KILIMO BORA CHA MABOGA

Related image
Maboga Hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi. MABOGA ni mojawapo ya jamii aina ya mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,matikimaji na maskwash. Zao la MABOGA ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine. Boga lipo katika jamii ya Cucurbita pepo.


Faida ni kubwa kwa mkulima, kwa kuwa zao hili huuzwa kwa kilo na ukubwa hutegemeana na matunzo shambani. Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa. Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha maboga. Asili ya boga ni Amerika kaskazini, maboga yamekuwa yakipandwa kwaajili ya biashara na kwaajili ya chakula. Kwa sasa maboga yamekuwa yakilimwa maeneo mbalimbali duniani, Antarctika pekee ndiko maboga hayawezi kustawi. Mataifa yanayozalisha maboga kwa wingi ni Marekani (USA), Canada, Mexico, India, and China.
Maboga yanahitaji joto la wastani kutoka kwenye jua, pia eneo ambalo halituamishi maji udongo wake uwe na pH kati ya 6.0 – 6.8. Pia udongo uwe na joto inchi tatu (sm 7.6) kushuka chini angalau nyuzi 60 °F (15.5 °C), maboga yatadhoofika kama maji yatakosekana.


UTAYALISHAJI WA SHAMBA NA UPANDAJI
Baada ya kuchagua aina ya mbegu unayohitaji kupanda, inashauriwa kulima shamba na kuacha kwa muda wa kipindi kitakachoruhusu nyasi na magugu mengine kuoza kabla ya kupanda.Hii inasaidia majani na magugu kutoota upesi pindi ukipanda miche yako ya MABOGA.Hakikisha kuwa shamba lako limelimwa vizuri na udongo kulainika, udongo uwe umechimbuliwa kiasi cha inchi 8-10 kwenda chini. Hakikisha kuwa shamba lako lina nafasi ya kutosha kwa kuwa MABOGA huhitaji nafasi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kupata mwanga wa jua wa kutosha. Katika shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande katika kitalu kwasababu miche ya MABOGA huwa ni dhaifu sana wakati wa upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 60 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za MABOGA uliloninua kwasababu linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na ubora wa MABOGA yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili (F2)
Kila shimo hakikisha umeweka mbegu tatu na uzipande kwa utaratibu wa pembe tatu au kwa lugha rahisi mafiga.
Zikishaanza kutoa matunda hakikisha kila shina unaacha matunda matatu mengine kata ili kuruhusu ukuaji mzuri wa tunda kwani yakiwa mengi yatakuwa yanagawana chakula hivyo tunda kuwa dogo ambalo ukipeleka sokoni unapata pesa kidogo.



AINA ZA MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga 
Ni vizuri zaidi kununua mbegu za maboga zilizotayarishwa na zinazouzwa katika maduka ya pembejeo kuliko kutumia mbegu zile zinazopatikana baada ya kuvuna boga na kisha kuondoa mbegu zilizo ndani na kukausha kisha kuotesha.


Aina za mbegu
Kuna aina mbalimbali za mbegu ambazo huweza kutumiwa na wakulima katika kufanya kilimo cha maboga. 
a) Jack Be Little
Aina hii hutoa maboga ya mviringo nyororo na ambayo hukomaa kuanzia siku 90 hadi 100 toka kuoteshwa.
b) Autumn Gold
Aina hii hukomaa ndani ya siku 100 hadi 120 na huweza pia kutoa boga lenye uzito wa kilogramu 4 hadi 8 kulingana na matunzo. 
c) Sugar Treat 
Aina hii hukomaa ndani ya siku 100 hadi 120 na huweza pia kuwa na kilogramu kuanzi 4 hadi 8 kwa boga. Ubora wa maboga hutokana na utunzaji na usimamizi sahihi. 
d) Maxima 
Aina hii huweza kutoa boga lenye uzito wa hadi kilogramu 10 na hukomaa ndani ya siku 90 hadi 120.



HALI YA HEWA
Kabla ya kupanda hakikisha kuwa udongo una joto la wastani wa nyuzi joto 70°C. Unaweza kupanda kwa kutumia jembe la mkono au reki. Fukia mbegu kwenye mashimo kwa kutumia udongo laini na shimo lisiwe na kina kirefu, liwe na wastani wa inchi 1, ili kutoa urahisi kwa mbegu kuota. Kwa kawaida tikiti hupandwa kwa mstari mmoja kwenye tuta lenye mwinuko wa inchi 6 na upana wa futi 4. Nafasi kati ya mche na mche iwe ni sentimita 120.



Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Maboga hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo maboga itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota 
Mvua: kwa upande wa mvua maboga yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.



Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0



AINA ZA UDONGO
Kuna aina kuu tatu za udongo,
• Kichanga (Sand soil) – 
una uwezo mdogo wa kuhifadhi maji na unyevunyevu. Hivyo, hukauka upesi.
• Tifutifu (Loam soil) –
unahifadhi maji vizuri na upatikanaji wa maji na virutubisho kwa mimea ni mkubwa. 
• Mfinyanzi (Clay soil) –
unahifadhi maji mengi zaidi, bali upatikanaji wa virutubisho kwa mimea ni mdogo.


