ZIJUE AINA ZA BILINGANYA ZINZOLIMWA KWA WINGI NCHINI TANZANIA
Bilinganya imo katika mimea ambayo inahusisha
jamii ya nyanya, pilipili, viazi mviringo na nyanya mmshumaa. Mboga hii
ina viiini lishe muhimu kama vile madini
ya chokaa na chuma, vitamin A, B, na C , wanga, protini na maji. Mboga hii
hutumika kutengeneza supu au hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali. Lakini
pia huweza kukatwa na katika vipande na kuhifadhiwa kwenye makopo.
Mazingira yafaayo kwa kilimo hiki ni hali ya
joto ya wastani , udongo wenye kina kirefu na rutuba ya kutosha na udongo
usiotuamisha maji.
Aina za bilinganya;
Aina za bilinganya ambazo hulimwa kwa wingi
hapa Tanzania ni kama ifuatavyo;
1. Peredeniya
Aina hii ya bilinganya huzaa matunda makubwa
kiasi yenye umbo la yai. Lakini aiana hii huvumulia sana magonjwa ya mnyauko wa
bacteria.
2. Black beauty.
Aina hii ya bilinganya huzaa matunda yenye
lrngi nyeusi, yenye ukubwa sana na umbo la mduara.
3. Frorida high bush.
Matunda yake ni makubwa na yenye rangi ya
kijani kibichi iliyochanganyika na nyeusi.
4. Frorida market.
Matunda ya frorida marketi yana umbo la yai. Aina
hii huzaa sana, lakini hushambuliwa kwa urahisi sana na ugonjwa wa mnyauko wa
backeria.
5.
Newyork
spineless.
Matunda ya newyork spineless ni ya mviringo,
makubwa na yana rangi za dhambarau.
Somo hili litaendelea siku ya kesho ambapo
tutangalia vitu vifuatavyo;
·
Kuotesha mbegu
·
Kuhahamisha mbegu kutoka kwenye
kitalu hadi shambani
·
Palizi
·
Mbolea
·
Kukata kilele
·
Umwagiliaji.
Muhimu;
usiasahu kusoma mwendelezo wa somo hili kupitia blogu yetu pendwa ya kilimo
bora.
ZIJUE AINA ZA BILINGANYA ZINZOLIMWA KWA WINGI NCHINI TANZANIA
Reviewed by BENSON
on
January 04, 2018
Rating:
No comments