KILIMO BORA CHA DENGU
Dengu ni nafaka kama zilivyo nafaka zingine, ni zao la jamii
ya mikunde pia ni zao la biashara, ni miogoni Mwa zao muhimu sana la biashara
ukanda wa ziwa kwa sababu ya thamani yake Kuwa juu sana, zao hili hutumika pia
kama zao la chakula kama mbonga , mchaganyo wa wali mseto , makande ,
kutegeneza Bagia , chiichiri namengineyo mengi.
Kanda ya ziwa hili ndiyo Zao llinalotegenewa zaidi likiogozwa
na zao la choroko kwa kuwa na thamani kubwa, hivyo zao hili nizao muhimu kwa
uchumi wa wanakanda ya ziwa.
Dengu ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha
protini, vitamini A na B, Madini ya Potassium na chuma. Zao hili likilimwa
vizuri linaweza kutoa mavuno ya kilogram 200 hadi 500 kwa ekari. Zao hili
huchukua wastani wa siku135 kupandwa hadi kuvunwa.
HATUA MUHIMU KATIKA KILIMO CHAKE
Kilimo cha ndegu ni kilimo rahisi sana hakina usubufu sana
kama yalivyo mazao mengine hasa ukifata utaratibu wa hatua za mwanzo.
Mambo ya kuzingatia
1. Kuwa makini na hali ya hewa ya mwaka husika kwa kuangalia
ukame katika mbuga utaaisha lini pia hali ya mvua ikoje kwa maana kuwa msimu wa
kulima huwa mwezi wa tatu mwishoni kwenye maeneo ambayo mbuga huwahi kukauka
mapema yaani muda huo ndiyo watu huanza kuandaa shamba kwa kulilima mara ya
kwanza kama hatua ya kukiandaa shamba pia hatua hii hufanyika mwenzi nne lakini
iwe kwenye kumbukumbu sahihi kuwa ndegu kwa hali ya uzuri kabisa hulimwa mwezi
nne na mwanzoni kabisa mwa mwezi wa tano kabla mbuga hazichakauka .
2. Uchaguzi wa Mbengu,
mbengu bora za dengu ni muhimu kuzifahamu na kuzitumia katika kilimo hiki
Ziko mbengu ambazo hazihimili magonjwa lakini zipo zinazohimili magonjwa na
zinakuwa na uzito hii husaidia katika swala la uuzaji kwa maana ya kuwa mara
nyungi dengu kwa sasa huuzwa kwa kilo ili mkulima apate faida zaidi
3. Baada ya kulima mara ya kwanza kama kuliandaa shamba
unapaswa kulima mara ya pili na kupanda mbengu kwa kufata misitari au kufata
tumba au vitalu au misingi itakayokuwa imeadaliwa.
4. Hakikisha dengu unapanda katika mbunga isiyo na maji
yaliyotuama , unyevunyevu wa udogo wa shambani ndiyo hitaji muhimu la
uoteshaji dengu hairuhusiwi kabisa kupanda dengu kwenye shamba lenye maji.
5. Ardhi inayofaa kwenye kilimo cha dengu ni shamba nyeusi au
udongo mweusi ambao hutumika pia katika kilimo cha mpunga, mahidi, choroko na
mengineyo .
6. Baada ya dengu kuota hakijisha hakuna maji yaliyotwama
katika shamba lako
7. katika ulimaji wa dengu palizi haina ulazima mara nyingi
dengu haina palizi kabisa ukizigatia hatua za mwanzo za uandaaji wa shamba
8. Dengu hutumia miezi mitatu mpaka kuvuna hivyo inajulazimu
kusubiri ikauke mpaka hali ujano itokee kwenye mmea, mavuno ya dengu mara zato
hufanyika kwa kung’oa mmea wote na kukusanya sample dogodogo ili kumaliza
mapema mavuno yake baada ya hatua hiyo unaleta mkokoteni shambani unajusanya
kwa mkokoteni nakupeleka sehemu kavu iliyosafi kwa ajili ya kutoa maganda ya
zao la dengu,hatua ya kutoa maganda ya dengu inaweza fanyika kwa kienyeji kwa
kupiga na miti au ikatumika kwa kitaalamu kwa kupiga .
na Tractor yaan tractor inapita kwa mzuguko kwenye navuno ya
dengu yaliyosambazwa mpaka kuputua maganda ya juu ya dengu na kubaki dengu
yenyewe tayari kwa biashara au kukoborewa tena kwa chakula.
9. Uhifadhi wa zao la dengu hauna chagamoto sana japo
hushambuliwa na wadudu baada ya miezi mitatu bila kuweka dawa unapaswa
kuhifadhi kwenye eneo la wazi yaan kama ni chumba kiwe na uwazi wa hewa ya
kutosha lakini pia kunagunia special nitazieleza kwenye utatuzi wa
chagamoto.
CHAGAMOTO KATIKA KILIMO CHA DENGU
Zipo chagamoto kadhaa katika kilimo cha dengu kama ifatavyo
1. Wakati wa kupanda huwa kunachagamoto ya mvua ambazo
hujitokeza na kuharibu zao la dengu kwa kisukuma tunaita SHIBOJA yaani mvua za
kuozesha dengu chagamoto hiyo ikijitokeza subiri maji yakauke katia mbengu upya
kama zao limeathiriwa kidogo kama limeathiriwa sana unarudia shamba lote.
2 Chagamoto ya Funza baada ya mmea kutoa maua . mmea ukitoa
maua funza hushambulia kwa kasi kama eneo hilo liko na funza tiba ya funza hao
nikupulizia dawa unaenda duka la kilimo watakupatia.
