KILIMO BORA CHA BILINGANYA sehemu ya 2

Image result for kilimo bilinganya
Kuotesha mbegu.
Mbegu huoteshwa kwanza kwenye vitalu na baadaye miche kuamishiwa shambani. Kabla ya kusia mbegu tengeneza tuta lenye upana  wa mita moja na urefu wowote. Weka mbolea ya asili kama vile samadi au takataka zilizoooza vizuri, kiasi cha ndoomoja au mbili katika eneo la mita moja. Sia mbegu kiasi gramu mbili mpaka tatu katika eneo hilo. Kumbuka gramu 500 za mbegu zinatosha kusia katika eneo la hekta moja.

Lakini pia ikumbukwe nafasi kati ya mstari na mstari lazima iwe sentimeta 10 hadi 15 na kina kiwe sentimeter 1.5.

Kuhamisha miche ya bilinganya.
Miche huwa tayari kupandikizwa shambani mara baada ya wiki sita had inane. Wakati huwa na urefu wa sentimmita 15 hadi 20 amabyo ni sawa na kalamu moja ya risasi. Lakini unakumbushwa ya kwamba kabla ya kupeleka miche shambani ni muhimu kurutubisha shamba vizuri kwa mbolea ya asili.

Weka kiasi cha tani 10 za mbolea ya asili kwa hekta, hii ikiwa ni sawa maana ya kwamba kufanya hivi ni sawa na kwenda debe moja katika eneo la mita moja ya mraba. Mbolea yenye mchanganyiko wa N.P.K yenye uwiano wa  20: 10: 10  huwekwa kwenye shina wakati wa kupandikiza miche. Lakini pia kiasi kinachohitajika  ni gramu tano hadi tano kwa kila himo.

Kutunza shamba.
Kuweka matandazo.
Mara baada ya kupandikza miche, tandaza nyasi kavu. Matandazo husaidia unyevu, huzuia magugu yasiote lakini pia huongeza rutuba katika udongo.

Palizi.
Hakikisha shamba lako ni safi muda wote ili kuzuia ushindani wa chakula, maji na mwanga kati yam mea na magugu. Lakini pia palizi husaidia kubomoa maficho ya wadudu na kuzuia kuenea kwa wadudu.

Mbolea.
Weka mbolea ya S/A wiki tatu  mara baada ya mimea kuanza kutoa maua.  Mbolea hiyo huweka kwa kiwango cha gram tatu hadi tano huwekwa kuzunguka kila mche. Mbolea huwekwa umbali wa sentimita tano mpaka 15 kutoka shina hadi shina hii hutegemea na ukubwa wa mche.  Hakikisha mbolea haigusi mmea.

Kukata kilele.
Wiki mbili baada ya kupandikisha miche, kata sehemu ya juu ya mmea  kama umepanda aina ya mbegu ndefu. Kufanya hivi kusaidia kutengeneza umbile la kichaka.
Kumwagilia.

Zao la bilinganya hustawi vizur endapo litamwagiliwa vizuri, lakini ikumbukwe hali umwagiliaji ni lazima ufanyike mara mbili. Yaani asubuhi na join kutegemeana na hali ya hewa,

Usikose mwenedelezo wa somo hili siku ya kesho ambapo tutangalia kwa undani kuhusu
·         Wadudu waharibifu na jinsi ya kuwazuia wadudu hao.

Muhimu ni kuendelea kusoma blog yetu ya Kilimo Bora
KILIMO BORA CHA BILINGANYA sehemu ya 2 KILIMO BORA CHA BILINGANYA sehemu ya 2 Reviewed by BENSON on January 05, 2018 Rating: 5

No comments