UMUHIMU WA KUTENGENEZA VIOTA VYA KUTAGIA MAYAI
Viota ni
mahali ambapo kuku hutaga mayai, kuhatamia na kuangua vifaranga. Hii
inamaanisha kuwa viota ni sehemu muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kupata
mayai mengi yaliyo salama pamoja na vifaranga.
Kuku anapotagia
porini, mayai huliwa na wanyama kama vile nyoka na wengineo. Kuku pia anaweza
kudhuriwa na wanyama hao na wakati mwingine kuibwa.
• Kwa
kuwa na viota vya kutosha itapunguza usumbufu wa kuingia kukusanya mayai kwa
mfugaji.
• Njia
mojawapo ya kuzuia kuku kula mayai.
• Upotevu
wa kuku na mayai utapungua.
• Utapata
mayai bora kwa ajili ya kutotolesha.
•
Kupunguza mayai kupasuka, pia mayai kuwa safi.
• Kuku
kuwa huru wakati wa kutaga au kuhatamia.
UMUHIMU WA KUTENGENEZA VIOTA VYA KUTAGIA MAYAI
Reviewed by BENSON
on
January 08, 2018
Rating:
No comments