MAMBO YA MSINGI KUZINGATIA KABLA YA KUANZA KUJENGA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI.
Ni jambo muhimu
sana kuchagua eneo zuri ili kurahisisha na kufanikisha kwa urahisi kazi
ya kufuga samaki. Si kila eneo la ardhi hufaa kwa kazi ya kufuga samaki.
Eneo zuri kwa ufugaji samaki ni eneo lenye maji ya kutosha na ya kuaminika,
udongo unaotuamisha maji (mfinyanzi), ikiwezekana pawepo mtelemko wa kiasi.
Pia eneo
hilo la kufugia samaki lazima liwe na:
1.
Maji ya kutosha ni
yale yanayoweza kujaza bwawa lako ndani ya siku chache. Pia maji hayo yawe ni
ya kuaminika ili wakati unapoyahitaji, yapatikane. Chanzo chaweza kuwa mto au
chemichemi. (Maji ya mvua hayaaminiki, wakati yale ya bomba ni ya ghali sana
kutokana na kuyalipia kwa mamlaka husika)
2.
Udongo unaofaa ni
ule unaotuamisha maji, kama vile wa mfinyanzi au mchanganyiko wa mfinyanzi na
tifutifu. Mchanga mtupu haufai kwani huruhusu maji kunywea kirahisi.
3.
Mteremko ni vema
usiwe mkali sana, ila uwezeshe maji kutiririka kuingia na kutoka bwawani. Eneo
la tambarare kabisa si zuri sana, kwani utafanya uchimbaji wa bwawa kuwa kama
kisima na haitakuwa rahisi kuondoa maji toka bwawani itakapo
hitajika ambalo si zuri kwa ufugaji bora wa samaki.
4.
Ni vizuri eneo
liwe karibu na nyumbani ili kudhibiti wezi na maadui wa samaki, pia huwezesha
kutoa huduma kwa urahisi.
CHAGUO LA UMBO NA UKUBWA WA BWAWA
1.
Umbo na ukubwa wa
bwawa hutegemea sura na mwinuko wa eneo husika na eneo alilonalo mfugaji.
2.
Kwa kawaida umbo
lolote hufaa kwa uchimbaji wa bwawa, lakini, ili kurahisisha uvunaji, umbo
mraba au mstatili upendekezwa zaidi.
3.
Vile vile, ukubwa
wa bwawa hutegemea ukubwa wa eneo husika, uwingi wa maji na uwezo wa mkulima.
4.
Bali, ili
kupata pato la kuridhisha na kurahisisha utoaji huduma kama vile kulisha,
inapendekezwa kuwa ukubwa wa bwawa ni vema liwe na upana wa kati ya mita 10 na
mita 20 na urefu wa kati ya mita 20 na mita 30. Umbo la mraba au mstatili
huvutuia zaidi.
Hatua za muhimu katika uchimbaji wa bwawa
·
Fyeka mahali pa
kujenga bwawa.
·
Pima bwawa na weka
mambo.
·
Ondoa udongo wa
juu (mbolea, mchanga, mizizi n.k.) na weka pembeni.
·
Chimba msingi wa
kuta; upana futi 1 na kina futi 1½.
·
Jaza huo msingi
kwa udongo wa mfinyanzi na kuushindilia. Hii itasaidia kupunguza kunywea kwa
maji.
· Anza kuchimba
bwawa na kujenga kuta kwa kutumia udongo tu (bila mchanga, mawe, miti, mizizi
n.k.) ili kupunguza kunywea kwa maji kutoka bwawani baada ya kulijaza.
· Shindilia
kikamilifu udongo unaowekwa kwenye kuta.
· Jaribu kusawazisha
juu ya kuta na chonga kuta ziwe na mtelemko wa kiasi, zisiwe wima kwani
zitamomonyoka kirahisi.
· Chonga sakafu ya
bwawa kwa kuiwekea mteremko wa kiasi kutoka upande wenye kina kifupi kwenda
upande wenye kina kirefu..
· Weka bomba la
kuingizia maji na bomba la kuondolea maji bwawani.
· Rudishia udongo wa
juu uliouondoa hapo awali kwenye kuta za bwawa.
· Panda majani
yanayotambaa kama mbudu ukutani kuzuia mmomonyoko.
· Jenga wigo wa
kuweka mbolea ya samadi au Mbuji ndani yake
· Jenga uzio,
seng’enge au panda miti yenye miba kuzunguka bwawa kuzuia maadui wa samaki
kuingia bwawani.
· Tawanya mbolea na
majivu chini ya bwawa ili kuua wadudu wanaoweza kuwamo ndani ya bwawa kabla ya
samaki kupandwa bwawani.
· Baada ya hatua
hizo kukamilika, sasa jaza maji bwawani.
MAMBO YA MSINGI KUZINGATIA KABLA YA KUANZA KUJENGA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI.
Reviewed by BENSON
on
September 17, 2017
Rating:
No comments