MBINU ZA KUTAMBUA JOGOO NA TETEA BORA KWA AJILI YA KUFUGA.
Karibu sana mpenzi msomaji wa blog hii ya
kilimo bora, nipende kuchukua wasaa huu kukushukuru sana kuwa sehemu yetu, kwa
kuwa mara kadhaa umekuwa unajifunza masomo mbalimbali kupitia blog yetu hii,
hivo niseme asante sana. Baada ya kusema hayo machache naomba twende moja kwa
moja katika somo letu la leo. Na siku ya leo tutajifunza kwa pamoja kuhusu namNa
ya kujua yupi ni jogoo au tetea bora.
Mara nyingi wakati unafanya uchaguzi wa jogoo
kwa ajili ya kufuga ni lazima uangalie, jogoo ambaye atakuwa na sifa zifuatao;
1.
SIFA ZA JOGOO BORA
- Awe na umbo kubwa.
- Awe na ukiko nzuri usioangukia upande mmoja.
- Awe mchangamfu.
- Apende kuwa na himaya yake. Sifa hii utaigundua pindi ukimjazia wapinzani, atakuwa anapigana badala ya kufuata matetea.
2. SIFA ZA TETEA BORA
- Awe na umbo kubwa.
- Awe na uwezo wa kuatamia.
- Awe na uwezo wa kulea vizuri (high mothering
ability).
- Aweze kutaga mayai ya kutosha.
MBINU ZA KUTAMBUA JOGOO NA TETEA BORA KWA AJILI YA KUFUGA.
Reviewed by BENSON
on
September 15, 2017
Rating:
miminaitajikufugakuku
ReplyDeleteWa kienyeji