ZIFAHAMU TOFAUTI YA ASALI YA NYUKI WADOGO NA ASALI YA NYUKI WAKUBWA
Watu wengi huwa tunatumia asali pasipo kujua
wametokana na asali wa aina gani, hivyo kila asali ambayo unaitumia kuanzia leo
ni lazima ujue wanatakona na nyuki wa aina gani. Asali za NYUKI WAKUBWA na WADOGO zina
tofautiana katika mambo kadhaa na hvyo ni muhimu kujua tofauti hizo kabla
hujanunua ili kua na uhakika.
NYUKI WADOGO
1. Ni nyepesi zaidi kwani
ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 24
2. Ina ladha ya UCHACHU
ingawa ni tamu sana.
3. Mara nyingi ina rangi
ya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoenda kwenye WEUSI
NYUKI WAKUBWA
1. Ni nzito kuliko ya
nyuki wadogo kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 17 hadi 20.
2. Ni tamu moja kwa moja
bila kua na ladha ya uchachu kama nyuki wadogo
3. Ina rangi nyingi
kuanzia NYEUPE, NYANO, KAHAWIA ILIYOPOA, KAHAWIA ILIYOKOZA n.k
Hizo ni tofauti za muhimu
kuzijua kwani zitakuwezesha kupata asali unayoitaka na kuepuka kuibiwa
ZIFAHAMU TOFAUTI YA ASALI YA NYUKI WADOGO NA ASALI YA NYUKI WAKUBWA
Reviewed by BENSON
on
September 20, 2017
Rating:
No comments