YAJUE MAKOSA YANAYOFANYWA NA WAFUGAJI WA SAMAKI.
Wafuga wengi wa samaki wamekuwa wakilalamika ya kwamba mambo
yamekuwa ni magumu, wakati mwingine wamekuwa wakisema ya kwamba ufagaji wa
samaki hauna faida, ila ninachotaka kukwambia ni kwamba samaki wanafaida lukuki
endapo utafuga katika misingi kamili ya kufuga samaki.
Baadhi ya makosa yanayofanywa
nawafugaji wa samaki ni kama ifuatavyo;
1. Maandalizi yasiyo rasmi katika
bwabwa la samaki.
Hili ni moja ya mapungufu au ni kosa kubwa katika shughuli
ya ufugaji samaki ambao wafugaji wengi huyafanya, mfano Mzee Kuota ni mfugaji
wa samaki wa samaki wa muda mrefu sana,lakini kawaida yake kila anapo maliza
kuvuna samaki katika bwawa lake huyaacha yale maji ndani ya bwawa mpaka pale
inapokaribia muda mwingine wa kupanda mbegu ndio hutoa maji na kuweka mengine
na kuanza kupandikiza mbegu.
Madhara yake.
Endapo maji uliyomaliza kuvulia samaki wako hukuyatoa kwa wakati ule uliomaliza
kuvua, unapelekea kuendelea kuzaliana kwa wadudu wadogo wadogo hujulikana kama
bakteria ambao ni hatarishi kwa samaki, madhara yake bakteria wanaweza
kushambulia samaki au vifaranga vya samaki kupelekea kupata magonjwa kama vile
fangasi, hivyo mfugaji huendelea kuhesabu kuwa nimepandikiza vifaranga 3000 na
anaweka mategemeo ya kuvuna 3000 au 2800 pasi kujua kwamba vile vifaranga
alivyopandikiza vilishakufa tangu wakiwa wadogo kwa kushambuliwa na wadudu,
hivyo mfugaji hukuta mategemeo aliyoyategemea kuyapata ni tofauti, hali kama
hiyo humsononesha mfugaji kwa kukata tamaa wa kuendelea na mradi pasi kujua
kama alikosea wapi katika maandalizi ya awali katika bwawa
Vile vile husababisha kuoza kwa udongo hali inayopelekea harufu mbaya na endapo
mkulima asipotoa ule udongo wa awali hupelekea ukuaji hafifu kwa samaki kutoka
kushindwa kupata hewa safi wakati wote.
2. Kutofanya matengenezo ya uhakika ya
bwawa la samaki.
Baadhi ya matengenezo muhimu ni kama vile kuhakikisha kuwa
kuta ziko imara,kutotoa udongo wa chini,kutochimba au kuongeza kina cha
bwawa .
3. Kujaza maji kabla ya kuweka dawa
ya kuuwa vijidudu katika bwawa.
Mara nyingi hushauriwa kuweka chokaa kitaalamu hujulikana
kama hydrated lime,ambayo moja kwa moja huenda kuua vijidudu vidogo vidogo
ambavyo ni hatarishi kwa samaki.
4. Kutokuturubisha bwawa kwa kutumia
mbolea.
Mbolea ambayo ni nzuri zaidi ya kurutubishwa bwawa kama
vile ya kuku,ng’ombe,au mabaki ya mifugo mingine,kutofanya hivi
unapelekea kuwa kutokuwa na chakula cha ziada kwa samaki pindi
chakula cha kutengenezwa kutokuwepo na wafugaji wengi wa samaki
baada ya mavuno hutoa maji na kujaza maji mapya bila kuweka mbolea kwa
ajili ya urutubishaji wa bwawa kusaidia kuzalishwa chakula cha asili
.
Hayo ni baadhi ya mapungufu ambayo wafugaji wengi wa
samaki huyafanya pasi na kuyafahamu hali inayowapelekea kulalama na kwa
kutopata faida kupitia mradi wa ufugaji samaki.
YAJUE MAKOSA YANAYOFANYWA NA WAFUGAJI WA SAMAKI.
Reviewed by BENSON
on
September 07, 2017
Rating:
No comments