JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI
Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za
kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa
kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo
itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.
Mahitaji
1. Pumba ya mahindi sadolini 1.
2. Pumba ya ngano au
mpunga sadolini 1.
3. Dagaa sadolini 1.
4. Kilo moja ya soya.
5. Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti.
Namna ya kuandaa
1. Changanya malighafi hizo kwa pamoja.
2. Saga hadi zilainike.
3. Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati.
4. Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au
kutengenezea tambi.
5. Anika kwenye jua la wastani.
6. Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande
vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha.
7. Tumia lishe hiyo
kwa samaki mara tatu kwa siku.
JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI
Reviewed by BENSON
on
July 28, 2017
Rating:
ASANTE SANA
ReplyDeleteChakula hakizami?
ReplyDeletejamani hiyo mashine naweza pata wapi
ReplyDeleteHiyo mashine inapatikana wapi?
ReplyDelete