KILIMO BORA CHA VIAZI VITAMU
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini
Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame.
Zao la viaViazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini
Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma,
Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma.
Viazi vitamu hutumika kama
chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa.
Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati
na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha
mboji.
Aina za viazi vitamu
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania
aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali
mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista.
Faida:
vina wanga, vitamin, kambalishe,
madini ya kalisiuamu, potasiamu, chuma, protini, na kalori.
Uzalishaji
Zao hili hustawi maeneo mengi Nchini Tanzania. Viazi hustawi vizuri katika
maeneo ya tambarare yenye udongo tifutifu, unaoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
Udongo wa mfinyazi na wenye kokoto nyingi haufai kwani huzuia mizizi kupenya na
kupanuka.
Namna ya kuandaa ardhi:
Shamba jipya litayarishwe vizuri
kwa kufyeka vichaka na kung’oa visiki. Majani yafukiwe wakati wa kutengeneza
matuta ili kuongeza rutuba ya udongo.
Ukuaji wa viazi huathirika kama
kiwango cha oksijeni kwenye udongo si cha kutosheleza, mifereji na ulimaji wa
matuta makubwa ni muhimu, safisha ardhi mapema kwa kuondoa magugu, lima mara
kwa mara ili kulainisha udongo.
Upandaji:
kupanda
ni kwa kutumia mbegu halisi za viazi, usipande sehemu zenye maji mengi maaana
mbegu zinaweza kuoza,hifadhi kwenye sehemu yenye baridi kidogo na giza mpaka
mbegu zitakapoota, kadri upandavyo viazi vikubwa, ndivyo mavuno yatakuwa mengi,
Tengeneza matuta ya kupandia yaliyoinuka. Kitalu kilichopandiswa juu hutoa
mavuno Zaidi, panda mbegu nzima au kata katika vipande viwili kabla ya
kupandda,ziache mbegu kwa wiki moja ili zitoe vifundo, panda vipande vya mbegu
umbali wa inchi 10-12 kati ya mbegu moja na nyingine na fukia katika shimo la
urefu wa inchi 1 hadi 3, mfumo wa upandaji kwa mstari mmoja au miwili
unaweza tumika, iwapo mfumo wa mstari
mmoja
utatumika acha nafasi ya inchi 24 mpaka 36 kati ya mstari hadi mstari na ikiwa
mfumo wa mistari miwili utatumika acha nafasi ya inchi 70 kabla ya mstari
mwingine.
Kutunza
shamba
Ni muhimu kupalilia viazi vitamu katika miezi miwili ya mwanzo ili kuupa mmea
nguvu ya kutambaa vizuri. Baada ya muda huo, viazi huweza kufunika ardhi na
hivyo huzuia uotaji wa magugu.
Palizi:
palilia
mara tu magugu yatakapoonekana na wakati huohuo ondoa baadhi ya miche
iliyoota karibu karibu ili kutengeneza nafasi, funika nyufa ardhini kwa udongo
ili kuzuia wdudu. Baada ya mimea ya viazi kuota, unaweza kutandaza majani
ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu kushamiri na kupoza udongo.
Wadudu na
magonjwa.
Viazi
hushambuliwa na wadudu mbalimbali wakiwemo kipepeo, mbawa kavu, fukusi na
minyoo fundo.Pia hushambuliwa na magonjwa yakiwemo magonjwa yanayotokana na
virusi kama Sweet Potato Chlorotic Stunt virus (SPCSV),ukurutu
ugonjwa usabababishao unyaukaji na kifo cha tishu za kiazi ( potato blight),
kuoza shingo (Bacteria soft Rot), minyoo fundo ( Root notes Nematodes), uozo wa
kahawia ( Brown Rot).
Magonjwa
na wadudu yaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia usafi wa shamba, kubadilisha mazao,
na kuzingatia udhibiti sango.
Mavuno ya
viazi hutofautiana kulingana na aina, hali ya hewa, na udongo. Mavuno ya viazi
yanakadiriwa kufikia tani 20 kwa hekta.
KILIMO BORA CHA VIAZI VITAMU
Reviewed by BENSON
on
January 30, 2018
Rating:
No comments