JINSI (ALOE VERA) INAVYOWEZA KUTIBU MAGONJWA YA KUKU.
Shubiri mwitu (Aloe VERA) ni mmea ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu
magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza
sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi.
Na kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu
baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya
kuweka umuhimu kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea.
Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa
coccidiosis na kwa kiasi fulani Newcastle disease. Tafiti zilifanyika kwa kutumia
mti huu kutibu ugonjwa coccidiosis ambao mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala
wa dawa za viwandani.
Maji maji ya mmea huu yanauwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha
majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya
kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali.Mmea wa aloe vera unaweza
kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake
na unakubali maeneo karibu yote.
Majina ya mmea huu kulingana na baadhi ya makabila na kimataifa
Jina la Mmea
|
Lugha
|
Shubiri
mwitu
|
Kiswahili
|
Mkankiruri
|
Kinyaturu
|
Itembwe
|
Kigogo
|
Ibhata
|
Kinyiha
|
Litembwetembwe
|
Kihehe
|
Koli
|
Kikaguru/Kinguu
|
Aloe
|
Kiingereza
|
Aloe
vera
|
Kisayansi
|
Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kuku Kulingana na tafiti zilizofanywa na Bejar (Chuo kikuu cha Kilimo na Misitu cha Samar) na Clapo (Chuo Kikuu cha Ufilipino Mashariki) inaonyesha kuwa ziada ya Shubiri mwitu kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka.
Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na
lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yanauwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na
kuongeza uzito wa ukilinganisha na wale ambao hawajapewa.
Uandaaji wa Shubiri mwitu Kunjwa:
Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe
vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3
kutegemeana na idadi ya kuku. Viache humo kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha
maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi
unakuwa ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku
90 kama unakuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi.
Vidonda:
Kuku wenye vidonda kama kwa ugonjwa
wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande
vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na
kuvichekecha ili upate unga laini. Uanike na kisha tunza vizuri tayari kwa
kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na
sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye
vidonda hivyo.
JINSI (ALOE VERA) INAVYOWEZA KUTIBU MAGONJWA YA KUKU.
Reviewed by BENSON
on
September 16, 2017
Rating:
Asante kwa somo zuri, ntaenda kuwaandalia hii dawa kuku wangu
ReplyDeleteNaweza kupata aloevera halisi na kwa be I gani
ReplyDelete