3 chagamoto ya wadudu wakati wakati mmea unatoa zao lenyewe
Wakati huu pia unapulizizia dawa kama wakijitokeza Jambo la funza na wadudu
hujitokeza mara chache sana hivyo ni vyema kuwa na.tahadhali hiyo.
4 Chagamoto ya panya Panya hujitokeza kwenye shamba wakati
zao Linaanza kukomaa wao hutafuna dengu kamili hivyo unaweza jikuta unapata
hasara wakati dengu zilisitawi vyema, Utatuzi wa chagamoto hiyo ni kuwatega panya kwa sumu kwa ukanda wa mkoa
wa shinyanga serikali hutoa dawa nasi huchaganya na mahidi nakusambaza pembezoni
mwa shamba maana panya hutokea kwenye nyasi hivyo watakutana na mahidi nakuyala.
Chagamoto nyingine ni za masika unaweza lima mwishoni sana
kwenye mavuno ukakutana na mvua.
5 Chagamoto ya uhifadh Hapo kunachagamoto ya kushambuliwa na
wadudu ndani ya miezi mitatu ya mwanzo unashauriwa kuhifadhi kwenye magunia
nasiyo mifuko ya plastic.
Unashauriwa kutia dawa inaitwa AKTERIA mapema kabisa
unapohifadhi kama unahifadhi kwa muda mrefu baada ya miezi mitatu unatia tena
Au unaweza hifadhi kwaifuko maalumu ambayo imetiwa dawa kabisa na dani inajuwa
kama mfuko wa sukari na upaswa kuifuga kitaalamu kama maeelekezo yalivyo .
Chagamoto nyingine ni ya soko naieleza hapa chini na utatuzi
wake
HALI YA HEWA NA
UDONGO
Ni zao linalohitaji hali ya hewa ya kibaridi kiasi kwani joto
kali na ukame sana huathiri mavuno yake, hupunguza wingi wa mavuno. Ni zao
linalostahimili ukame, linaweza kukua katika hali ya hewa ya unyevunyevu tu.
Kama utakuwa unamwagilia basi epusha unyevu mwingi ikifikia
kipindi cha maua hadi kuvuna. Zao hili linaweza kulimwa katika udongo wa aina
tofauti tofauti wenye Ph 6-8. Udongo wenye asidi na base kidogo.
Kwa Tanzania zao hili linaweza kulimwa katika mikoa ya
Iringa, Dodoma, Mwanza, Singida, Morogoro, Shinyanga N.K. Lakini kwa sasa mikoa
yaShinyanga na Mwanza ndio wazalishaji wakubwa wa Dengu.
UPANDAJI NA NAFASI
Zao hili huitaji mbegu kiasi cha kilogram15 hadi 40
kutegemea ukubwa wa mbegu husika. Zao hili hupandwa mwishoni mwa msimu wa
mvua,unaweza kupanda baada ya kuvuna mazao mengine uliyopanda mapema.
Mbegu za dengu hufukiwa katika kina cha sentimeta 5 hadi 6
ili kufanya mazingira rafiki kwa bacteria wa rhizobia kufanya kazi. Zao hili
usipande pamoja na vitunguu na tangawizi. Panda kwa kutumia drilling
method-njia ya vifereji kwa nafasi ya mistari miwili ya sentimeta 15 na
sentimeta 30 hadi 50 kwa mstari hadi mstari.
MBOLEA ZA VIWANDANI NA SAMADI
Mbegu unaweza
kuzipanda baada ya kuziongeza inoculam kundi F na Pia Mbolea ya DAP kilogram 25
hadi 50 kwa ekari katika shamba lisilo na rutuba ya kutosha.
PALIZI-Palilia mapema shamba lako.
WADUDU WAHARIBIFU
KWA DENGU
Dengu hushambuliwa na Mchwa wakubwa weusi, aphid wa njegere,
funza wa vitumba, Inzi wa lucina n.k. wazuie wadudu hawa kwa kupuliza dawa za
wadudu mara tu uonapo dalili za mashambulizi ya wadudu.
MAGONJWA YA DENGU
Dengu hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu ambayo. Hivyo
kama eneo lako hushambuliwa na ukungu mara kwa mara basi puliza dawa za ukungu
(FUNGICIDES ).
UVUNAJI WA DENGU
Zinavunwa mara tuu pindi vitumba vya chini vibadilikapo rangi
kuwa kahawia angavu na vitumba vikiguswa hutoa sauti Mavuno ya dengu kwa heka
yanaweza kuwa gunia 6,5,4 Inategemeana na eneo ulilolima linarutuba kiasi ngani
na umefata taratibu zote.
Soko la dengu ni la uhakika sana kwa maana ya uhitaji wa
dengu katika soko la ndani na nje
Dengu ndiyo zao ambalo mkulima wa mkoa wa shinyanga na niko
jirani hulitegemea kwa kipato cha juu.
KILIMO BORA CHA DENGU
Reviewed by BENSON
on
January 11, 2018
Rating:
Natafuta soko la dengu,unaweza kunisaidia?
ReplyDelete0768491304
Samahani naomba kuulizia kwamba Kwa hekari Moja unapolima dengu inagharimu kiasu Gani cha pesa?
ReplyDeleteSamahani naomba kuulizia kwamba Kwa hekari Moja unapolima dengu inagharimu kiasi Gani cha pesa?
ReplyDeleteSamahani naomba kuulizia mbegu za dengu zina bei gani na unaweza kutumia kiasi gani kupanda kwa hekari moja?
ReplyDeleteNi lazima udongo uwe mweus
ReplyDeleteMbegu za dengu zinapatikana kwenye maduka ya pembejeo? Au unanunua tu zilizopo sokoni?
ReplyDelete