TOFAUTI ZA MUONEKANO KATI YA KUKU MWENYE AFYA NA KUKU MGONJWA
Wakati mwingine unaweza ukawa ni mfugaji wa kuku lakini
usitambue yupi ni kuku mwenye afya bora na yupi ni kuku dhaifu hivyo katika Makala
yetu ya leo nitaeleza sifa na muonekano wa kuku dhaifu na kuku mwenye afya.
KUKU MWENYE AFYA NZURI
1. Macho yenye uangavu
2. Hupenda kula na kunywa maji
3. Pua zilizo safi, upanga na undu mwekundu, manyoya
4. laini na yaliyopangika vizuri
4. Hupumua kwa utulivu
5. Sehemu ya kutolea haja huwa kavu
6. Kinyesi kikavu, cheupe na kisicho na rangi
7. Hutaga mayai kawaida
KUKU ASIYE NA AFYA NZURI
1. Huonekana mchovu na dhaifu
2. Hula na kunywa kidogo au zaidi ya kawaida
3. Hutoa kamasi puani, ute na matongotongo; manyoya
yaliyovurugika
4. Hupumua kwa shida na kwa sauti
5. Sehemu ya kutolea haja inakuwa na unyevunyevu na
kinyesi kuganda
6. Huharisha, kinyesi huwa na damu au minyoo
7. Hutaga mayai machache au husimama kutaga kabisa
8. Huwa na tabia ya kujitenga na wenzake katika kundi
TOFAUTI ZA MUONEKANO KATI YA KUKU MWENYE AFYA NA KUKU MGONJWA
Reviewed by BENSON
on
October 28, 2017
Rating:
No comments