MFAHAMU MDUDU HUYU MHALIBIFU KWA MAHARAGE
Funza
wa vitumba ni nondo, na ni mdudu mharibifu maarufu wa kunde na maharage
mengine kote Afrika Mashariki na Magharibi. Viwavi hula vitumba na
maua, na kuingia ndani ya mifuko ya maharage na kuacha tundu kwenye
mfuko wa maharage na kula mbegu.
Je huyu mdudu yukoje?
Nondo
aliyekomaa hutaga mayai moja moja au katika makundi madogo juu ya maua
au vikonyo vya maua na pia kwenye vichomozo vya mimea michanga. Mayai
yana umbo la mduara dufu, rangi nyeupe na manjano nyepesi; yai moja
linaonekana kama tone dogo la maji. Larvae, au viwavi, vinaweza kukua na
kufikia urefu wa milimita 17-20.
Viwavi
huwa rangi ya kijani chepesi na madoa ya kahawia-meusi na kichwa ni
rangi ya kahawia iliyokolea. Viwavi wachanga hupatikana katika makundi
wanapokuwa katika hatua hii, lakini baadaye kupatikana kila mmoja
kivyake. Viwavi wachanga hushambulia maua na majani, lakini viwavi
waliozeeka wana uwezo zaidi wa kutembea na mara nyingi wanapatikana
wakila na kutoboa na kuingia ndani ya mfuko wa mbegu ambapo hula mbegu
zinazokua. Vinapokomaa viwavi huanguka kutoka kwa mmea mpaka mchangani
ambapo hubadilika na kuwa pupa wakiwa chini ya takataka.
Kiwavi wa nondo akiwa ndani ya jumba la maharage (podo) |
Mbawa
za nondo ni nyeusi-kahawia na zina alama nyeupe juu ya mbawa za mbele
na upana wa mbawa wa milimita 20-25. Nondo huchangamka usiku. Wakati wa
mchana hupatikana wakipumzika upande wa chini wa majani na mbawa zao
zikiwa zimetandazwa.
Kuna
hatua nne katika mzunguko wa maisha: mayai, viwavi, pupae na nondo
aliyekomaa. Kukua kwa mayai huchukua wastani wa siku 3, hatua ya viwavi
huchukua wastani wa siku 13-14, hatua ya pupae siku 6-7 na nondo
waliokomaa wanaweza kuishi kwa wastani wa siku 6-10.
Maharage yanashambuliwa yakiwa katika hatua gani?
Maharage
hushambuliwa na funza wa vitumba kuanzia wakati wa kutoa vitumba mpaka
wakati wa kuvuna. Angalia matundu ya mviringo kwenye maua na pia majani
yaliyokunjwa ambayo yamekwama pamoja. Fungua maua na uangalie viwavi.
Mifuko ya mbegu itakuwa na tundu la wazi ambalo kiwavi aliingilia.
Angalia mipira ya manjanokahawia nje ya mifuko ya mbegu; hiki ndicho
kinyesi kilichoachwa na viwavi walipoingia ndani ya mfuko wa mbegu.
Athari ya funza wa vitumba kwenye mapodo ya kunde |
Njia Za Kudhibiti Funza Wa Vitumba
Kinga – mambo ya kufanya kabla dalili kuonekana
Mbinu za kitamaduni:
- Panda mapema ili kuepuka kipindi cha ushambulizi mzito.
- Tumia aina sugu / zakuhimili na /au za kukomaa mapema ikiwa zinapatikana katika eneo lako.
- Ondoa mimea mingine wenyeji kama vile maharage ya kawaida, kudzu, maharage ya lima, pojo na mimea mingine ya mikunde kutoka ndani na nje ya shamba.
- Kupanda mseto maharage na mtama au mahindi kunapunguza idadi ya wadudu wakutoboa mifuko ya mbegu na kupunguza hasara ya mavuno.
- Fanya mzunguko wa maharage na mahindi.
Kudhibiti – mambo ya kufanya baada ya dalili kuonekana
Mbinu za kitamaduni:
- Okota kwa mkono mayai na viwavi kutoka kwa mimea na uviharibu.
- Kata majani yaliyofungwa fungwa pamoja yenye nyuzi nyeupe za hariri na pia uondoe majani yaliyozeeka ili kuruhusu mwanga zaidi kufikia majani na mashina ya mimea.
Mbinu za kikemikali:
- Ni vigumu kudhibiti funza wa vitumba na dawa za kuua wadudu kwa sababu hubaki wamejificha ndani ya mfuko wa mbegu / maharage.
- Dawa ambazo unaweza kutumia kuua hawa wadudu ni pamoja na Thiodan, dusban, serecron and Karate
MFAHAMU MDUDU HUYU MHALIBIFU KWA MAHARAGE
Reviewed by BENSON
on
February 22, 2018
Rating:
No comments