FAIDIKA KWA KULIMA KILIMO BORA CHA MCHICHA
Mchicha ni mboga za majani pia maua yake hutumika katika
kutengeneza mchuzi rojorojo. Mbegu za mchicha ni chakula safi kwa watoto
wachanga. Mbegu husagwa na kutengenezwa uji na zaidi ya hayo pia mchicha huweza
kumwongezea mkulima kipato hasa pale mkulima huyo akijikita katika kilimo hiki.
MAHITAJI YA HALI YA HEWA KWAAJILI YA KULIMA MCHICHA.
Mchicha
unahitaji maji ya kutosha katika kipindi chake chote cha ukuaji hadi kuvuna.
Vilevile mchicha huhitaji udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye kuhifadhi
maji.
UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Tengeneza shamba la mchicha kwa kutifua ardhi na kulainisha udongo wenye kina
cha sentimeta thelathini. Weka mbolea ya samadi debe moja katika kila mita moja
ya mraba. Panda mchicha katika matuta yenye upana wa 90cm-100cm.
AINA ZA MBEGU ZIFAAZO KWA KILIMO HIKI CHA MCHICHA
1.
Amaranthus hybridus huu ni mchicha wenye majani mekundu na mbegu
zake ni nyeusi.
2.
Amarantus africana ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu
zake ni ni nyeusi.
3.
Amaranthus hypochondriacus ni mchicha wenye majani ya kijani na
mbegu zake ni njano hasa mbegu zake hutumika kutengeneza uji wa watoto wachanga
4.
Amaranthus dubius ni mchicha wa kienyeji na Aspinosus ni mchicha
wenye miba mingi.
UPANDAJI
·
Changanya mbegu za mchicha na mchanga kwa uwiano wa 1:3, 1:4,
1:5 au 1:6 ili kurahisisha upandaji.
·
Mchicha upandwe katika
tuta kwa mistari yenye nafasi ya sentimita thelathini.
·
Funika mbegu kwa kutumia udongo uliolaini na tandaza nyasi kavu
baada ya kupanda ili kutunza unyevunyevu na toa matandazo baada ya siku tatu
hadi tano tangu siku ya kupanda.
·
Pandikiza mchicha kwa nafasi ya sentimeta kumi na tano kwa
ishirini.
·
Mwagilia maji ya kutosha.
KUKUZIA
Tumia mbolea ya samadi iliyolowekwa kwenye maji kwa muda wa masaa ishirini na
nne kumwagilia mchicha wako ili kupata mavuno mengi zaidi. Tumia kiasi cha debe
moja kwa kila mita moja ya mraba.
NAMNA YA KUDHITI WADUDU WAHARIBIFU
Adui
mkubwa wa mchicha ni wadudu aina ya mafuta au kitaalamu zaidi huitwa spinach
aphids ambao hufyonza utomvu wa mchicha na kusababisha majani kujikunja ,
mchicha kusinyaa na kunyauka. Kudhibiti wadudu hawa mwagilia mchicha wako
kutumia chombo kinachotoa maji mithili ya mvua kitaalamu kinaitwa
"watering can" ili kuwadondosha wadudu hao.
Wadudu
wengine ni kitambazi ambacho hula majani ndani kwa ndani hivyo tumia mwarobani
kunyunyuzia majani ili kuwaua wadudu hao waharibifu.
MAVUNO
Mchicha huwa tayari kuvunwa baada ya majuma 3 hadi 6 tangu
kupandwa au kupandikizwa. Uvunaji huweza kuendelea kwa muda wa miezi 2 hadi 3
kutegemeana na namna utakavyoamua kuuvuna mchicha wako.
KIASI CHA MAVUNO
Kila
mita moja ya mraba huzalisha kiasi cha 4kg hadi 5kg za mchicha. Hii inamaanisha
kuwa utapata kiasi cha tani 20 hadi 40 kwa hekta moja ya mchicha.
NAMNA YA
KUHIFADHI MCHICHA KWA SIKU NYINGI ZAIDI
Baada ya
kuvuna funga mashina ya mchicha na weka katika chombo chenye maji kwa kufanya
hivyo unaweza kuhifadhi mchicha kwa muda wa masaa 24 yaani siku moja.
Ili kuhifadhi mchicha kwa zaidi ya miezi 4 fanya kama
ifuatavyo:-
1. Vuna mchicha
wako kisha usafishe vizuri
2. Funga katika mafungu.
3.
Chemsha maji mpaka yachemke.
4.
Tumbukiza mafungu ya
mchicha katika maji yanayochemka kwa muda wa dakika 1 hadi 2.
5.
Kausha vizuri chini ya kivuli na utunze mchicha wako katika
sehemu isiyo na unyevunyevu.
6.
Hapo utakuwa na uhakika wa kuuza mchicha wako supermarket na
kuusafirisha hata nje ya nchi.
FAIDIKA KWA KULIMA KILIMO BORA CHA MCHICHA
Reviewed by BENSON
on
September 05, 2017
Rating:
No comments