JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA CHA “HYDROPONIC FODDER” NA NAMNA INAVYOWEZA KUKUPA MAFANIKIO MAKUBWA KWENYE UFUGAJI.
"CHAKULA BORA NA CHENYE GHARAMA NDOGO KWA MIFUGO. |
Hydroponics ni utaratibu wa kuotesha mimea kwa kutumia
maji bila kuhusisha mchanga/udongo kabisa. Mimea inaoteshwa katika chombo
maalum “tray” ambacho kipo safi na kina matundu kwa chini ili kusaidia maji
yasituame wakati unamwagilia mimea yako.
Tuangalie mfano wa uoteshaji mbegu za ngano kwa njia hii
ili zitumike kama chakula cha mifugo kama kuku, ng’ombe, mbuzi kondoo,
sungura n.k
VIFAA:
1.Tray ya plastic au aluminium yenye matundu (umbo lolote
tu).
2. Chupa ya kunyunyizia maji (sprayer).
3. Mbegu za ngano au shayiri(chagua ambazo hazijambunguliwa).
4. Chombo cha kulowekea mbegu (ndoo au beseni itafaa).
5. Chujio la plastiki au unaweza tumia kitambaa.
JINSI YA KUANDAA.
1. Pima uzito wa mbegu zako kisha zisafishe kuondoa
takataka zote.
2. Weka maji kwenye ndoo au beseni kisha weka mbegu zako
ili kuziloweka kwa masaa 4 mpaka 12(unavyoloweka muda mrefu ndio zinaota haraka
zaidi).
3. Baada ya kuloweka toa mbegu zako kisha chuja maji kwa
chujio au kitambaa safi.
4. Baada ya kuchuja mbegu zako zihamishie kwenye tray
kisha zisambaze ili zisibanane sana. (Kama huna trei tumia hata ungo).
5. Baada ya kusambaza mbegu zako kwenye tray funika mbegu
zako kwa kitu chochote kama nguo, gunia, kiroba tupu au ungo mkubwa juu yake
kwa masaa 48(siku 2). Katika hizo siku mbili kagua mbegu zako kama ni kavu
kisha mwagilia maji kiasi kuzilowesha. Hakikisha kifaa unachofunikia kina uwezo
wa kupitisha hewa au kina matundu. Endelea kufunika baada ya kunyunyiza maji.
6. Baada ya saa 48 mbegu zako zitaanza kuchipua, utaona
nyuzi nyuzi nyeupe zimeanza kutoka. Hamishia tray za mbegu kwenye kichanja au
eneo lolote lenye hewa ya kutosha lakini zikinge dhidi ya jua kali kwa kuweka
turubai au nailoni juu ya kichanja au tumia hata mifuko ya viroba, weka
kichanja chako mazingira salama ili kuzuia wadudu na ndege kushambulia mbegu
zako.
UMWAGILIAJI
Mwagilia angalau mara 3 kwa siku yaani asubuhi. Mchana na jioni. Hakuna haja ya
kumwagilia usiku kwasababu usiku hua kuna unyevu mwingi tu hivyo usishangae
hata asubuhi kukuta mbegu zako zina umande.
UVUNAJI
Unaweza kuvuna fodder zako baada ya siku 4 mpaka 9. Kumbuka kwamba unapoziweka
fodder zako muda mrefu zaidi (siku 7 – 9) ndio unapata fodder nyingi zaidi.
Lengo ni kupunguza gharama za chakula cha mifugo yako hivyo zalisha kwa wingi.
Mfano kilo 2 za ngano huzalisha kilo 4 za fodder ndani ya siku 4 lakini
ukiziacha ndani ya siku 7 – 9 zinazalisha kilo 12 – 16 za fodder
UPATIKANAJI WA CHAKULA MUDA WOTE.
Ili uweze kuhakikisha chakula cha njia hii kinakua tayari muda wote kwa malisho
ya mifugo yako ni lazima ujue mahitaji halisi ya chakula kwa siku. Kwa mfano
kama kuku wako wanakula kilo 25 za chakula kila siku, na kilo 2 za ngano
zimekupatia kilo 16 za fodder ndani ya siku 8, basi utahitaji kiasi gani cha
mbegu kuzalisha kila siku?
