KILIMO BORA CHA MTAMA
Mtama ni kundi la
mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi kikubwa cha
kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame kuliko mazao
mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua Pungufu na
hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa
kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya
kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia mikate ya
mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa (mnyoma-lugha ya
kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua yake yanaweza
kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza kutumika katika
kujengaea uwa .
HALI YA HEWA IFAAYO
Mtama ni zao linaloweza kustahimili ukame.Hivyo unaweza
kulimwa na kukua kuanzia ukanda wa chini wa bahari 0 - 100 mita hadi Mwinuko wa
mita 1500.pia unaweza kulima zaidi ya hapo lakini pasiwe na baridi kali mtama
haukubali seheme zenye baridi.Huitaji kiasi cha mvua cha wastani wa milimita
300 - 800 za kwa mwaka ili uweze kukua vizuri.Mtama hukubali sehemu zenye joto
hivyo huitaji nyuzi joto 18 - 33 °C.
ARDHI IFAAYO KWA
KILIMO CHA MTAMA
Mtama unapenda ardhi ambayo haituamisdhi maji na mwingine
unavumila katika ardhi inayotuamisha maji kidogo,hivyo kwa mavuno mazuri
usipande katika ardhi ambayo hutuamisha maji kwa ajili ya kupata mavuno
bora,kama ni udongo wa mfinyanzi hakikisha maji hayasimami shambani kwa muda
mrefu ikinyesha mvua.Mtama hukubali katika kichanga chenye rutuba au mchanganyiko
wa mchanga na mfinyanzi au mfinyanzi.Hukua vizuri katika udongo wenye soil PH 5
- 9.
MAANDALIZI YA SHAMBA
Andaa shamba lako mapema kabla ya msimu wa kupanda mtama
kuanza.Shamba lisafishwe na kulima kwa jembe la mkono,jembe la kukokotwa na
Ng'ombe au trekta na pia unaweza kupanda bila kulima (zero tillage).
MBEGU BORA ZA MTAMA
Zipo aina mbalimbali za mtama na mbegu zake.Aina hizi
hutofautiana kulingana na rangi zake,nyekundu,kahawia,nyeupe ambazo
zinajumuisha aina zaidi ya 20 za mtama duniani.Pia mtama na aina zake huwa kuna
ambao ni mtama mchachu (Hasa mbegu za kahawia na nyekundu),mtamu hasa Rangi
nyeupe.Wakulima wengi hupendelea mtama mweupe.Pia mtama wa mbegu sa kisasa huwa
laini kuliko mbegu za asili ambao ni mtama mgumu.Mtama wa asili huwa ni mbegu
ndefu kwenda juu na huchukua muda mrefu kupanda hadi kuvuna kuliko mtama wa
kisasa ambao mwingi ni mfupi na huchukua muda mfupi zaidi na hutoa mavuno bora
zaidi ya mtama wa asili.
AINA HIZO NI KAMA
VILE;
1.SEREDO
Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa
Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina
hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii
huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha Tani 2 kwa ekari moja. Ina uwezo wa
kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya
kahawia kwenye majani.
2.SERENA na DOBBS.
Aina hii huwana punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye
eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii
huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha Tani 1.5 kwa
ekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina
uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.
3.GADAM
Hufanya vizuri katika
sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama
hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na
ugonjwa wa majani.
4.HAKIKA NA WAHI
Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha
Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba
yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa
aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.
5.PATO na MACIA
Hizi hutoa mbegu nyeupe laini na hufaa kwa ugali na hata kwa
unga wa Dona (kusaga bila Kukoboa)
6.MBEGU NYINGINE
Tegemeo,Lulu,Sandala,Imani.
7.MBEGU ZA ASILI
Huchukua muda mrefu kupandwa hadi kuvunwa.Zaidi ya siku 120
UPANDAJI WA MTAMA
Mtama upandwe moja kwa moja shambani katika mashimo katika
kina cha sentimeta 2.5 hadi 5.Kiasi cha mbegu kupanda inategemea nafasi na aina
ya mbegu unayopanda na aina ya upandaji,Mbegu ambazo hupndwa kwa nafasi ndogo
ndogo huchukua kiasi cha kg 2.5 hadi 5 na ule ambao hupandwa kwa nafasi kubwa
huchukua Kg 2.5 - 3 kwa ekari
NAFASI ZA UPANDAJI
kwa mtama wa asili tumia Sentimeta 70 kwa 30 au Sentimeta 80
kwa 30 ,kwani huu huwa ni mrefu zaidi kwenda juu na pia katika shina acha miche
2 au 1 ambao huwa na afya zaidi.
