MCHANGANUO WA TSHS 300,000 (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Wapo watu
mbalimbali ambao wana ndoto za kufuga kuku lakini wengi wao wamekuwa hawaelewi
waanzie wapi, ila ukweli ni kwamba mara nyingine ukiwa una pesa mkononi unaweza
ukajikuta unakosa cha kufanya, hii ni kwa sababu pesa ina makelele hasa pale aipatapo
mtu. Ila kama unazo pesa leo nitakupa mchanganuo jinsi ya kufuga kuku.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanaotaga yani majike 10
na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na
kuku mia Tatu (300) au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa
usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao
safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.Tafuta sehemu ya uhakika na nunua
kuku wenye matunzo na kinga ili wasipatwe na magonjwa na wenye afya nzuri.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza kabisa wape chanjo ya mdondo
(Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa
kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo
wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda la kutosha kulingana na
idadi ya kuku na kwa ajili ya badae kwa kuwa mradi utaongezeka kadri siku
zinavyoenda na Chakula.
Mchangunuo huo wa kufuga kuku ni kama ifuatavyo;
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha
kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material
ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.
-baraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo
vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
-mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
- layer's consetraite Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo
kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8. Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe
kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape
kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku.
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo
ni gram 1300. Hivyo tutaweza kuona
Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000
AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake
Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa
shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500.
Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei
nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa
kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana
wakati wakutaga.Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao
itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga
nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda
juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama
mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito
mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh
50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh
25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi
hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo
wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000. Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku
ambapo kwa mwezi ni Mayai 240.
Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea
(incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga
200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni
wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha
kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya
kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200.
Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na maana
kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni
wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii
itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu
yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo
na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa
miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndiyo kitakuwa kinaishia hapa
utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi
cha kula Chakula chochote. Kumbuka kujibana ili kuongeza banda kwa ajili
ya kufugiia kuku.
MCHANGANUO WA TSHS 300,000 (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Reviewed by BENSON
on
August 31, 2017
Rating:
No comments