NJIA ZA UTUNZAJI WA KUKU WANAOTAGA MAYAI.
Kwa kawaida kuku huanza kutetea (Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha
miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri
wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji
anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na
kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku
aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa
yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga
ndani ya chombo hicho.
Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza
kutagwa.
UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea
vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa
wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza
kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili
KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai
yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia
yawe na sifa zifuatazo
·
Yasiwe na uchafu yawe masafi
·
Yasiwe na nyufa
·
Yatokane na kuku aliyepandwa na
jogoo
·
Yasiwe madogo wala makubwa bali
yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
·
Yasiwe mviringo kama mpira pia
yasiwe na ncha kali sana.
·
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya
wiki mbili toka yalipotagwa
·
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye
sehemu yenye joto.
KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri
yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini
kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa
wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii
husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
·
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani
ya kiota
·
Pia mnyunyuzie dawa kuku
anayetarajia kuatamia
·
Weka mayai kwenye kiota huku mikono
yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza
kuyasusa.
·
Ni vizuri kuifanya kazi hii ya
kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa
kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.
PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI.
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia
na kutotoa pamoja.
Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho
kutaga.
Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na
kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee
mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa
hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga
watoke.
UTEKELEZAJI WAKE.
Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku
anayotaga.
Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku
ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.
Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza
kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai
ya ukweli wakati wa usiku.
MUHIMU.
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za
mafuta ya taa, manukato n.k.
JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA
MBEGU NA YALE YASIYO NA MBEGU.
Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku
ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box
lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba
chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa
chakula cha familia au kuyauza.
NJIA ZA UTUNZAJI WA KUKU WANAOTAGA MAYAI.
Reviewed by BENSON
on
January 03, 2018
Rating:
No comments