UFUGAJI BORA WA MBUZI-sehemu ya 01

Ufagaji wa mbuzi ni rahsi endapo utaamua kujitoa kikamilifu katika ufagaila ingawa kuna wakati mwingine huwa ni kazi ngumu sana kufuga endapo hutajitoa kikamilifu katika kufuga. Pia watalam wa mifugo wanasema ya kwamba ufagaji wa mbuzi hasa katika maeneo ya vijinini ni bora kwa sababu hutumii gharama kubwa za kuwalisha, ukilinganisha na ufagaji wa mbuzi maeneo ya mjini.

Mambo ya msingi ya kuzingatia katika ufugaji wa mbuzi.

1.    Wafugwe kwenye banda au zizi bora,
2.     Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji (nyama, maziwa au sufu),
3.     Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili,.
4.    Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na mtaalam wa   mifugo,
5.     Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji na kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko

Zizi bora kwa ajili ya kufugia mbuzi lazima liwe lenye sifa zifuatazo:-


1 1.   Lililo imara linaloweza kumkinga mbuzi/kondoo dhidi ya wanyama hatari na wezi,
  2.  Lililojengwa mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama,
3 3. Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo. Ni vema mbuzi/kondoo watengwe    kulingana na umri wao; na
4 4. Liruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
5   5. Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa
hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama
hatari,
6 6.  Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika
kwa urahisi,
7 7. Lijengwe sehemu isiyoruhusu maji kutuama na liwe mbali kidogo na
nyumba ya kuishi watu. Pia ujenzi uzingatie mwelekeo wa upepo ili hewa
kutoka bandani isiende kwenye makazi,
8  8. Liwe na sakafu ya kichanja chenye urefu wa mita 1 kutoka ardhini (Kwa
banda la mbuzi),
9  9.  Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji na mahali pa kuweka jiwe la
chumvichumvi; na
1 10. Liwe na vyumba tofauti kwa ajili ya majike na vitoto, mbuzi/kondoo wanaokua, wanaonenepeshwa na wanaougua.

Mbuzi jike wanaofaa kwa ajili ya kuzalisha maziwa na nyama wawe na sifa
zifuatazo:-
• Historia ya kukua upesi, kuzaa (ikiwezekana mapacha) na kutunza vitoto
vizuri,
• Umbo la mstatili linaloashiria utoaji wa nyama nyingi
• Asiwe na ulemavu wa aina yoyote.

Sifa za Ziada kwa Mbuzi wa Maziwa
• Awe na miguu ya nyuma iliyo imara na iliyonyooka na yenye nafasi kwa ajili ya kiwele; na
• Awe na kiwele kikubwa na chuchu ndefu zilizokaa vizuri

Sifa za ufugaji dume bora awe na sifa zifuatazo:-
• Miguu iliyonyooka, imara na yenye nguvu,
• Asiwe na ulemavu wa aina yoyote,
• Mwenye uwezo na nguvu ya kupanda
• Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri na zinazolingana.

Utunzaji wa Vitoto vya Mbuzi/Kondooa
Utunzaji huanza mara tu baada ya kuzaliwa.
Mfugaji ahakikishe:-
• Kitoto cha mbuzi kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) ndani ya
masaa 24 tangu kuzaliwa na kwa muda wa siku 3,
• Kama kinanyweshwa maziwa, kipewe lita 0.7- 0.9 kwa siku. Maziwa haya, ni
muhimu kwani yana viinilishe na kinga dhidi ya magonjwa,
• Iwapo mama hatoi maziwa au amekufa, inashauriwa kutengeneza dang’a
mbadala au kama kuna mbuzi/kondoo mwingine aliyezaa anaweza kusaidia
kukinyonyesha kitoto hicho,
• Kitoto cha mbuzi/kondoo kiendelee kunyonya kwa wiki 12 - 16. Wiki 2 baada
ya kuzaliwa, pamoja na maziwa, kianze kupewa vyakula vingine kama nyasi
laini na chakula cha ziada ili kusaidia kukua kwa tumbo. Aidha, kipewe maji
wakati wote,
• Vyombo vinavyotumika kulishia vinakuwa safi muda wote,
• Kitoto cha mbuzi/kondoo kiachishwe kunyonya kikiwa na umri wa miezi 3 hadi
4 kutegemea afya yake.
• Vitoto vipatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.
Matunzo Mengine

Utambuzi
Mbuzi huwekewa alama ili atambulike kwa urahisi na kuwezesha utunzaji wa kumbukumbu zake. Shughuli hii hufanyika kwa mbuzi/kondoo akiwa na umri wa
siku 3 - 14. Njia zitumikazo ni pamoja na:
• Kuweka alama sikioni kwa kukata sehemu ndogo ya sikio,
• Kumpa jina kwa wafugaji wenye mbuzi wachache,
• Kumvisha hereni ya chuma au plastiki yenye namba kwenye sikio,
• Kumvalisha mkanda wenye namba shingoni; na Kuweka namba kwa kuunguza sehemu ya ngozi ya mbuzi. Pale mfugaji anapotumia njia hii inashauriwa aweke alama kwenye eneo ambalo halitaathiri ubora wa ngozi

Ili mbuzi aweze kukua na kufikia uzito wa kuchinjwa/kupevuka mapema,
mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:-
• Kumpatia vyakula vya ziada kwa muda wa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo 0.2 –
0.7 kwa siku kuanzia anapoachishwa kunyonya.
• Kumpatia dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 na kutoa kinga za
magonjwa mengine kama itakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo, Kuchanja na kuogesha ili kuzuia magonjwa mbalimbali,
• Kukata kwato mara zinapokuwa ndefu
• Kuhasi madume yasiyotumika kuzalisha

Itaendelea.......kesho
UFUGAJI BORA WA MBUZI-sehemu ya 01 UFUGAJI BORA WA MBUZI-sehemu ya 01 Reviewed by BENSON on July 22, 2017 Rating: 5

No comments