Vipimo vinavyoonyesha hali ya rotuba ya udongo ni: 
• Tindikali ya udongo 
• Kiasi cha mboji 
• Kiasi cha Naitrojeni, Fosfati, Potashi, Salfa, Chokaa (Calcium) na Magnesium. Vilevile kiasi cha zinki, shaba, manganese na boroni vinapimwa.


Kipimo cha PH ya udongo (Soil pH) 
PH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa na tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7.Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0).



Maboga hustawi katika udongo wowote ambao hautuamishi maji.Hivyo zao hili linaweza kulimwa katika maeneo yoyote na pia linaweza kulimwa katika udongo wenye asili ya mfinyanzi katika maeneo yanayopata mvua kwa kiasi kidogo.


MBOLEA
Katika matumizi ya mbolea yanatofautiana kutokana na mbegu, Lakini tumia mbolea za asili (samadi au mboji) ili kuongeza rutuba kwenye udongo, ukihitaji kutumia mbolea za viwandani weka kiasi, sana, labda eneo hilo kama hakuna rutuba, mbolea ya NPK,UREA,CAN,DAP unaweza tumia.


MATANDAZO (MULCHES ),UPALILIAJI & UMWAGILAJI
Kwasababu ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika ardhi. Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo. Palilia shamba nyasi zinapoanza kuota, pia safisha shamba ili kuondoa wadudu. Shamba la maboga linatakiwa liwe na unyevunyevu kila mara ili maboga yaweze kustawi vizuri yasidumae.mwagia maji mara pindi unyevu unapotea shambani sio kila siku kwani mabonga yahaitaji maji mengi sana


WADUDU NA MAGONJWA YA MABOGA
Mangonjwa
1) Ubwiru chini (Downy mildew)
Huu ungonjwa husababishwa na fangasi (Pseudoperonosporacubensis).Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na hupendelea sana wakati wa baridi,
Dalili zake:
Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka na madoadoa meus kwa mbali..


Tiba yake.
Tafuta dawa yenye viambato...Metalaxyl na mancozeb ....kama vile Ridomil gold.


2) Ubwiru juu (Powdery mildew )
Dalili za huu ungonjwa...utaona majani yanakuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu


Tiba yake
Tafuta dawa yenye kiambato...Difenoconazole ..kama vile Score.


3) Kata kiuno.(Damping off)
Huu ugonjwa husumbua sana miche midogo,huanzia aridhini ,husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.


Tiba yake.
Tafuta Ridomil gold na anza kupulizia mara tu baada ya mimea yako kuota.


Wadudu
1) Wadudu mafuta (Aphid)
Hawa hushambulia majani na kufyonza juis ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kupelekea mangonjwa ya virusi.


Dawa yao.
Tafuta Actara na pulizia majani pamoja na udongo.

Wadudu wengine ni;Nzi weupe (whitefly )-Actara itawamaliza.
,Utitiri mwekundu (Redspidermites)-Dynamec itawamaliza,Thrips-Actara na Dynamec itawamaliza kabisa.


Anthracnose
Huu ugonjwa hushambulia mizizi na shina na kuweka ugumu ugumu kisha rangi nyeusi kama ukilipasua katikati. Namna ya kuzuia Wadudu hawa na magonjwa huweza kuzuiliwa kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo, na kwa kutumia madawa ya asili kama vile majivu ambayo unaweza kuyamwaga kwa kuzunguka kila shina la boga au sabuni,kitunguu swaumu na mwarobaini kulingana na ushauri wa mtaalamu wa kilimo.



UVUNAJI
Maboga hukomaa baada ya siku 95 mpaka 120, ili kujua kuwa boga lako limekomaa unaangalia kikonyo, kikonyo cha boga kinapoteza maji na kinaanza kuwa kikavu.



MATUMIZI 
•Boga hutumika kama chakula kwa kuchemsha, kukaanga, kuoka, kupika kwa mvuke au kwa kuchoma. 
•Majani yake hutumika kama mboga 
•Mbegu zake hutumika kama vitafunwa kwa kukaangwa.


•Mbegu zake zikiliwa zikiwa mbichi hutumika kutibu sukari ya kushuka type-1. •Huongezaprotinimwilini. 
•Mbegu zake zina wingi wa madini aina ya magnesium. 
•Ikiuzwa hutumika kujipatia kipato.



MWISHO WA MAKALA
TEMBELEA MAKALA ZANGU KWENYE MTANDAO
• ,karanga,nk
• Kilimo cha vitunguu,pilipli,nyanya na mazao yote ya mbogamboga
• Kilimo cha matunda kama mipesheni mipapai,michungwa,nk
• Ufugaji wa kuku wa kienyeji kisasa



KILIMO BORA CHA MABOGA KILIMO BORA CHA MABOGA Reviewed by BENSON on December 27, 2017 Rating: 5

5 comments

  1. Makala nzuri asante kwa Elimu,naomba msaada kwa ni kama mentor juu ya ukulima na ufugaji kiujumla.naweza pata namb yako au social media pages zako?

    ReplyDelete
  2. Masoko yake yapo wapi Sana Sana

    ReplyDelete
  3. Mimi nimelima Kama ekari tatu Ila bdo Sina uhakika wa masoko yake

    ReplyDelete