UJUE UGONJWA WA NDUI YA KUKU (FOWL POX)

Related image
Ugonjwa wa ndui ya kuku mara nyingi huwashambulia kuku wadogo na wakubwa. pia tafiti mbalimbali za masuala ya ufugaji zimebaini ya kwamba ugonjwa huu  husababishwa na virusi.

Jinsi unavyoambukizwa:
i) Ugonjwa huu huambukizwa kwa kupitia kwenye vijeraha vya kuku.
ii) Mbu na wadudu wengine waumao huweza kuambukiza anapomuuma kuku mgonjwa na alfu akamuuma kuku asiye na ugonjwa.

Dalili zake:
1) Homa kali .
2) Kupoteza hamu ya kula.
3) Kupoteza uzito.
4) Kutokea kwa vipele sehemu mbalimbali zisizo na manyoya.
5) Baada ya siku kati ya 7 hadi 14 vipele hupasuka na kuacha vidonda.
6) Vifo huweza kutokea kwa kuku wenye umri mdogo.
7) Kutoa kamasi kwenye pua.
8) Mara nyingi vipele husababisha kuziba macho.

Matibabu:
Ugonjwa huu hauna tiba,kwani huambukizwa na virus.Ila inashauriwa kuwapa kuku dawa ya Antibiotic ili kuzuia kutibu magonjwa nyemelezi yanayoweza kuwashambulia kuku kupitia kwenye vidonda.

Kinga:
1) Ndui ya kuku huzuiwa kwa chanjo ya sindano.
2) Vifaranga wapatiwe chanjo wakiwa na umri wa siku moja na kurudiwa baada ya miezi 2 hadi 3.
3) Tenga kuku wagonjwa na wazima.
4) Epuka madimbwi karibu na nyumba ili kuepusha mazalia ya mbu.


Muhimu:Ili kupunguza kasi endapo ugonjwa huu umewapata kuku,sugua majeraha au vipele kwa pamba iliyochovywa kwenye dawa ya madini joto (Iodine) na baadaye paka mafuta mazito (Petroleum jelly)au samli.Hii sio kutibu ugonjwa bali unawasaidia kuku kulainisha ngozi na macho yapate kuona chakula na maji.
UJUE UGONJWA WA NDUI YA KUKU (FOWL POX) UJUE UGONJWA WA NDUI YA KUKU (FOWL POX) Reviewed by BENSON on November 13, 2017 Rating: 5

No comments