni kiungo kikali, hutumiwa kwa kukoleza mchuzi na vyakula mbali mbali. Pilipili zinaweza kupikwa zikiwa nzima au kukatwakatwa na kutumiwa katika kachumbari; au kuwekwa kwenye siki na achali, au kusagwa na kutumia unga wake.

Hili ni zao la nchi za kitropiki, na hutumiwa sana na wakazi wa Bara Hindi, Mashariki ya Mbali. Amerika ya Kusini na Afrika ya Tropiki. Pilipili huwekwa katika makundi makubwa mawili, yaani: 

1. Pilipili Hoho (Hot Pepper)- Hizi ni ndogo ndogo, ndefu, nyembamba, na kali sana. Aina zinazojulikana zaidi ni Green Chilli, Cherry Pepper, Long Cayenne na Tabasco.

2. Pilipili Manga (Sweet Pepper)- Hizi zina umbo kubwa, nyama nying, mviringo na ndefu kidogo, siyo kali. Aina zinazojulikana zaidi ni Sweet, Neapolitan, Keystone, Giant, Ynlo Wonder na california wonder.

Kupanda: Mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa majuma manane hadi kumi. Kisha miche hupandikizwa bustani kwa umbali wa sentimeta 45 kwa 90.

Kuvuna: Umri wa kuvuna zao hili hutegemea aina ya pilipili na matumizi yake. Aina ambayo ni kubwa na tamu kwa kawaida huvunwa kabla haijapevuka na kugeuka rangi yake. Pilipili katika hali hii hutumiwa zaidi kwenye michuzi, kachumbali na kutiwa kwenye makopo. 

Pilipili kali, ambayo mara nyingi ni ndogo ndogo, kwa kawaida huvunwa baada ya kupevuka na kuwa nyekundu. Halafu hutumiwa katika mapishi na vyakula mbali mbali, lakini sehemu kubwa zaidi hukaushwa na kusagwa ili kupata unga wake.

Magonjwa: Damping- off, Bacteria Spot, Fusarium wilt na Antracnose, ni miongoni mwa magonjwa yashambuliayo zao hili. Tuseme magonjwa ya pilipili ni sawa na ya Nyanya. Hivyo njia za kupigana nayo ni sawa.

Wadudu: Wadudu ambao hushambulia zao hi wengi, lakini walio wabaya zaidi ni Aphids, Cut worm, Flea beetle, Pepper weevil na Pepper Maggot.

Kinga: Parathion 1% au Chlrdane 5%. Dawa itumiwe mara wadudu watokeapo na kurudiwa kila baada ya siku 7.
Ahsanteni!


KILIMO CHA PILIPILI KILIMO CHA PILIPILI   Reviewed by BENSON on December 28, 2017 Rating: 5

No comments