KILIMO BORA CHA VIAZI VITAMU
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi
nchini Tanzania ambayo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga
ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame.
Zao la viazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya
Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya
Mara, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro, Kagera, Arusha na Ruvuma.
Matumizi
Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa
katika njia mbalimbali kama
vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu
hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya
viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika
kutayarisha mboji.
Aina za viazi vitamu
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni.
Hapa nchini Tanzania aina
zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega,
Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli,
Sinia,Vumilia na Polista
Uzalishaji
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi
hustawi vizuri katika maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa
urahisi. Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi
kupenya na kupanuka. Shamba jipya
litayarishwe vizuri kwa kufyeka vichaka na kung’oa visiki. Majani yafukiwe
wakati wa kutengeneza matuta ili kuongeza rutuba ya udongo.
Viazi vipandwe kwa kutumia Marando yenye urefu
wa sentimita 30 kwa mavuno bora.
Inashauriwa kutumia sehemu ya juu ya shina kwa
mavuno zaidi. Marando yapandwe katika umbali wa sentimita 25 hadi 30 kutoka
mmea hadi mmea na sentimita 60 hadi 75 kutoka tuta hadi tuta.
Viazi pia vyaweza kupandwa kwa kutumia viazi
vyenye afya vyenye uzito wa kati ya gramu
20 hadi 30. Hata hivyo inashauriwa kutumia marando
ili kupata mavuno zaidi na kuepuka
kuenea kwa magonjwa.
Kutunza
shamba
Ni muhimu kupalilia viazi vitamu katika miezi miwili
ya mwanzo ili kuupa mmea nguvu ya
kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza
kufunika ardhi na hivyo huzuia uotaji wa
magugu. Viazi hushambuliwa na wadudu mbalimbali
wakiwemo kipepeo, mbawa kavu, fukusi na minyoo fundo.Pia hushambuliwa na
magonjwa yakiwemo magonjwa yanayotokana na virusi
kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV).
Magonjwa na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba, kubadilisha
mazao, na kuzingatia udhibiti sango.
MATUMIZI
YA MBOLEA ZA VIWANDANI NA
SAMADI
Samadi hutoa virutubisho kama vile N, P, K, Ca,
Mg , S. Samadi ikitumiwa vizuri huchangia katika kuimarisha mazao, huboresha
ubora wa udongo na hulinda unyevu unyevu. Weka samadi angalau siku 90 au 120
kabla ya kuvuna mazao yoyote ambayo yanaweza kuliwa bila kupikwa.
Virutubisho katika samadi katika tani 1:
Samadi za ng’ombe (32% DM): kg N 5.9, kg P 2.6
na kg K 5.4
Samadi za nguruwe (40% DM): kg N 8.2, kg P 5.5
na kg K 5.5
Samadi za kuku (57% DM): kg N 16.6, kg P 7.8 na
K 8.8
Virutubisho/madini katika mfuko mmoja (kilo 50)
cha 15-15-15 mbolea ambayo ina N kilo 7.5, P
kilo 3.3, na K kilo 6.2, kwa mtiririko.
Njia
bora za matumizi ya samadi:
- Epuka
kuweka samadi baada ya kupanda mazao
- Changanya
samadi na udongo kabla ya kupanda
- Usitumie
samadi ya mbwa au paka kwa sababu aina hizi kushiriki vimelea wengi na
binadamu
Osha vizuri mazao yanayotoka katika shamba ambalo
umetumia samadi kabla ya matumizi
Uvunaji
Viazi vitamu huwa tayari kuvunwa miezi mitatu hadi
minne tangu kupanda kutegemea hali ya hewa. Viazi vinaweza kuvunwa kidogo kidogo kwa
kutumia mikono, vijiti, jembe, au rato kadrivinavyohitajika.
Aidha inashauriwa viazi
visiachwe ardhini muda mrefu bila kuvunwa kwani vitakomaa sana na kuwa na
nyuzi, na hivyo kuharibu ubora wake. Pia kuacha viazi muda mrefu hukaribisha mashambulizi
ya wadudu kama fukusi na kuoza. Kwa maeneo makubwa zaidi, inashauriwa kutumia
mashine ya kukokotwa na ng’ombe.
Uvunaji ufanywe kwa uangalifu ili kuhakikisha viazi
visikatwekatwe wala kuchubuliwa wakati wa kuvuna. Mavuno ya viazi hutofautiana kulingana na aina,hali
ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi yanakadiriwa kufikia tani 12 kwa ekari.
UCHAKATAJI
viazi vinachakatwa ili:
- Vikae
muda mrefu bila kuharibika
- Kupunguza
uwingi na kurahisisha usafirishaji
- Kuondoa
sumu katika viazi
- Kutengeneza
aina mbali mbali za vyakula zenye radha nzuri, hurufu na mwonekano nzuri
Kuzalisha malighafi ya viwanda
Kazi
za uchakataji wa viazi
Kumenya:
Karibu mazao yote ya viazi hutengenezwa kwa kumenywa kwanza. Kumenya
kunaongeza ubora na usalama wa chakula.
Ukamuaji:
Njia za kienyeji za kukamua kwa mawemazito na magogo ni hatari, kazi ngumu na huchukua muda mrefu. Zipo mashine za kukamua
kwa sasa
Ukaushaji:
viazi hukaushwa kati ya 12 – 14% ya unyevu nyevu kabla kuhifadhi. Njia
iliyozoeleka ya kienyeji ni kwa jua pia mashine.
Usagaji:
viazi vyaweza kutengenezwa unga kabla ya matumizi ya nyumbani au viwandani
KILIMO BORA CHA VIAZI VITAMU
Reviewed by BENSON
on
November 12, 2017
Rating:
No comments