mtama wa kisasa tumia nafasi ya sentimeta 60 kwa 15 au 60 kwa
20
Muda wa kupanda mtama ni pale msimu wa mvua unapoanza
kulingana na siku za mtama wako kupandwa hadi kuvunwa ili kuuepusha kuvuna
katika kipindi cha mvua.Pia mtama wa asili ukipanda mapema zaidi unaweza
kukusumbua kwa kupata tatizo la kuanguka kipindi ambacho mvua huwa nyingi
zaidi.Hivyo usipande mapema sana msimu wa mvua unapoanza.
KILIMO MSETO -unaweza kuchanganya mtama na mazao mengine japokuwa
kama ni kilimo cha biashara haishauriwi kufnya hivyo.unaweza kuchanganya mtama
na mazao kama vile Kunde,maharage,choroko n.k
7.PALIZI
Palizi ya mtama ifanyike mapema mara tuu mtama wako unapoona
unaanza kushambuliwa na magugu.Kipindi cha mwanzoni mimea ya mtama huitaji hali
ya usafi zaidi kuliko unapokuwa mkubwa hivyo huitaji kupaliliwa mara mbili
kupandwa hadi kuvunwa.
Pia kama katika shimo kuna miche zaidi ya miwili inabidi
ipunguzwe mapema tuu katika palizi ya kwanza.Pia unaweza kupalilia kwa kutumia
Dawa maalum za palizi za Magugu ambazo uantakiwa uwe mwangalifu usipulize
katika mtama mdogo au katika majani ya mtama wako.
MBOLEA
Mtama unaweza kuvumilia katika shamba lenye rutuba kidogo
lakini hustawi zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.hivyo unaweza
kutumia mbolea za samadi katika kupanda au mbolea za viwandani kama vile DAP au
TSP na kukuzia mbolea za CAN au UREA kiasi cha kg 50 kwa ekari.
WADUDU NA MAGONJWA
WADUDU
Mtama hushambuliwa zaidi na ndege (Quelea) Kwelea kwelea.Pia
Funza wa Mabua na wadudu wengine ambao unaweza kuwazuia kwa kupuliza dawa za
wadudu kama vile DUDUBA, .Ndege unaweza kutumia mbinu mbalimbali za kufukuza au
kama ni wengi kuwasiliana na kitengo cha udhibiti wa ndege kwa msaada zaidi.
MAGONJWA.
Ugonjwa mkuu wa mtama ni KUTU (smuts) ambapo unaweza kuzuia
kwa kupuliza dawa za ukungu.
UVUNAJI WA MTAMA NA
MUDA WA KUKOMAA
Mtama huchukua siku tofauti za kupandwa kukomaa hadi kuvunwa
kulingana na aina ya mbegu uliyopanda Kwa kawaida huchukua siku 120 - 150 Mtama
mrefu na siku 115-120 Mtama Mfupi.Mtama ukishakomaa na kukauka huvunwa kwa
kukatwa masuke yake kwa kisu kikali kwa mtama mfupi na kuangushwa chini na
kukatwa masuke kwa kisu kwa mtama mrefu.Pia ili kuuwahisha kuvuna mtama unaweza
kukata mabua yake na kuulaza chini shamabani hadi utakavyokauka vya
kutosha.Kisha baada ya kukauka masuke yake hupigwa kwa fimbo au magongo katika
turubai safi au sakafu ya sementi ili kuutenganisha na masuke yake,Pia kuna
mashine maalumu za kufanya kazi hii.
KUHIFADHI
Mtama ukishavunwa
na kukaushwa vizuri huifadhiwa katika magunia maalum ambayo hayaruhusu wadudu
kupenya na kuharibu mtama au kwa kutumia magunia ya kawaida ambapo mtama kabla
ya kuwekwa huchanganywa na dawa maalum za wadudu kama vile Akteliki au
SHUMBA.Yahifadhi magunia yako katika sehemu kavu isiyo na unyevu.
MTAMA kwa kawaida ukilimwa vizuri hutoa wastani wa Tani 1
hadi 2.5 kwa ekari
SHUKRANI-Nashukuru kwa ushirikiano wako nataraji hili litakuwa
lenye manufaa kwa kilimo chako cha mtama.
KILIMO BORA CHA MTAMA
Reviewed by BENSON
on
November 28, 2017
Rating:
No comments