UFAHAMU UGONJWA WA MDONDO/KIDERI (NEWCASTLE DISEASE)

Ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege ambao unasababishwa na vimelea aina ya paramyxovirus.

Kuenea kwa Ugonjwa
Ugonjwa wa Mdondo (Newcastle disease) huenea kupitia njia mbalimbali kama zifuatazo:-

  • Mayai ya kuku aliyeugua ugonjwa wa mdondo/kideri (Newcastle disease).
  • Kugusana na kuku mgonjwa.
  • Kupitia maji yenye maambukizi.
  • Wakati wa totoleshaji vifaranga.
  • Chakula chenye maambukizi.
  • Hewa yenye maambukizi ya ugonjwa huu.



Dalili za Mdondo/Kideri (Newcastle disease)

  1. Vifo vya ghafla.
2. Kutoa udenda mdomoni.
3. Kukosa hamu ya kula.
4. Kuharisha kinyesi cheupe na kijani.
5. Kuhema kwa shida.
6. Kukakamaa viungo au kupooza hasa mabawa, shingo na miguu.


7. Kupunguza utagaji.
8. Vifo hutegemea kasi ya ugonjwa huweza kufikia hadi asilimia mia moja (100%).


Namna ya kudhibiti Mdondo/Kideri (Newcastle disease)


  1. Wapewe chanjo kwa muda unaofaa (Siku ya 7 na 28, na kila baada ya miezi 3).
  2. Kuku wote waliozidiwa (wagonjwa) wachinjwe na wafukiwe katika shimo lenye kina kirefu kuzuia kuenea ugonjwa.
  3. Fuata maelekezo ya Daktari au Mtaalam wa mifugo.
  4. Matibabu
  5. Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila kwa msaada na ushauri zaidi katika ufugaji wasiliana na Daktari au Mtaalam wa mifugo.
UFAHAMU UGONJWA WA MDONDO/KIDERI (NEWCASTLE DISEASE) UFAHAMU UGONJWA WA MDONDO/KIDERI (NEWCASTLE DISEASE) Reviewed by BENSON on November 30, 2017 Rating: 5

No comments