KANUNI BORA ZA ULISHAJI WA KUKU WA MAYAI.
Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa
walishwe chakula bora kwa utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea
hawatotaga vizuri. Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri kama
ifuatavyo:-
UMRI WA WIKI 1 -2
Katika umri huu wanapewa chakula aina ya "Super Starter" kwa
ajili ya kuwatengenezea kinga mbadala ili waweze kuhimili mikiki mikiki ya
vijidudu vya magonjwa kadri wanavyoendelea kukua, wanapewa chakula hicho kwa
kiwango maalum kama ifuatavyo:-
Wiki ya 1: Gramu 12 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 2: Gramu 22 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 3 - 8
Hapa wanakuwa bado ni vifaranga na wanapewa chakula aina ya "Chick
Starter" kwa ajili ya kuendelea kuwajenga miili yao waweze kupoekea
virutubisho vizuri, hii inatokana na kwamba kuna baadhi ya viinilishe vinafanya
kazi ya kumeng'enya chakula na kupatikana viinilishe vingine, kwahiyo
vikikosekana katika mwili wa kuku basi hata wale chakula gani bora, hawawezi
kutoa mazao bora, lakini kwa kuwapa "Chick Starter" itawapelekea kuwa
na virutubisho hivyo muhimu. Kiwango na ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 3: Gram 27 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 4: Gram 32 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 5: Gram 38 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 6: Gram 42 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 7: Gram 46 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 8: Gram 50 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 9 - 18
Katika umri huu kuku wanapewa chakula aina ya "Grower Mash"
kwa ajili ya kuwakuza na kuwajenga mfumo wa uzazi kwa maandalizi ya utagaji.
Kiwango cha chakula kinategemea na wiki kama ifuatavyo:-
Wiki ya 9: Gram 56 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 10: Gram 62 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 11: Gram 64 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 12: Gram 66 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 13: Gram 68 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 14: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 15: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 16: Gram 80 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 17: Gram 82 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 18: Gram 88 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 19 - 40
Huu ni umri ambao kuku wanataga kwa kiwango kikubwa sana (85% hadi 100%)
hali ambayo inawafanya kutumia nguvu nyingi mno, hivyo hupewa chakula aina ya
"Layers Phase 1" kwa ajili ya kufidia nguvu ya ziada
wanayotumia ili waendelee kutaga kwa kiwango hichohicho. Ulishaji wake ni kama
ifuatavyo:-
Wiki ya 19: Gram 92 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 20: Gram 102 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 21: Gram 108 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 22: Gram 114 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 23: Gram 116 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 24: Gram 120 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 25 - 40: Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja
UMRI WA WIKI 41 - 80
Katika umri huu kuku wanakuwa wameanza kuchoka na huanza kutaga kwa kiwango
cha kawaida (65% hadi 75%) hivyo hupewa chakula aina ya "Layers Phase 2"
kwa ajili kuendeleza (maintain) kiwango chao hicho kwa muda mrefu. Kiwango chao
ni "Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja".
NB: Kuanzia wiki 81 na kuendelea unaweza kuwauza na kuweka kuku wengine.
KANUNI BORA ZA ULISHAJI WA KUKU WA MAYAI.
Reviewed by BENSON
on
September 13, 2017
Rating:
No comments