UFAHAMU UGONJWA WA KIPINDUPINDU CHA KUKU (FOWL CHOLERA) NA TIBA ZAKE.
Ni
ugonjwa unaosababishwa na bacteria ambao unaoshambulia karibu aina zote za
ndege, ugonjwa huu ni hatari ambapo vifo ni kati ya 30% hadi 80%.
Njia
za ueneaji ugonjwa
- Utupaji ovyo wa mizoga ya kuku, kwani mzoga unaweza kukaa na vimelea kwa zaidi ya miezi mitatu.
- Kupitia
chakula na maji yenye mchanchanyiko na vimelea hivyo.
- Kuku
mzima kugusana na kuku mgonjwa.
- Kupitia
njia ya upumuaji.
Dalili
za Fowl Cholera
- Huarisha majimaji ya kijani yenye harufu.
- Kilemba na masikio ya kuku hupauka na kulegea.
- Hupumua kwa shida.
- Hutokwa na ute mdomoni na puani.
- Joto la mwili hupanda.
- Vifo
hutokea
Jinsi
ya Kudhibiti Fowl Cholera
- Usafi
wa ndani na nje ya banda.
- Tenganisha
kuku kwa rika zao (wakubwa kwa wakubwa na wadogo kwa wadogo).
- Zingatia
sifa za banda bora.
- Mizoga
ichomwe moto au ifukiwe katika shimo la kina kirefu kuzuia kuenea kwa
ugongwa.
Tiba
ya Fowl Cholera
Ukiona
dalili za ugonjwa huu wahi mapema kutumia dawa mojawapo kati ya zifuatazo:~
- Trimazin
- Typhoprim
- Sulphonamides
- Hipraloma
- O.T.C
- C.T.C
- Ganadex
UFAHAMU UGONJWA WA KIPINDUPINDU CHA KUKU (FOWL CHOLERA) NA TIBA ZAKE.
Reviewed by BENSON
on
December 01, 2017
Rating:
No comments