JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI
Kuna njia mbali mbali waweza kuepuka kutumia mboga mboga
zinazolimwa usikokujua na kuepuka kujiingiza katika afya mbaya kwa matumizi ya
kemikali za kuulia wadudu na magonjwa zinazotumika katika ukuzaji wa mboga
mboga.
Aina za bustani
1. Unaweza tumia makopo amabayo mara nyingi hutumika kupanda
maua kando kando ya nyumba
2. Unaweza tumia gunia la sandarusi kubwa..
3. Unaweza tengeneza key hole garden ( bustani ya tundu la
Ufunguo)
Bustani Ya Makopo/Ndoo
Vifaa
Udongo, makopo/ndoo, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk),
Mbole ya samadi iliooza vizuri.
Udongo - Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia
virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk - Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia
kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na
hewa.
Mbolea ya samadi - Kutoa virutubisho kwa mmea
Hatua za utengenezaji.
- Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole
katika uwiano wa 5:2:1.
5 udongo, 2 samadi,
1 Mchanga/rice husk
- Toboa makopo yako kwa chini ili kuzuia maji kubaki kwa
wingi kwenye kupo na weka pamba kwenye matundu uliotoboa.
- Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye makapo/ndoo. Hapo
utakuwa tayar kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote.
- Kuepuka uchafuzi wa
mazingira kwa maji yanayo toka kwenye makopo endapo makopo hayo yapo kwene
simenti, weka makopo/ndoo hayo juu sahani/besen
Uangalizi.
- Mwagilia mboga yako mara tu baada ya kupanda na kuendelea
ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa
mboga unaweza tumia dawa zisizo za kemikali za viwandani kama vile majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na
tumbaku.
- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi
yako ni kumwagilia tu.
- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya
mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii
inategemeana ni aina gani ya mboga)
Faidi
- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
- Gharama za uhitaji wa mboga za majani.
SEHEMU YA PILI
BUSTANI YA GUNIA
Vifaa
Udongo, Kokoto (mawe madogo madogo), Gunia, mchanga/Pumba za
mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri, mti/mbao na kopo dogo
(sadolini).
Udongo - Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia
virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk - Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia
kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na
hewa.
Kokoto - Kusadia maji
kupita ndani ya gunia toka juu hadi chini
Mbolea ya samadi - Kutoa virutubisho kwa mmea
mti/Mbao - Kusaidia
gunia lako kusimama vyema/ imara
Hatua za utengenezaji.
(i) Changanya udongo wako na mchanga/rice husk
pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
5 udongo, 2
samadi, 1 Mchanga/rice husk.
(ii) Toboa kopo
lako na ondoa kitako ili kuweka uwazi pande zote mbili (juu na chini)
(iii) Weka mti/ubao
katikati ya gunia ukiuchimbia ardhini kisha weka kopo lako katikati ya mti/mbao
hiyo na lijaze kokoto
(iv) Weka udongo
uliochanganywa vizur kwenye gunia lako ukilizunguka kopo lenye kokoto hadi
kufikia kimo cha kopo. Baada ya hapo ondoa kopo na hakikisha kokoto zinabaki
zikizungukwa na udongo.
(v) Weka kopo juu ya
kokoto zilizozungukwa na udongo kisha, lijaze kopo hilo na kokoto, rudia kujaza
udongo ukilizunguka kopo hadi kimo cha kopo hilo. Endelea kufanya hivyo (kama
hapo juu) hadi pale gunia lako litakapokuwa limejaa.
(vi) Toboa gunia kwa
kuweka matundu kuzunguka gunia kwa ajili ya kupandia katika umbali sawa
(inategemea na aina ya mboga)
(vii) Hapo utakuwa
tayari kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote juu na pembeni ya gunia
lako
Mboga aina ya letuce (Lactuca sativa)
Mboga aina ya
sukumawiki (Brassica carinata) zikiwa zimepandwa kwenye gunia
Uangalizi.
- Mwagilia mboga yako mara baada tu ya kupanda na kuendelea
ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa
mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na
tumbaku.
- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi
yako ni kumwagilia tu.
- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya
mavuno 2 ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii
inategemeana ni aina gani ya mboga)
Muhimu: Ukitumia miche kwa siku tatu/mbili za mwanzo usije
ogopa kuona miche yako imelala endelea kuimwagilia itasimama tu. Pia katika
umwagiliaji hakikisha unamwaga maji katika kati ya guni pale kulipo na kokoto
ili kuhakikisha maji yanasamba ndani ya gunia hadi chini.
Faidi
- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
- Gharama za uhitaji wa mboga za majani.
- inatumia nafasi ndogo na kutoa kiasi kikubwa cha mboga mboga.
JINSI YA KUTENGENEZA BUSTANI NDOGO NYUMBANI
Reviewed by BENSON
on
November 21, 2017
Rating:
No comments