KANUNI BORA ZA KILIMO CHA MACHUNGWA
Mchungwa ni jamii ya mlimao, lakin hustawi zaidi ukandawa
pwani wenye joto kiasi, mvua zaidi na udongo wenye rutuba. Hapa Tanzania mikoa
kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa
kilimo hiki. Pia tunda la mchungwa huliwa na binadamu ili kuongeza vitamini
mwilini.
Hali ya hewa.
Michungwa huweza kukuzwamaeneo yenye joto na hata yale yenye
baridi. Kama ilivyo kwa matunda mengineya citrus, ili kupata mazao mazuri haina
budi kukuza michungwa katika joto la nyuz ijoto 15.5c – 29c.
Kuandaa mbegu.
Mchungwa kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika
malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake
na kasha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.
Kuandaa kitalu.
Tengeneza kitalu chako vizuri kwa kutumia jembe, kisha
changanya na mbolea za mboji au samadi baada ya kukauka vema mwaga mbegu zako
na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimita, kasha mwagia maji kila siku na
baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kichipua, baada ya miche kufikia kiasi cha
sentimita 3 – 5, miche ihamishwe kwenye pakiti zenye udongo (viriba) wenye
mbolea ya kutosha na viwekwe kwenye kivuli kiasi.
Kuunga miche.
Miche ikifikia urefu wastani wa sentimita 30 – 45 huungwa ili
kupata michungwa. Kwa michungwa kuna aina mbili kuu hapa Tanzania ambazo ni
Jaffer na Valencia. Jaffer ni rahisi kuunga sababu vikonyo vyake ni vikubwa na
viko wazi kwenye miti, miti yake ni mikubwa na inazaa sanalakini huathirika
sana jua likiwa kali na matunda yake huanguka, pia machungwa yake hukua kwa
haraka sana ilasoko likiwa baya huishia shambani kwa kuanguka. Vlencia ni miti
ya wastani , vikonyo havipo wazi kwa hiyo huwapa kazi waungaji (hawaipendi) ina
uzao wa wastani na inakaribia ukame na matunda yake hayaivi haraka.
Upandaji.
Baada ya uungaji kukubali unaweza kuandaa shamba lako kwa
kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kusubiri msimu wa mvua, miche ipandwe mara
tu baada ya mvua za kwanza kunyesha, umbali wa kupanda ni mita 8 * 8 kwa Jaffer
na mita 5 * 8 kwa Valencia.
Palizi na matumizi
ya mbolea.
Palizi ifanyike si chini ya mara 2 – 4 kwa mwaka na miche
ikifikisha miaka 3 unaweza ukasafishia miaka mitatu unaweza ukasafishia
visahani na kufyeka sehemu nyingine. Kwenye mbolea weka samadi iliyoiva debe
moja hadi mbili kwa shimo, changanya mbolea na udongo wa kwanza kutoka shimoni,
iwapo itatumika mbolea ya viwandani kama DAP, TSP, NPK na Mijingu Phosphate
changanya mbolea hiyo na udongo wa juu wenye mboji (top soil).
Uzao.
Kuanzia miaka mitatu miche itaanza kutoa maua na kuzaa na
huchanganya kuzaa baada yamiaka mitano, miche huendelea kuzaa hadi kufikia
miaka mitano 25 – 30 tangu kupandwa.
Magonjwa na wadudu
katika michungwa.
Magonjwa.
1.Vidonda katika
shina .
Huletwa na aina fulani ya ukungu. Dalili za ugonjwa huu
nikutokea sehemu ya shina ambayo hubadilika rangi.
Dalili; Huongezeka ukubwa na baadae kutoa utomvu.
Kudhibitisha; Hutokea sana sehemu iliyo na udongo ambao
huatamisha maji.
2. Ugonjwa wa
kukauka miti.
Husababishwa na virusi ambavyo husambazwa na chawa weusi.
Dalili; Sehemu ya shina hunyauka na ndani yake hutokea
mipasuko pasuko,kasha mmea hudhoofika polepole na kutoa matunda madogo madogo,
na majani hubadilika ghafla na kuwa ya njano.
3.Ugonjwa wa
kutobadilika rangi kwa machungwa yanapokomaa.
Hutokea hasa kwenye sehemu za miinuko ya kati na kusambazwa
na vidudu viitwavyo psyllids, na vile vile kwa kuchukua vikonyo na kubebeshea
kutoka kwenye miti inayoonyesha dalili za ugonjwa.
Dalili; Hutokea mabaka ya njano kwenye majani, pia matunda
huwa ya ukali nay a njano sana.
KUZUIA:
Sehemu ambazo ugonjwa unaweza kutokea angalia wadudu kama
chawa. Hakikisha wadudu hawa hawashambulii miche kwenye kitalu. Wakiwepo,
majani huonyesha kujikunja kwa kuweka mafundo sehemu ya juu. Vilevile epuka
kuchukua vikonyo kutoka kwenye miti yenye dalili za ugonjwa huu.
WADUDU:
1.Nzi weupe (white fly).
Hawa ni wadudu ambao hukaa kwenye majani ya mimea wakizaliana
na kufyonza virutubisho vya mmea, na hii husababisha mmea kudumaa na kutoa
mazao duni.
Kuzuia:
Njia ya kiusalama zaidi ni kwa kupandisha shambani wadudu
aina ya Cales noacki ambao huwala hawa nzi weupe na kuzuia kusambaa kwao.
2.Wadudu mafuta
(aphids).
Hawa ni wadudu weusi ambao hukaa kwenye majani ya mimea
wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, nah ii pia husababisha mmea
kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Tumia kiuwa wadudu (insectside).
Kuvuna
Mchungwa huwa tayari kuvunwa miezi 3 – 4 baada ya kupandwa.
Kuvuna ni kwa njia ya mikono au kwa kutumia kikapu cha kuvunia.
Hifadhi
Machungwa huhifadhiwa kwenye ghala safi lenye kuruhusu hewa.
Ghala lijengwe nje ili kuruhusu hewa safi ili yasioze.
Soko
Soko la ndani na nje ya nchi lipo. Kiasi kikubwa cha
machungwa hutumika hapa nchini, pia huuzwa nchi za jirani. Bei ya chungwa ni
shilling 200 – 300 kwa kila moja na hadi 500 hufikia kulingana na aina ya msimu.
KANUNI BORA ZA KILIMO CHA MACHUNGWA
Reviewed by BENSON
on
August 29, 2017
Rating:
Asante kwa elimu tumekupata. ila kwa bei 200-300 umeenda mbali sana chungwa kwa mkulima ina range 20 tsh hadi 50 tsh hii ndo uhakika hayo ya wafanya biashara. hapa mtu anaetaka kuwekeza anaweza kadiria kwa kiwango hicho cha chini na si huko kwa 200-500
ReplyDelete