MBINU BORA ZA UFUGAJI WA KWARE.
Siku ya leo tutakwenda kujikita zaidi kwa kuangalia ufugaji wa
kwale na faida zake. Kwale ni jamii ya ndege wa porini ambao kwa sasa hufugwa
sana majumbani kutokana na kugungulika kua ni ndege wenye faida, hasa mayai yake kua na faida nyingi
mwilini.
kwale hutaga mayai kama kuku, kanga au bata, pia kwale hua na umbile dogo 280- 300g.
kwale hutaga mayai kama kuku, kanga au bata, pia kwale hua na umbile dogo 280- 300g.
KANUNI ZA UTUNZAJI WA VIFARANGA VYA KWALE.
vifaranga wa kwale hutakiwa kutunzwa vizuri kama ambavyo vifaranga wa ndege wengine hutakiwa kutunzwa.
vifaranga wa kwale hutakiwa kutunzwa vizuri kama ambavyo vifaranga wa ndege wengine hutakiwa kutunzwa.
·
Hivyo unatakiwa kuandaa mazingira mazuri kabla ya vifaranga wa
kwale hawajeletwa bandani.
·
Siku ya kwanza wanapofika unatakiwa kuwapa GLUCOSE
ukiiichanganya kwenye maji, pakti moja kwa lita 20 za maji.
·
Baada ya masaa 2 unaweza kuwakea chakula kilicho andaliwa maalum
kwaajili ya vifaranga.
·
Siku ya pili hadi tano unatakiwa kuwawekea amin total kwenye
maji, na uwape maji yasiyo changanywa kitu sita na kuendelea.
·
Pia watoto hutakiwa kuwapa joto unaweza kutumia bulb au
chemri au jiko la mkaa kulingana na uwezo wako, vifaranga hutakiwa kupatiwa
joto kwa masaa 24 ndani ya siku 7.
·
Siku ya 15 -21 uhitaji wa joto utapungua unaweza kuwapa joto
wakati wa usiku tu, ila hiki ndio kipindi ambacho vifaranga hula sana hivyo
wanatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha pia.
·
kuanzia siku ya 21na kuendelea nikipindi ambacho kwale hawaitaji
joto hivyo chakula na maji ya kutosha ndio muhimu kwa kipindi hiki.
KUANZA KUTAGA
Kwale wakipewa huduma nzuri, chakula na maji ya kutosha huanza kutaga wanapofikisha wiki ya sita kuelekea ya saba ,kwa kipindi hicho utaanza kuona kwale wakianza kutaga mayai kila siku , kwa wastani kwale mmoja anauwezo wa kutaga mayai 250- 300 kwa mwaka wakipewa chakula stahiki.
MAGONJWA
Kwa bahati nzuri kwale ni ndege ambaye hua na kinga sana mwilini kwake na sio rahisi sana kwa kwale kupata magonjwa kirahisi, na pia pindi wanapo ugua ni rahisi pia kutibika.

Hivyo ni muhimu kuweka mazingira na banda safi ili kuweza kuzuia magonjwa kama typhoid, mafua na kuharisha. Pia kwakua kwale ni jamii ya ndege kama alivyo kuku hivyo utakiwa kupewa chanjo ili kuweza kuzuia magonjwa.
·
Siku ya 7 wapatie chanjo ya kideri/new castle ambayo inapatika
kalibia maduka yote ya dawa za mifugo.
·
Siku ya 14 unatakiwa kuwapa chanjo ya GUMBORO ambayo pia
hupatikana katika maduka ya dawa za mifugo.
·
Siku ya 21 unatakiwa kurudia kuwapa chanjo ya kideri/new
castle
·
Siku ya 35 unatakiwa kuwapa chanjo ya ndui/ fowl pox
FAIDA ZA KUFUGA KWALE
Ufugaji wa kwale hua na faida ukilinganisha na ufugaji wa ndege wengine
Ufugaji wa kwale hua na faida ukilinganisha na ufugaji wa ndege wengine
·
Chanzo cha kipato kwa wafugaji.
·
Hawana gharama sana katika suala kufuga.
·
Hawataji utaalam sana katika kuwafuga.
·
mayai yake ni tiba ya magonjwa mbalimbali.
·
mayai yake hayakosi soko.
MBINU BORA ZA UFUGAJI WA KWARE.
Reviewed by BENSON
on
September 14, 2017
Rating:
No comments