UFUGAJI BORA WA KULOIREL
Kuloirel ni kuku chotara ambaye asili
yake ni nchini india, na imetokana na mchanganyiko wa dume la broiler na
jike aina ya Rhode island red au dume la white legham na jike la Rhode island
red. Kuku hawa ni moja kati ya kuku wasio na gharama kubwa katika kuwafuga
lakini pia wana faida kubwa pindi ukiamua kuwafuga. Lakini pia
kuku hawa ni moja kati ya mbegu ambayo inafanya vizuri sana katika nchi nyingi.
SIFA ZA KULOIREL
1. Ni aina ya kuku ambao hutumika kwa matumizi ya ani nyama
pamoja na mayai
2. Kuku mmoja anauwezo wa kutaga mayai 150 hamsini kwa
mwaka ukilinganisha na kuku wengine hutoa 40- 50 kwa mwaka.
3. Madume ya kuloirel hua yana kilo 3.5 na jike ni
kilo 2.5 ukilinganisha na kuku wengine dume hua na kilo 2.5 na jike ni
kilo 1.5.
4. Pia ni moja kati ya aina ambayo haipati magonjwa kirahisi
(disease resistance)
5. Kuku hawa hawana gharama sana katika kuwalisha kwa sababu
wanauwezo pia wa kula chakula kama kuku wa kienyeji.
Banda
Kama walivyo kuku wengine banda lazima
liwe bora ili kuweza kupata kuku bora pamoja na mayai mengi, ila pia kuku wa
aina ya kuroiler sio lazima uwafungie ndani moja kwa moja unaweza kutengeneza
sehemu ambayo utawafungulia ili kuweza kujipatia chakulatofauti na kuku wa
kisasa.
Lakini pia ni vyema kila wakati ukazingatia usafi ni muhimu hivyo ni vyema
kuzingatia hilo
chakula
Chakula ni lazima kiwe bora ili kupata kuku bora pamoja na mayai ya kutosha.
1. Kuku jike mmoja anakadiliwa kula kilo 5-8 kabla ya kuanza
kutaga.
2. muhimu sana kwa mfugaji kujifunza jinsi ya kuchanganya
chakula mwenyewe.
3. kuanzia siku 1 hadi wiki 4 unatakiwa kuwapa chakula cha
kuanzia (chick starter mash)
4. kuanzia wiki ya 4 hadi 8 unawapa chakula cha kukuzia (chick
grower mash)
5. Kuanzia wiki ya kwanza kuanza kutaga hadi mwisho unatakiwa
kuwapa chakula(layersmash)
6.
7. Lakini pia inakadiliwa kua na drinker 15 na vyombo vya kulia
chakula, wastani wa kuku 1000.
UFUGAJI BORA WA KULOIREL
Reviewed by BENSON
on
December 29, 2017
Rating:
No comments