NUFAIKA KWA KILIMO BORA CHA STRAWBERRY

Image result for STRAWBERRY
Zao hili hustawi katika joto la wastani, na hukua kwa haraka zaidi na uzalishaji kuongezeka linapolimwa kisasa, hasa katika nyumba maalumu ya kuzalishia mimea yaani green house. Katika Tanzania zao hili linakuwa vizuri mikoa ya Morogoro na IringaZao hili hukua vizuri katika mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari.

Endapo unahitaji kuzalisha strawberry katika maeneo ya bondeni itakulazimu kuwa na maji kwa wingi kwa ajili ya umwagiliaji wa mara kwa mara. Strawberry inaweza kustawi vizuri kwenye udongo tifutifu wenye rutuba. Zao hili haliwezi kustahimili ukuaji kwenye udongo wenye chachu nyingi, hasa chokaa kwani mizizi yake huoza kwa urahisi.

KUPANDA
Ili kuwa na mazao bora ambayo yatakuwezesha kupata soko la uhakika, bila vipingamizi, inashauriwa kuzalisha kwenye nyumba maalumu ya kuzalishia mazao (green house). Katika kuzalisha strawberry baada ya kujenga green house andaa mabomba ya plastiki ambayo yatawezesha kutoboa matundu kwa urahisi Matundu katika bomba hilo yawe na umbali wa inchi 1.
1.    Ni vyema matundu hayo yakawa zigzag, ili kuruhusu mimea utakayopanda kukua vizuri bila kuwekeana kivuli.
2.     Tandika karatasi la nailoni sakafuni ili kuwezesha maji utakayotumia kunyeshea kurudi kwenye bwawa au sehemu ya kuhifadhia.
3.     Ning’iniza mabomba hayo kwa kutumia waya.
4.     Jaza kokote, yenye mapande makubwa kiasi.
5.    Panda miche kwenye kila tundu kwa uangalifu ili mizizi isikatwe na kokoto zinazoshikilia mmea. Kumwagilia Mimea ya strawberry inahitaji maji kwa kiasi kikubwa sana. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa umwagiliaji kabla ya kuanza kilimo cha zao hili.
6.    Unapaswa kumwagilia mara nne kwa siku, kila baada ya saa nne unapaswa kumwagilia kwa robo saa. Hii itawezesha mimea yote kupata maji ya kutosha. Endapo strawberry haitapata maji ya kutosha, uzalishaji wake pia utakuwa ni hafifu sana, kwani maua ya Strawberry inapooteshwa kwenye greenhouse hutoa mavuno mengi na yenye ubora yatachanua ipasavyo na hata matunda kukomaa inakuwa ni shida.

Mbolea
Uzalishaji wa kisasa wa strawberry, unaambatana na ufugaji wa samaki kwenye bwawa ndani ya green house. Mbinu hii husaidia mimea kupata mbolea inayotokana na chakula wanacholishwa samaki kwenye bwawa, kwani maji yanayofugia samaki ndiyo hayo yanayotumika katika mzunguko wa umwagiliaji. Hii inamaanisha kuwa hakuna mbolea nyingine inayohitajika kwa ajili ya strawberry. Wadudu na magonjwa Endapo strawberry inazalishwa kwenye nyumba maalumu ya mimea, hakuna magonjwa wala wadudu wanaoishambulia.
Uzalishaji wa green house.
Ikiwa mkulima anazalisha strawberry kwenye eneo la wazi, strawberry inaweza kushambuliwa na magonjwa ya ukungu, pamoja na magonjwa yanayosababishwa na virusi.
Dawa.
Endapo strawberry itashambuliwa na magonjwa ya ukungu na virusi, nyunyizia dawa za asili kama vile pareto na mwarobaini, na baada ya muda kutakuwa na matokeo mazuri.

Kuvuna.
Zao la strawberry, huzaliana na kukomaa kwa haraka sana. Unaweza kuanza kuvuna strawberry baada ya mwezi mmoja tangu kupandwa. Kila wiki strawberry inakuwa na matunda mapya, na kila tunda likishatokeza huiva kwa haraka, hivyo uvunaji wake ni wa mfululizo. Ikishafikia hatua hiyo tegemea kuwa na wiki 2 hadi 3 za kuvuna mfululizo.
Kwa kuwa matunda ya strawberry ni laini, epuka kushika tunda wakati wa uvunaji ili lisiharibike. Shika kikonyo cha tunda ili kuvuna kwa usalama. Usiache matunda yaliyoiva shambani kwa muda mrefu kwani yanaweza kusababisha mimea kuoza.
Pia yatapoteza ladha na virutubisho halisi vinavyotakiwa. Virutubisho Strawberry ina kiasi kikubwa cha virutubisho hasa vitamin B, C, K, na E . Pia yana wingi wa madini ya chumvi. Matunda haya husaidia kuchangamsha mwili na yana kiasi kidogo cha kalori.

Matumizi
Matunda ya strawberry yana matumizi mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji, jamii na maeneo. Miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na:
1.     Kuliwa kama tunda.
2.     Kutia ladha katika aina mbalimbali za vyakula. •
3.    Kuweka rangi, harufu na nakshi katika vipodozi. •
4.     Kutengeneza marashi n.k.
Soko:
Soko zuri kulingana na ubora wake. Kwa sasa gramu 500 za strawberry zinauzwa kati ya shilingi 5,000/= hadi 10,000/= za kitanzania.



NUFAIKA KWA KILIMO BORA CHA STRAWBERRY NUFAIKA KWA KILIMO  BORA CHA STRAWBERRY Reviewed by BENSON on January 31, 2018 Rating: 5

No comments