UFAHAMU UGONJWA MWINGINE AMBAO UNASUMBUA VIFANGA UNAITWA (CHICK PASTING).
Katika malezi ya vifaranga kumekuwa na tatizo
sugu ambalo kwa bahati mbaya wafugaji wengi hawalijuhi na limekuwa likiwatesa
sana. Vifaranga wadogo walio chini ya umri wa wiki moja wamekuwa na tatzo la
kugandia kinyesi nje ya njia zao za haja yaani kwenye kale katundu kakutolea
kinyesi. Wakati mwingine huziba njia ya choo na kumsababishia kifo kifaranga
lakini hata asipokufa hukosa raha na mwishowe na ukuaji usiokuwa mzuri.
Kwa uzoefu wangu nimegundua kuwa zaidi 50% ya
vifaranga wanaopata tatizo hilo ufa kama wasipopata huduma inayostahili. Mara
nyingi unaweza kushangaa vifaranga wako wanakosa raha, wanakufa, nk. Lakini
ukimchunguza vizur utamkuta na uchafu kwenye njia zake za kutolea haja kubwa na
pengine pameziba kabsa.
Tatzo hili husababishwa na kuwapa chakula kingi
vifaranga na kuwapa maji kidogo au usipate kabisa.Kifaranga anapozaliwa kama kiumbe mwingine huwa
hajawa imala katka maumbo yake ya mfumo
wake wa mmeng'enyo hivyo unapompa chakula bila maji ya kutosha ni kwamba hata
upataji wake wa choo itakuwa wa tabu.
Kuepuka hili tatzo unapaswa kuanzia siku moja
hadi 5 kuhakikisha vifaranga wako wanapata maji mengi na chakula cha wastani
ili kumuwezesha njia zake za mmengenyo kukaa sawa na kutoathirika na vitu
vikavu na vigumu. Ili kuliwezesha hili kuepukana na kadhia hiyo. Pia natoa
angalizo na fundisho kuwa, vifaranga wadogo hawawezi kujishughurisha sana kutafuta
chakula na maji yalipo badala yake kinachokuwa mbele yake anakula na kama
hakuna kitu basi sasa akikuta chakula bila maji tatzo linaanzia hapo.
Jinsi ya kuwahudumia walioathirika ni
kuwasafisha kwa kutumia maji ya uvuguvugu au kitu chochote mithiri yake ili
kuhakikisha unaondoa uchafu bila ya kumuumiza na njia yake ya haja ibaki
safi.Wakati huo huo inapendekezwa ukiwa unampatia Antibacterial ili kumuepusha
na madhara zaidi ya hayo na pia inashauriwa kuwa unampaka mafuta ya mgando
asili ya jelly kwa ajili ya kumlainisha njia yake ya haja ili asiumie zaidi.
UFAHAMU UGONJWA MWINGINE AMBAO UNASUMBUA VIFANGA UNAITWA (CHICK PASTING).
Reviewed by BENSON
on
November 15, 2017
Rating:
Je mbali nahii blog mnayo application naka mnayo inaitwaje? Hiliniweze kui download.
ReplyDelete