JINSI YA KUZUIA WADUDU NA MAGONJWA KATIKA ZAO LA BILINGANYA, sehemu ya 3
Wadudu
waharibifu
Vinyotomvu.
Wadudu waharibifu
katika bilinganya hutambuliwa zaidi katika sehemu ya chini ya jani. Hufyonza utomvu
wa majani na kusababisha majani kuwa na mabaka meupe au njano. Mashambulizi yakizidi
majani huangauka chini. Vinyamtomvu wanaweza kuzuiwa kwa kunyunyizia moja ya
dawa zifuatazo;
1. Dimethoate
2.
Karate.
Vidukari.
Hawa ni wadudu
wadodgo wenye rangi nyeusi. Hushambulia majani machanga na kuyasababishia
huduma na kunjamana. Zuia wadudu hawa kwa kutumia dawa zifuatazo;
1. Dimercon 50% E.C
Utitiri
wa mimea.
Ni wadudu wadogo
wenye rangi nyekundu iliyoiva. Hushambulia mmea kwa kufyoza mtomvu. Majani yakishambuliwa
huonyesha utando kama wa buibui. Mashambulizi yakizidi mmea hudumaa, kukauka na
hatimaye kufa. Njia ya kuzuia wadudu hawa ni kubadilisha mazao shambani. Kwa mfano
mara baada ya kuvuana zao hili linalofuata liwe ni zao lingine. Pia dawa aina
ya furadan inaweza kutumika kuzua wadudu hao.
Magonjwa.
Mnyauko
backteria.
Ugonjwa huu husababishwa
na bacteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla wakati wa jua kali. Unaweza kuzuia
ugonjwa huu kwa kubadilisha mazao sahambani, na endapo kama ugonjwa huo utakuwa
umekithiri sana shambani unashauriwa
usipande zao hilo la bilinganya kwa muda wa miaka mitatu hadi mitano. Au njia
nyingine ni kupanda aina nyingine ya bilinganya ambayo nilieleza siku ya juzi.
Phomopsisi
Vexans.
Ugonjwa huu
husabaishwa na bacteria lakini pia hushambulia shina, majani na matunda
yenyewe.
Verticillium
wilt.
Husababuisha mmea
kudumaa, majani kunjamana na kuanguka, jinsi ya kuzuia ugonjwa huu ni kung`oa
mimea yote iliyoshambuliwa kish kuichoma
moto. Lakini pia inashauriwa shamba liwe safi muda wote.
Kuvuna
bilinganya.
Zao hili huvunwa
miezi miwili au mitatu tangu kupandikzwa kwake. Uvunaji hufanyika kwa muda wa
miezi mine, lakini paia inashauriwa uvune bilinganya mara baada ya matunda
kukomaa, kwani matunda yaliyokomaa sana hayafai kuliwa. Pia inasemakana kama
matunzo yote yakazingatiwa shamba la hekta moja linauwezo wa kutoa tani 50/60.
ASANTE SANA KWA
KUWA NASI HAPA KATIKA BLOG YETU YA KILIMO BORA, AMBAPO KWA SIKU TATU MFULULIZO TULIKUWA
TUNAJIFUNZA KUHUSU KILIMO BORA CHA BILINGANYA, TUKUTENE SIKU YA KESHO KWA SOMO
JINGINE, ASANTE
JINSI YA KUZUIA WADUDU NA MAGONJWA KATIKA ZAO LA BILINGANYA, sehemu ya 3
Reviewed by BENSON
on
January 07, 2018
Rating:
No comments