KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
Pilipili mbuzi ni zao ambalo linaweza kulimwa kibiashara
na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua
angalau kiasi cha masaa 6 kwa siku.
Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea
ya asili, undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.
Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni chini ya 6.0
ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya udongo imefika 8 onana na
wataalam wa kilimo wakusahuri namna ya kuipunguza.
Kuandaa miche.
Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya
kwenda kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu week 7 hadi 10
kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche shambani. Panda mbegu tatu
tatu kwenye kila kishimo na chagua mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya
kuhamishia shambani.
Kuhamishia miche shambani.
Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa kuhamisha ikiwa na
majani machache au mengi zaidi haitapelekea shida yoyote.
MUHIMU...Unashauriwa kuhamisha miche shambani kwa kuzingatia mambo
yafuatayo.
1. Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au
mahali ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri siku
zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.
2. Chimba mashimo marefu kuzidi urefu wa mizizi ya miche
kisha changanya vyema udongo na mbolea ya Ngo’ombe. Muda mzuri wa kuhamisha
miche yako shambani ni jioni au kipindi ambacho jua limefifia kuepuka miche
kukauka.
3. Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia
na rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia kuuwa
fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia huasaidi mizizi kusambaa
na kukua kwa haraka na kupata virutubisho.
4. Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia
shambani hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa mazingira.
Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.
Mahitaji ya mmea.
Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji yasiwe
yenye ktuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda vya pilipili vimeanza
kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna unyevu wa kutosha hupelekea maua
kudondoka. Epuka umwagiliaji ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji.
Unaweza kutandaza nyasi kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea
huanza kutoa maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Maua ya mmea hua na set
iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza kujichavusha
yenyewe.
Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza
uchavushaji.
Mbolea
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia
mbolea,wakati huu tumia Yaramila winner 5-10g kwa mche.NB:Usitupie
juu..hakikisha mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na mmea,weka
4-6 cm kutoka kwenye mmea.
Na kila baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila
winner au NPK Isipokuwa wakati maua yameanza weka Yaramila nitrabo au CAN 10g
/plant,na baada ya hapo utaendelea na Y-winner mpaka mwisho wa mavuno.
Kupalilia.
Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo
basi mkulima anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia
kuepuka kukata mizizi.
Magonjwa.
1. Fusarium wilt (Mnyauko)
Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili kupunguza joto.
•Ng'oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.
•Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba na chini ya miguu
uingiapo shambani.
•Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya kutosha.
•Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.
2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi weupeweupe (Whitish
fungal growth on the stems of infected plant) .Majani ya chini huweza
kunyauka,Huu ungonjwa hutokea muda mfupi kipindi cha joto kali.
Kuepuka/Kuzuia.
•Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi
waende chini sana ambapo mizizi haifiki.
•Mimea iliyoshambuliwa...Ing'oe yote na choma moto lakini chomea nje ya eneo la
shamba.
•Pulizia Ortiva.
3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa huweza kukaa
ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama kuna sehemu zinakuwa nyeusi
na panajaa majimaji ...dalili hii huenea sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda
huoza.
Kuepuka.
Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya
kuvuna choma mabaki yote.
•Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo zaidi ya
mara mbili...badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio jamii moja na pilipili
mbuzi (Do crop rotation).
•Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu...kwa hiyo mkulima lazima achukue mbegu
kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na mwaminifu...mbegu hazitakiwi kutengenezwa
kutoka kwenye mimea iliyoathirika na ugonjwa.
4) Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda....huweza kutokea na kusambaa haraka
wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia huu ugonjwa huweza kuenea
kupitia mbegu.
Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na pia kwenye
matunda.
Kuepuka.
•Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu ugonjwa.Nunua kutoka
kwa wakala.
•Pulizia dawa yoyote copper.
5) Virusi.
Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili
mbuzi.
Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .
Kuepuka.
•Nunua mbegu bora
•Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na kuendelea.Wadudu
wanaosababisha virus sanasana na wadudu mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda
wote shambani hakuna hao wadudu kwa kupulizia Actara.
NB:Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila kupiga dawa ya
wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna ugonjwa.
Wadudu.
Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;
1. Wadudu mafuta ( Aphids)
Kuwadhibiti.
Tumia Actara 8g/20L.
Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.
2. Crickets
Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka
walipo jificha na kukata miche michanga.
Kawadhibiti.
Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na
kuwaacha katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama ni
miche na iko kwenye tray...basi weka hizo tray juu ya kichanja.
3. Beetle.
Tuma Karate 40cm/20L.
4. Utitiri
Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.
5. Nematodes
Tumia solvigo.
Mavuno.
Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina ya mbegu
uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili uendelee kuzalisha.
Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi 1 hadi 3.
Usalama wakati wa uvunaji.
Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza
kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa gloves wakati wa
kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye macho.
Soko.
Fursa
Pilipili ni zao ambalo halina mbadala wake au (substitute)
hivyo kufanya mahitaji yake kuwa ni ya muda wote bila kutetereka.
Changamoto
Muda ambao wakulima wengi wanakuwa wamezizalisha zaidi huathiri sana soko la
pilipili kwa maana hata bei ikishushwa sana haiwezi kushawishi watumiaji
kutumia pilipili nyingi zaidi.
Kuepuka changamoto hiyo wakulima wanashauriwa kupunguza huduma shambani hadi
pale soko litakapo tengemaa vizuri.
Mbinu za mafanikio kwenye kilimo
hiki.
1. ZALISHA KWA WINGI
Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo haziepukiki yani
(Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo utaweza pia uza bidhaa
zako kwa bei ndogo na bado utapata faida nzuri na kujihakikishia soko la
uhakika kwa bidhaa zako.
2. TAFUTA MASOKO YA BIDHAA KABLA YA
KUANZA UZALISHAJI
Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri ukiachilia
mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema kutengeneza channels mapema
kupata wateja wa mazao yako. Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia
sana kwenye kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza
wateja na wateja watakutengenezea biashara.
Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.
•Unafuu wa bei
•Ubora wa zao
•Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa
Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa umejihakikishia
soko la uhakika.
3. USILIME KWA KUFUATA MSIMU
Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi mmezalisha zao fulani kwa
wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa
kuliko inavyo hitajika kwenye masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei
ndogo na kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara muda
mwingine.
Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/mazao kipindi
ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji yatakuwa makubwa na upatikanaji wa
zao hilo utakuwa ni mdogo hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao
yake.
4. USIFANYE KILIMO KWA MAZOEA
•Tumia wataalamu wa kilimo
•Tumia njia za kisasa za kilimo
•Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia wataalamu)
•Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho wengine hawawezi
kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri zaidi,
FAIDA ZA KUTUMIA PILIPILI
1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu.
2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu
wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa
timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika
American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.
3. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula
Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini
kwa 60%. baada ya kula chakula.
4. Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye
tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu.
Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili.
5. Pilipili husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi
pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi.
6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani
ya kwenye tumbo (Stomach Cancer).
7. Pilipili husaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic,
ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na
metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.
8. Kula pilipili husaidia kupunguza cholesterol, na
kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.
KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
Reviewed by BENSON
on
July 29, 2017
Rating:
No comments