FAHAMU UGONJWA WA HOMA YA MATUMBO KATIKA KUKU (Fowl Typhoid)
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria na
huwapata kuku wa umri wote. Mara nyingi ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa kuku
wagonjwa kwenda kwa kuku wasio wagonjwa kupitia kwenye mayai , chakula chenye
kinyesi cha kuku wenye ugonjwa pia watu iwapo watabeba vimelea na kuja navyo
kwenye banda.
Jinsi unavyoambukiza:
i)
Kuku asiye mgonjwa kula vimelea vya ugonjwa kupitia kinyesi cha kuku mgonjwa
kwenye chakula.
ii) Kuku mgonjwa huweza kurithisha vifaranga
wake kupitia mayai yaliyotagwa.
iii) Watu na vyombo vya usafiri wanaweza
kuhamisha ugonjwa kutoka sehem hadi sehemu.
iv) Vyakula vya kuku kutoka sehemu yenye
ugonjwa kwenda kusiko na ugonjwa.
v) Mizoga ya kuku yenye ugonjwa ikipelekwa
sehem isiyo na ugonjwa.
Dalili
a) Homa Kali
b) Manyoya husimama
c) Kinyesi kuonekana kuganda sehem za nyuma.
d) Kukosa hamu ya kula.
f) Kuku kudhoofika.
g) Kiwango cha utagaji hushuka.
Kinga:
Tenganisha
vifaranga na kuku wakubwa.Kuku wagonjwa watengwe na kupewa tiba ya
antibiotic.Zingatia usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji.
Matibabu:
Dawa
aina ya Oxytetracycline(OTC)au Salfa ambayo huchanganywa kwenye maji na kupewa
kuku kwa siku 5 hadi 7.
Nipigie 0752153342
FAHAMU UGONJWA WA HOMA YA MATUMBO KATIKA KUKU (Fowl Typhoid)
Reviewed by BENSON
on
November 14, 2017
Rating:
No comments