JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI
Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za
kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa
kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo
itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.
Mahitaji
• Pumba ya mahindi sadolini 1.
• Pumba ya ngano au mpunga sadolini
1.
• Dagaa sadolini 1.
• Kilo moja ya soya.
• Robo kilo ya mashudu ya pamba au
alizeti.
Namna ya kuandaa
• Changanya malighafi hizo kwa
pamoja.
• Saga hadi zilainike.
• Kanda kama vile unga wa
kutengenezea chapati.
• Weka kwenye mashine ya kusaga nyama
au kutengenezea tambi.
• Anika kwenye jua la wastani.
• Baada ya kukauka, vunja vunja
kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia
kuwalisha.
• Tumia lishe hiyo kwa samaki mara
tatu kwa siku.
JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI
Reviewed by BENSON
on
September 08, 2017
Rating:
No comments