MBINU ZA KUZUIA WADUDU, NDEGE NA WANAYAMA WAHARIBU WA MAZAO
Wadudu
Wadudu wanaoweza kushambulia mazao ni pamoja na katapila
na jongoo.
Katapila
Hukata ncha ya mmea inayokua
Kudhibiti
Kagua shamba mara kwa mara ili kutambua kuwepo kwa wadudu
hao na kuwaua.
Jongoo
Hukwangua shina na kuacha michubuko
Kudhibiti
Kagua shamba mara kwa mara na kuwaua.
Kuku
Huharibu mmea kwa kuparura juu ya ardhi na kusababisha kujeruhi na kukata
mizizi. Uharibifu huu husababisha mmea kuwa katika mazingira rahisi ya
kushambuliwa na vimelea kama Fusarium batatis ambao huozesha mizizi ya mmea.
Kudhibiti
Zuia kuku wasiingie shambani.
Konokono
Husababisha uharibifu zaidi kipindi cha mvua. Wanapotambaa
kwenye mmea huacha utando, hasa katika sehemu inayochipua na kusababisha mmea
kudumaa.
Kudhibiti
Kagua shamba mara kwa mara na kuwaondoa.
Weka mchanganyiko wa mbolea ya samadi na majivu kuzunguka
shina la mmea ili kuzuia wasiweze kupanda juu ya mimea.
ANGALIZO: Ni muhimu kupulizia / kunyunyizia dawa uharibifu ukiwa mkubwa
sana. Tembelea maduka ya Kilimo kwa aJili ya Ushauri Zaidi na kununua Dawa.
MBINU ZA KUZUIA WADUDU, NDEGE NA WANAYAMA WAHARIBU WA MAZAO
Reviewed by BENSON
on
December 06, 2017
Rating:
No comments