JINSI YA KUZUIA MINYOO, VIROBOTO NA KUDOANA KATIKA UFUGAJI WA KUKU

Related image
Siku ya leo ningependa  tuangalie jinsi ambavyo minyoo, viroboto na kudoana vinavyooweza kusababishwa na jinsi ya kuzuia.

Tukianza kuangalia na minyoo

Dalili za kuku mwenye minyoo.
Kuku mwenye minyoo hudumaa na anakuwa mwepesi, damu hupungua (anaemia), kama nikuku wa mayai mayai hupungua na husababisha vifo.
Image result for minyoo ya kuku

jinsi ya kusuiya minyoo kwa kuku
Zingatia usafi. Ndugu msomaji wa mtandao huu minyoo wengi husababishwa na uchafu kwenye banda la kuku na unyevunyevu kwenye banda, unyevunyevu huo hupelekea minyoo kusambaa kwa wingi. Kwahiyo kama utazingatia usafi kuku wako watakuwa salama.

Badilisha maranda ya chumba cha kufugia kila kunapo kuwa kuchavu au kila unapo waingiza kuku wapya na pulizia huko dawa ya kuuwa wadudu wikimbili kabla ya kuwaingiza kuku wapya.
Pia nakushauri utumie dawa kama.Ascarex,piperazine, levifarm. Na zingatia ushauri wa daktari

viroboto na utitiri.

Dalili za kuku mwenye viroboto na utitiri.
Kuku hujikuna mara kwa mara, akiwa wa mayai anataga mayai machache, wadudu huonekana kwenye kope za maçho pia kuku hupungukiwa na damu.

Image result for minyoo ya kuku
Jinsi ya kuzuiya na tiba
Wadudu hawa mara nyingi huwapata kuku walioko kwenye banda chavu na lenye vumbi, ilikuepukana na wadudu hawa zingatia usafi wa mazingira na nyunyizia dawa kwenye banda aina ya. Pesticides ili kuuwa viroboto na utitiri


kuku kudonoana

Visababishi vya kuku kudonoana.
Upunguvu wa nafasi ya kutosha kwenye banda, rangi ya kuvutia ya manyoya hasa baada ya kujinyonyowa na kutoa manyoya upya, ncha kali ndani ya banda kama msumari, kuweka kuku walio pishana umri kwenye banda moja, pia upunguvu wa ptotin kwenye chakula cha kuku.
Related image

jinsi ya kuzuia
Tenganisha kuku wenye umri mdogo na wale walio na umri mkubwa, ondoa kuku wakorofi kwenye banda,


Ninginiza majani mabichi kwenyebanda na pulizia Wound spray kwenye vidonda vya walio donolewa, rekebisha ubora wa chakula au tumia chakula bora ambacho kina virutubisho sahihi na kwa kiwango sahihi.



JINSI YA KUZUIA MINYOO, VIROBOTO NA KUDOANA KATIKA UFUGAJI WA KUKU JINSI YA KUZUIA MINYOO, VIROBOTO NA KUDOANA KATIKA UFUGAJI WA KUKU Reviewed by BENSON on December 10, 2017 Rating: 5

No comments