JIFUNZE KILIMO CHA MATONE (DRIP IRRIGATION) WA GHARAMA NDOGO.
Hii ni njia ya kumwagilia mmea
kwa kutumia tone(matone) la maji kwa muda husika, ambapo bomba dogo huundwa kwa
kuwekewa matundu madogo madogo kwa kuzingatia mmea ulipo kwaajili ya kuupa maji
mmea muda wote.
Umwagiliaji huu unaweza
kuendeshwa kwa mashine au kwa mkono. Umwagiliaji huu pia unaweza fanyika kwa
mazao yaliyo mengi ikiwemo ya mboga mboga, matunda na hata nafaka. Katika
maeneo yaliyo mengi umwagiliaji huu wakulima hupendelea kuufanya kwa mazao ya
matunda na mboga mboga.
FAIDA ZA UMWAGILIAJI WA MATONE
1. Matumizi ya maji ni yenye mafanikio.
2.
Mavuno ni ya uhakika.
3.
Mgawanyo wa maji katika mimea ni
sawa.
4.
Mmonyoko wa udongo ni mdogo sana.
5.
Hupunguza gharama za wasaidizi
shambani.
6.
Huokoa muda.
CHANGAMOTO ZA UMWAGILIAJI WA MATONE
Kama maji yatakayo tumika katika
umwagiliaji yakiwa na chumvi husababisha udongo kuwa na chumvi. Kama
miundombinu haitawekwa sawa upotevu wa maji utakuwa mkubwa.
VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA
UMWAGILIAJI WA MATONE
1. Topografia Huu ni umwagiliaji wenye
mafanikio hakikikisha eneo lako lipo tambarare, hata kama mteremko utawepo uwe
mteremko wa wastani, kufanya mgawanyo wa maji kuwa sawa. Pia zingatia sehemu ya
kuweka chanzo cha maji inaweza kuwa ni pipa liliwekewa miundo mbinu mizuri
miundombinu hiyo kama bomba zilizo sanifiwa vyema kufikia kwenye mmea, pipa au
chanzo chochote cha maji hicho kiwekwe sehemu iliyo inuka ili kufanya maji
yateremke vizuri kwenye bomba mpaka kwenye mmea.
2. Aina ya udongo ni muhimu sana
kujua aina kama ni tifutifu, kichanga au mfinyanzi,hii itakusaidia mkulima
kujua uwezo wa aina husika ya udongo wa kuhifadhi maji ardhini.
3. Mgawanyo wa maji.
Maji ni lazima yawe yenye ubora na maji yawe ya uhakika, kwa kuzingatia hilo
pia topografia ya eneo husika ni iwe tambarare au mteremko kiasi Kuruhusu maji
kugawanyika vyema kwenye mmea kwa kiwango kile kile na spidi ile ile kwa kila
mmea.
3. Kila zao lina nafasi zake katika upandaji hivyo unavyoweka mfumo wa
umwagiliaji hakikisha nafasi unazo weka ziendane na nafasi ya zao husika.
Mfano: JINSI YA KUWEKA MFUMO WA
UMWAGILIAJI SHAMBANI
Vitu vifuatavyo viwepo; vifaa, chanzo cha maji,ukubwa wa shamba.
VIFAA – katika umwagiliaji huu vifaa
vinavyoweza tumika ikiwemo, Chanzo cha maji kinaweza kuwa pipa, hakikisha pipa
hili limetobolewa na kupitisha maji mpaka kwenye bomba ambazo zitakuwa
zimewekwa moja kwa moja kwenye mmea.
Bomba hizi ziwe zimetobolewa
kulingana na nafasi kutoka mmea hadi mmea, na zimewekwa kulingana na mstari
kama mistari ipo kumi na bomba ziwe kumi. Sehemu za mfumo huu wa umwagiliaji.
Vali(valvu) Kazi ya hichi chombo
ni kuruhusu maji yatoke au yasitoke, ni sawa sawa na koki kama wengine
wanavyoita.
Kichujio ni muhimu sana kwani itasaidia kuchuja maji kuzuia uchafu kama
mchanga, nyasi ambazo huenda zikasabibisha matundu yakutolea maji kuziba, hizi
chujio ziwekwe kabla ya kufungwa bomba za kupeleka maji kwenye mmea.
Emmita Haya ndio matundu ambayo yanapeleka maji kwenye mmea, kwa kawaida hutoa
maji kwa muda wa saa moja kwa maji lita 4 kwa gallon moja la maji.
Uendeshaji wa mfumo huu wa
umwagiliaji
1.
Mfumo huu uendeshwe kwa
kuzingatia maji yanafika katika mmea husika kwa kiwango kile kile kwa mimea
yote
2.
Hakikisha hakuna upotevu wa maji
kama bomba zinavuja hakikisha hazivuji. •Mfumo huu kuwa wenye mafanikio yapaswa
ukaguzi wa mara kwa mara ili kuangalia unavyo fanya kazi.
3.
Hakikisha maji yanafika katika
mmea kama inavyotakiwa. Kabla hauja upeleka katika utekelezaji mfumo huu
shambani chora kwanza ramani katika katika karatasi halafu nenda ukauweke
shambani.
JIFUNZE KILIMO CHA MATONE (DRIP IRRIGATION) WA GHARAMA NDOGO.
Reviewed by BENSON
on
September 19, 2017
Rating:
gharama za kuandaa miundombinu hii kwa ekari moja ni kiasi gani kwa wastani
ReplyDeleteNaomba kujua gharama ya kuweka me undombinu kwa ekari moja
ReplyDelete