UFUGAJI BORA WA NG'OMBE WA MAZIWA

Related image
Ndugu msomaji leo nitakuonyesha vitu vya muhimu vya kuzingatia pale unapo taka kuanza kufuga ng'ombe wa maziwa , 

 UTANGULIZI
ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ni moja kati ya ufugaji unao wakomboa wafugaji wengi sana endapo watazingatia kanuni za ufugaji bora
mimi mwenyewe nimekua shahidi nikiona watu wengi wana piga hatua kutokana na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa

 vifuatavyo ni vitu vya kuzingatia sana wakati unataka kuanza na hata kama umeanza kufuga ng'ombe wa maziwa

uchaguzi wa aina bora ya ng'ombe

hili ni jambo la msingi sana kabla ya kuanza kufuga unatakiwa ujue je ni aina gani ya ng'ombe bora ambaye anaweza kunifaa .
mwanzoni niliandika aina za ng,ombe wa maziwa hivyo sitopenda kurudia sana kuanza kuelezea aina za ng,ombe wa maziwa  nitaelezea kwa ufupi tu ukitaka kujua aina hizo kwa undani unaweza tafuta kwenye blog hii hii kwa kuandika AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA.

lakini kwa ufupi kuna aina tano kubwa ambazo zinatumika sana

·         fresian
·         guersey
·         jersey
·         ayrshire
·         brown swiss 
hivyo unaweza fanya uchaguzi wako kulingana na mahitaji yako kwa kua kila aina inasifa tofauti na nyezake japo kua fresian ndio aina inayopendwa sana na ndio aina ambayo inatoa maziwa mengi sana kuliko aina zingine zilizo bakia.

                                              

baada ya kukuonyesha aina chache  tunaenda kwenye eneo lingine la m muhimu

UJENZI WA BANDA
Wafugaji wengi hua wamezoe kufuga ng'ombe kienyeji ndo maana wanakua hawapati kulingana na jinsi walivyo tarajia 

banda ni lazima liwe bora ili kuongeza uzalishaji

·         banda unaweza kuweka  zege chini ili kuwezesha usafi na pia hii inapunguza magonjwa mengi kama vile kuoza kwa kwato
·         pia banda la ng'ombe wa maziwa unatakiwa kuweka paa juu ili kuzuia mvua na jua kufukia moja kwa moja kwa ng,ombe na hii pia inapunguza maamukizi ya magonjwa pamoja na stress kwa ng,ombe
·          lazima banda bora liwe na mifereji ambayo itasaidia kutoa uchafu nje ya banda wakati wa kusafisha hii itasaidia kuounguza uchafu ndani ya banda.
·         madilisha pia yanatakiwa kua makubwa kuwezesha hewa na mwanga wa kutosha kuingia ndani ya banda.
·         sehemu ya kulia chakula na pamoja na sehem ya kunywea maji ni lazima ziwepo
·         kitu kingine lazima sehemu ya kukamulia iwepo ili iwe rahisi wakati wa kukamua maziwa 
·         napia ndama lazima walazwe sehemu tofauti na ng'ombe wakubwa.

      CHAKULA
Ili ng'ombe aweze kutoa maziwa ya kutosha ni lazima apewe maji safi na chakula bora na pia lazima  chakula kiwe cha kutosha
kabla ya kuanza kufuga lazima ujiahakikishie chakula cha kutosha na chakukidhi mwanzo hadi mwisho.


·         watu wenye eneo hua wanapanda majani ili kuahikisha chakula hakikosekani(pasture)
·         napia unaweza kukata majani wakati wa masika na kuyatunza vizuri ili kuwalisha wakati wa kiangazi pale malisho yanapokua ya shida.
·         pia ng'ombe wa maziwa ni lazima apewe chakula maalumu ambacho kinaongeza maziwa kila siku na hua wanapewa kili 1 hadi 3 kulingana na uzito wake asubuhi na jion
·         na pia unaweza kumlisha mapumba au mashudu mabaki ya mazao kama viazi mahindi pia pale majani yanapo kua shida.
MUHIMU
natumaini umejifunza kitu kutoka mwanzo mpaka hapa tulipo fikia, japo kua ufugaji wa ng'ombe sio mgumu sana lakini kunavitu muhimu ambavyo nilazima wewe kama mfugaji uvizingatie ili kuongeza uzalishaji


·         ng'ombe ni lazima waoshwe kwa dawa ili kupunguza kushambuliwa na wadudu ambao wanaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa kama ECF, na unaweza kuwaosha ng'ombe kila wiki kutokana na ratiba yako pia unaweza kutumia dawa kama TICK FIX, PARANEX  na zingine nyingi
·         lazima banda liwe safi ili kuzuia maambukizi ya magonjwa kama FOOT ROUT  na usafi unaweza kufanyika kila siku asubuhi au jion.
·         ng'ombe lazima apewe chakula na maji safi  ili kuongeza uzalishaji
·          pia ni lazima kuwatibu au kuchukua hatua pale ng'ombe anapoonekana kua na ugonjwa ili kuepusha maambukizi kwa wengine na pia ili kumuokoa.

UFUGAJI BORA WA NG'OMBE WA MAZIWA UFUGAJI BORA WA NG'OMBE WA MAZIWA   Reviewed by BENSON on December 19, 2017 Rating: 5

No comments