BANDA BORA LA KUKU LAZIMA LIWE NA SEHEMU ZIFUATAZO.

Image result for ufugaji kuku
Kwa mfugaji yeyote yule ili aweze kupata faida katika ufugaji ambao anaufanya ni lazima aweze kuzingatia kanuni na misingi bora ya ufugaji, na miongoni mwa misingi bora ya ufugaji wa kuku ni pamoja na kuangalia sehemu za banda kwa ajili ya kufanya ufugaji huo
Zifuatazo ni sehemu za banda bora la kuku kulingana na aina ya kuku:-

1. Sehemu za kutagia (kama ni kuku wa mayai au wa kienyeji).
Katika banda bora la kuku wanaotarajiwa kutaga inapaswa kuwepo na sehem za kutagia zijulikanazo kwa jina la viota. Viota vinaweza kutengenezwa kwa mtindo wa kuku mmoja mmoja au ushirika.

2. Sehem ya kutembelea.
Ni ukumbi mkubwa kulingana na idadi ya kuku, ambao ndani yake kunakuwa na vyombo vya maji na chakula, pamoja na kuku wenyewe.

3. Sakafu
  Zipo aina mbalimbali za sakafu kama ifuatavyo:-
    a) Sakafu ya saruji
Ni vema zaidi ukajenga sakafu ya saruji kisha ukaweka maranda juu yake ili kuzuia ubaridi unaotoka sakafuni, na vilevile kupata wepesi wakati wa kufanya usafi.

     b) Sakafu ya udongo au mawe

Jaza udongo wa mfinyanzi au mawe kisha siliba vizuri acha pakauke mwisho weka maranda kwa wingi.

     c) Sakafu ya chaga
 Banda hujengwa kisha huwekwa chaga umbali wa futi mbili kutoka chini, chaga inaweza
 ikawa ya banzi, "chicken wire" au fito ili kuruhusu kinyesi cha kuku kudondoka choini.

4. Ukuta
 Unaweza kujenga ukuta kwa kutumia nguzo, pamoja na mabanzi au fito kisha kuzibwa vizuri na kuacha sehemu kubwa kwa ajili ya madirisha. Pia unaweza kutumia tofali za kuchoma, saruji au tofali za udongo kwa kujengea na kuacha sehem kubwa kwa ajili ya madirisha.

5. Paa
Vifaa vya kuezekea vinaweza kuwa ni vigae, nyasi, makuti au bati.
BANDA BORA LA KUKU LAZIMA LIWE NA SEHEMU ZIFUATAZO.  BANDA BORA LA KUKU LAZIMA LIWE NA SEHEMU ZIFUATAZO. Reviewed by BENSON on December 09, 2017 Rating: 5

No comments