Chukua kilo 25 za chakula gawanya kwa kilo 16 za fodder ulizopata kutoka kilo 2
za mbegu. Utapata 1.5625 na jibu hili zidisha kwa 2 (kiasi cha mbegu
kilichozalisha kilo 16 za fodder). Jibu lake itakua kilo 3.125 za mbegu
utazohitaji kuotesha kila siku ili kuweza kuwalisha kuku wako.
Zoezi hili ili kua endelevu utahitaji kua na tray walau 8
ili kila siku upande tray 1. Hakikisha tray inatosha kutandaza mbegu zako na
kama haitoshi basi utalazimika kua na tray ndogo ndogo nyingi ili kutosha hizo
kilo 3.125 za mbegu kila siku.
USHAURI
Ili kuku wako wasipate shida ya mmeng’enyo wa chakula basi wape pumba kavu au
punje za mahindi kidogo kila baada ya siku 1 au 2. Virutubisho vilivyomo kwenye
fodder vinatosha kabisa kukuza mifugo yako bila shida yoyote.
Fodder za shairi hukua haraka zaidi kuliko ngano. Kama
unaweza kuzipata ni bora zaidi kuliko ngano. Kwa wale ambao hatuwezi kupata
mbegu za ngano au shayiri basi unaweza kutumia mbegu hata za mtama.
Hydroponic fodder Ni kizuri zaidi kwa sasa maana ni nafuu
kulinganisha na vyakula vingine. Hydroponic fodder Ni uoteshaji wa mbegu pasipo
kutumia udongo kwa muda wa siku5- 7 tu kilo moja ya mbegu za ngano au mtama au
shayiri au Mahindi zinaoteshwa kwa kumwagiliwa virutubisho maalum(NUTRIENTS) na
kuongezeka kutoka kilo moja hadi kilo 10 za CHAKULA.
Kwakuwa kuku mmoja hula gram kati ya 100-120gm hivyo kilo
moja ya mbegu ikitoa kilo kumi za fodder zinatosha kulisha kuku wakubwa 100 kwa
siku
HYDROPONIC FODDER NI CHAKULA CHA MIFUGO YOTE CHENYE FAIDA NYINGI SANA KAMA VILE
1. Ni nafuu sana kulinganisha na gharama za CHAKULA cha
madukani au viwandani.
2. Kina virutubisho na vitamini mara 3 zaidi ya CHAKULA
cha kawaida cha Mifugo.
3. Hupunguza magonjwa ya mfumo wa hewa kama vile mafua kwa
mfugaji na Mifugo kwani hakina vumbi kabisa.
4. Kina protein nishati nyingi zaidi mara 3 ya
inayopatikana kwenye vyakula vya kawaida vya Mifugo kama kuku,mifugo hukua
haraka sana kutokana na wingi wa protein ambayo hufanya Kazi ya kujenga mwili
na kukua.
5. CHAKULA hiki Ni laini sana na kitamu kwa kuku na Mifugo
yote.
6. Mmeng'enyo wa chakula hiki huongezeka kutoka 30% kwa
CHAKULA cha kawaida hadi 95% kwa CHAKULA cha hydroponic hivyo kupunguza kinyesi
na usumbufu wa usafishaji banda.
7. Kinyesi hupungua na kuwa kati ya 5%-10% tu kwani
CHAKULA kingi humeng'enywa na kutumiwa na mwili wa Mifugo.
8. Mazao kama mayai au maziwa huongezeka kwa 40%
kulinganisha na chakula cha kawaida,kiini cha yai la kuku anayelishwa
hydroponic fodder huwa cha njano sana hata kama ni kuku wa kisasa.
9. Hupunguza garama za ufugaji kwenye manunuzi ya chakula
kwa 50-75%.
FANYA UFUGAJI WA KISASA WENYE GHARAMA
NDOGO FAIDA KUBWA KWA KUTUMIA HYDROPONIC FODDER
JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA CHA “HYDROPONIC FODDER” NA NAMNA INAVYOWEZA KUKUPA MAFANIKIO MAKUBWA KWENYE UFUGAJI.
Reviewed by BENSON
on
January 06, 2018
Rating:
No comments