KANUNI ZA KILIMO BORA UNACHOTAKA KULIMA.
Kwa kilimo chochote kile ambacho unatamani sana kukifanya
zipo kanuni na taratibu zake za kuweza kufanya hivyo. Baadhi ya mambo ya msingi
ambayo ni muhimu kuweza kufanya hivyo ni pamoja na;
KUTAYARISHA SHAMBA MAPEMA:
Shamba ni lazima litayarishwe mapema. Matayarisho hayo ni
pamoja na kufyeka, kukwatua na kulima.
KUTUMIA MBOLEA:
(a). SAMADI: Ihamishiwe shambani mapema kabla ya mvua
kuanza.
(b).MBOLEA ZA VIWANDANI: Tumia mbolea za kupandia kama vile Minjingu Rock
Phosphate (MRP), DAP na NPK. Zikifuatiwa na za kukuzia kama UREA na CAN.
UPANDA MAPEMA:
Panda mara mvua za kwanza zinapoanza kunyesha.
KUTAYARISHA MBEGU BORA MAPEMA:
Nunua mbegu au tayarisha mbegu nzuri kutokana na mavuno
yaliyopita kama ulitumia mbegu mchanganyiko.
Mbegu chotara (hybrid) zisirudiwe. Mbegu bora ziwe zilizopendekezwa kwenye
ukanda/eneo lako.
PANDA KWA NAFASI ZINAZOTAKIWA:
Hakikisha umepanda kila zao kwa nafasi maalum
inayoshauriwa kitaalam. Rudishia mapema pale ambapo mbegu hazikuota.
KUPALILIA VIZURI NA KWA WAKATI:
Hakikisha shamba lako halina magugu wakati wote kwa
kupalilia mapema. Wakati wa kupalilia punguzia miche na kuinulia matuta.
KUDHIBITI MAGONJWA, WADUDU NA NDEGE
WAHARIBIFU WA MAZAO:
Tumia njia za kitaalam za kudhibiti magonjwa, wadudu na
ndege waharibifu wa mazao.
KUVUNA MAPEMA:
Vuna mazao yako mapema mara yanapokomaa na kukauka vizuri.
Vuna kwa wakati ili kuepuka mazao yako yasiharibike kwa jua, mvua na wadudu.
KUHIFADHI MAZAO VIZURI:
Mara baada ya kuvuna na kukausha mazao vyema, hifadhi
kwenye vyomvo vya kuhifadhia kama vile vihenge na magunia. Hakikisha umeweka
dawa za kudhibiti wadudu waharibifu.
KUSAFISHA SHAMBA MAPEMA BAADA YA
KUVUNA:
Ng'oa mabua na masalia ya mazao na kuyalaza kati ya matuta na kuyafunika kwa
udongo ili yaoze mapema. Kwa mazao ya tumbaku na pamba ng'oa na kuchoma moto
mabua yake mapema.
KANUNI ZA KILIMO BORA UNACHOTAKA KULIMA.
Reviewed by BENSON
on
October 27, 2017
Rating:
No comments