KILIMO BORA CHA MAKAKARA (PASSION FRUITS)
Ni mimea inyotambaa na kuhimili
hali nyingi za hewa (sio ukame). Mmea huu hustawi zaidi ukanda usio na baridi
wastani wa 20c – 30c na kiasi cha mvua 1500mm za ujazo kwa Mwaka, tunda huwa na
ukubwa wa sentimeta 10 kwa kipenyo na uzito gramu 90.
kuna aina kadhaa za matunda haya
lakini yale ya kijani/manjano hustawi zaidi ukanda wa pwani na yale yenye
wekundu fulani hustawi zaidi maeneo ya misitu, hupendelea udongo wa kichanga
wenye mbolea na usiotuamisha maji, pia udongo usiwe na chumvi nyingi na pia
kusiwe na mwamba chini kasi cha mita moja tu.
Upandaji.
Mbegu zipandwe kwanza kwenye mifuko ya plastiki yenye udongo wenye rutuba ya
kutosha , kiasi cha Mbegu 3 kwa kila mfuko na mara zinapoota mimea ikingwe na
jua kali na ikifikia urefu wa sentimeta 30, huweza kuhamishiwa shambani
Kwenye shamba lako hakikisha kuna nguzo zenye waya mmoja kwa ajili ya mimea
kutambaa juu yake, sehemu ya juu baada ya nguzo kuzikwa chini ibakie kama mita
mbili na kati ya msatari na mstari iwe ni mita 2 (ukanda wa pwani ) na mita 3
ukanda wa juu kiasi, na umbali kati ya nguzo na nguzo kwenye mstari ni mita 6,
na mimea ipandwe umbali wa mita 3 kati ya nguzo na nguzo kufuata mstari.
Mbolea
Mbolea za viwandani ziwekwe kutokana na hali ya udongo, muone afisa ugani
kilimo ili afanye vipimo kujua mahitaji na upungufu wa udongo,
Magonjwa na madudu.
Wadudu kama chawa wa mimea na mchwa wekundu ndio adui wa makakara, pia fangasi
husshambulia sana maua ya makakara. Dawa za jamii ya kopa zitumike mara dalili
za magonjwa au wadudu kuonekana, kiasi cha kilo 2.8 – 3 hutosha kwa hekta moja
au gramu 225 kwa ajili ya dumu moja la lita 20
Magugu.
Makakara yanatakiwa yawe kwenye shamba safi lisilo na majani na magugu, jembe
la Mkono au madawa kama ROUND-UP na GRAMOXONE ynaweza kutumika mimea
ikishaefuka na kuwa juu kwenye waya
Kufundisha matawi ya mimea.
Ni lazima kuyafundisha matawi mawili ya kwanza kwa kuyaelekeza kutambaa kwenye
waya kila moja likielekea upande wake na matawi yatakayoota kutokana na matawi
makuu nayo yaelekezwe juu kwenye waya yakifikia ukubwa wa sentimeta 30 – 40.
Kupunguza matawi.
Silazima kupunguza matawi kwa sababu mmea mkubwa zaidi ndio hutoa matunda mengi
zaidi, labda kama kuna matatizo katika uchumaji ndio unaweza kupunguza baadhi
ya matawi kiasi.
Uvunaji.
Uvunaji huanza baada ya miezi 8 – 9 baada yam mea kupandwa na matunda
hukusanywa baada ya kudondoka yenyewe chini baada ya kuiva kila baada ya wiki
moja, matunda yahifadhiwe sehemu kavu na isiyo na joto , kiasi cha tani 5 – 10
huweza kupatikana katika hakta moja kwa msimu
KILIMO BORA CHA MAKAKARA (PASSION FRUITS)
Reviewed by BENSON
on
December 20, 2017
Rating:
No comments